Nina kubaliana na wewe lazima serikali lazima ishirikishe wananchi wake.Kwenye projects kama hizi serikali wanatoa kiwanja wanapewa percent fulani, hizo percent ndio wanaweza kuziuza kwa wananchi.Lakini kusema watanzania kushirikishwa kwenye hiyo project kwa 100pc ni ngumu kutoka na ukubwa hiyo project na kuna vipaumbele vingine.Uzuri wa mji utakusaidia nini? lazima ujenge uchumi kwa kuwashirikisha wananchi wako na si vinginevyo. matokeo yake watanzania wataishia kufagia katika hiyo mitaa unayoiona kwenye hizo picha. tunarudi kule kule tulikotoka.
Kiranga,
Nasema hivi: Je uliona wapi mji mpya unajengwa bila Masterplan? Tuanzie hapo, umeletewa Concept City unasema unataaka kuona kitu concrete, hata zege kabla ya kumwagwa kunakuwa na design stage.
Mambo mengine tuache ushabiki usio na msingi.
UDOM ilijengwa na inaendelea kujengwa na hata kama CDA walishindwa kazi Ujenzi wa UDOM na mji mpya wa Kigamboni ni ktu kizuri na ndiyo maana narudia kusema hii wanaochukizwa na hatua hii kamba ya kujinyongea ipo. hata kama itachukuwa karne moja kujenga kwa uwezo wetu wenyewe ni bora ifanyike hivyo. Nimechoshwa na kila kukicha hakuna kizuri tunachoweza kukifanya wenyewe mpaka kiwe kimefanywa na wengine.
Wengine wamediriki hata kusema ujenzi wa UDOM umeletwa kutoka nje. Kazi kweli kweli.
Nadhani lile somo la siasa halikueleweka enzi zile tunazungumzia ubepari. Inanishangaza kuona watu wanahoji nani watafaidika na mradi huu? Wakuu Tanzania inaendeshwa kibepari and we are in it. Kwa hiyo ni hela yako tu!
Hamna lolote.
pole kaka naona unaongea kwa uchungu sana
lakini hakuna jinsi, BATCH yao ya kwanza ya CIA wa KITANZANIA ndio mwaka huu inatoka UDOM, na vijana wanapikwa kuikana nchi yao yenyewe na ndio watakuwa wakaaazi wa huo mji mpya, nia na malengo makuu ni kukama URANIUM ya Tanzania iwe mikononi mwao, wanataka kuitengeneza hii nchi kiasi kwamba hata raisi awe nani wao wanakuwa na link nzuri mno ya information
hii nchi imeshauzwa
Dubai ilishauzwa kwa wazungu muda mwingi, nenda pale ukaone ilivyo, bombaaa...sisi tusiopenda kuuza tubakie na ardhi, tutakula mchanga. sasaivi makampuni ya magaribi yamejaa Dubai, yananunua hadi ardhi na kujenga magorofa ya ajabu, wauzile watu wa dubai kama hawafaidiki na hilo!