Serikali yenye kutenda sawa ingechukua hatua ya kuwalipa watakaoathirika uwekaji wa miundobinu kama barabara,mitaro ,madaraja ,shule,Hospitali ,umeme,maji na kwa ujumla vitu vyote amabvyo kiutendaji ni shughuli ya Serikali ,huku ikiweka miongozo ya aina ya mji unaofaa kuwa mahala hapo na ikaacha soko huru la biashara na maendeleo itawale shughuli husika na si kufanya udalali, ununuzi na uuzaji wa Ardhi ya wananchi kwa mbinu ya eti ujenzi wa Mjimpya.
Na mbaya zaidi wanaendesha zoezi hili kifisadi ,wameshindwa kufuata Sheria na wanachokifanya ni kuwatapeli wananchi-Nenda Kibada -Kigamboni utayasika na kujionea.