Kigamboni: Ndugulile tutakukumbuka kwa kuipigania ardhi yetu isiuzwe kwa mabeberu na akina Methew wa CHADEMA

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wananchi wa Kigamboni wanasema hata kama mbunge wa sasa wa jimbo hilo Dkt. Ndugulile hatapitishwa na CCM kugombea bado atakumbukwa daima na wapiga kura.

Wamesema Dkt. Ndugulile alisimama kidete kuwatetea barazani na bungeni ili manyang'au wasipole ardhi yao.
Wamedai waziri mstaafu Prof Tibaijuka na madiwani wakiongozwa na Selemani Methew ambaye kwa sasa ni kiongozi mkubwa wa CHADEMA walipanga kuiuza Kigamboni kwa mabeberu na walipelekwa hadi Ulaya kutalii lakini mbunge Ndugulile alikataa katakata kuwa sehemu ya uchafu huo.

Wananchi wamesisitiza kuwa wako pamoja na Dkt. Ndugulile kwani " usione vyaelea vimeundwa"

Nawatakia Sabato yenye baraka

Maendeleo hayana vyama!
 
Ana bahati mbaya safari hii ,Mtoto Pendwa kaja!!
 
Mkuu naona umetafuta weeeee utakapomuona mtu wa Chadema ulipompata ukaanzisha uzi chap chap. Huko Kigamboni kwanza liccm linaenda kupasuka na upo uwezekano Ndugulile akahamia kule kwingine na akashinda ubunge. Yani kama ni kufeli hesabu basi CCM imefeli Kawe, Ubungo na Kigamboni.
 
Ana bahati mbaya safari hii ,Mtoto Pendwa kaja!!
Mtoto pendwa alikosea sana kusema maneno haya ambayo baba yake sasa amegundua yame mfarakanisha na viongozi wenzake wakati kumbe yeye ndio anawahitaji zaidi.
Your browser is not able to display this video.
 
Hata Selemani Methew alikuwa CCM!

Maendeleo hayana vyama!
 
ma ccm ya ajabu sana, yaani unamuacha PhD holder(Dr Ndugulile) halafu uende kuchukua vyeti fake (Makonda sijui Bashite)???!!!.

hiyo ni akili au matope??
 
Natamani ¾ ya wabunge wawe wapya!

Bila kujali udhaifu Wa anayeshinda au umuhimu Wa aliyepo ninataka iwe vile.
 
ma ccm ya ajabu sana, yaani unamuacha PhD holder(Dr Ndugulile) halafu uende kuchukua vyeti fake (Makonda sijui Bashite)???!!!.

hiyo ni akili au matope??
Ndugulile ni daktari wa binadamu siyo Falsafa!
 
Uchaguzi huru ndani ya chama

Breaking News !


Dr. Faustine Engelbert Ndugulile ashinda kura za maoni za ndani ya chama cha CCM jimbo la Kigamboni jijini Dar es Sakaam.

Kura za maoni za wajumbe halali zilikuwa 399 hakuna kura iliyoharibika na Dr. Faustine Engelbert Ndugulile amefanikiwa kupata kura 190 za wajumbe hao wa mkutano wa wilaya ya Kigamboni..

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kutumbuliwa kwa kilichoitwa 'tamaa' isiyokubalika ndani ya CCM Mpya Bw. Paul Christian Makonda amepata kura 122.
 
...kampeni zilianza mapema...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…