Kigamboni New City Master Plan

Kigamboni New City Master Plan

Kudadeki..wabongo tunapenda vitu vya kufikirika.....tunashindwa hata kutunza hivi tulivyonavyo...tutaweza hayo maghorofa?

Sisi wabongo wengi wetu tuna asili ya uchafu..utakuta mtu kajenga ghorofa kwenye slums......Yaani hiyo Kigamboni..its too good to be in bongo..
chini ya serikali ya JK yote haya yanawezekana aisee
 
Naungamkono hoja hii nchi imeshauzwa kweli. ila ni lazima sisi tuwatengezee njia watoto wetu na ndugu zetu wanaokuja miaka ya mbele. na ili tufanikiwe hilo hatutakiwi kulala mpaka kieleweke.
 
Naungamkono hoja hii nchi imeshauzwa kweli. ila ni lazima sisi tuwatengezee njia watoto wetu na ndugu zetu wanaokuja miaka ya mbele. na ili tufanikiwe hilo hatutakiwi kulala mpaka kieleweke.

haya unayoyasema tueleze unayatekeleza vipi kwa vitendo maana wabongo kwa ngonjera hatujambo.
 
ha ha ha, hii clip ni nzuri kweli kweli kwa kuitazama, hivi katika nchi ambamo kuna shule zisizo na madawati, watoto wanakaa chini na wengine kusomea chini ya miti, katika nchi ambayo serikali yake inakiri kwamba haiwezekani kusomesha watoto mpaka form six bure, katika nchi ambayo wamama wanajifungulia chini, katika nchi ambayo rais wake ameahidi bajaji kwa wajawazito. Halafu kuna vijitu na degree zao kabisa wanaamini katika hizi njozi, tumeshindwa madogo tutaweza makubwa?

chadema's inferiority complex.....!
 
Huu mradi nimegundua kuwa umesha kamilika, hamna kinacho endelea.
CD ya michoro ilipo toka na kusifiwa sana ndio ukawa mwisho wa huu mradi.
 
Hii ndio nchi yetu BWANA, maneno meeeeengi yasiyo na vitendo.
 
Wenye na akili wanajua, hii ilikuwa maana yake nini?
Usijisumbue na viini macho vya serikali ya JK.
 
Labda inangojea ujenzi wa daraja la Kigamboni (utakaofadhiliwa na NSSF?) ukamilike kwanza
 
Hii Serikali ya CCM mimi nasema inaendeshwa na vihiyo. Haina priorities(vipaumbele)inakurupuka tu kama mlevi aliyetoka usingizini.
Utapangaje kujenga Jiji la Kigamboni wakti Jiji la DAR lenyewe limewashinda kulipangilia hasa upande wa miundombinu kwa maana ya Barabara na mfumo wa maji safi/taka ili kuondoa KERO YA MSONGAMANO WA MAGARI NA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI/SALAMA???

HIZO SHS.BILIONI 94 ANAZOLIPWA DOWANS ZINGEWEZA KUPELEKA KWA UMBALI MKUBWA TU KAMA ZINGEINGIZWA KWENYE MRADI WA KUPANUA BARABARA ZA JIJI.
 
The bottom line is this; the limits of the nation's developments will not surpass that country's leadership capacity.
 
Ule mradi kuwa lauched kipindi kile ulikuwa na maana yake mkuu, kama ilivyokuwa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa mabasi na kusaini kandarasi 5 za barabara kwa wakati mmoja na TanRoads!! Mazingaombwe hayataisha mpaka msanii atoke!!!:twitch::twitch:
 
Mwekezaji wa kichina anayekubali kuweka cha juuuu hajapatikana.

Mimi nimekerwa sana na huu mradi ambao kwa maneno ni mzuri lakini kwetu sisi tulio na maeneo tuliyokatazwa hata kuendeleza inatuuumiza. Nilitaka nifuge ng'ombe wa maziwa kwa hiyo siwezi kuweka mabanda.

SisiEm ninawachukia sana kutokana na ubabaishaji wenu.

Wiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiz mtupu
 
Mradi ulikua ugaramiwe na wamarekani ......mkaanza kuleta mbwembwe ohh nchi imeuzwa ...Bush akajitoa
Sasa utabakia kwenye CD na makaratasi.
 
Mchoro huo ulitoka kipindi cha kampeni nini? Hao ndiyo CCM mabingwa wa propaganda duniani!
 
jamani kigamboni kwa heriiii,wakazi wakigamboni hawajui hatima ya maisha yao baada ya stoporder kuisha watu wanajenga wangine hawajui cha kufanya,mama prof Tiba sijui haoni madudu haya au anataka nini?,
baadhi ya madudu haya hapo
1.mjini wa kigamboni unauzwa na mswada unapeleka bungeni wa mamlaka ya mji wa kigamboni wadau hawajui
2.HII NI KWA MZEE MAGOFULI
  • watadu wako hapa fresh walituletea mashine za kukatisha tiketi wakafunga mpaka leo hazifanyi kazi ila kila wakitaka kula wanaleta mafundi watengeneze,FUATILIA
  • Lile boti la kuokolea lililofunguliwa na raisi la mabilioni lipo tu pale ngombo ya bahari halifanyi kazi,Wandishi pigeni picha mumulize raisi watu anakumbuka ni mwaka jana tu alizindua boti hilo
  • wadau hii najua wengi hawatapenda,jamaani ukikata tiketi pale wakupe kipande cha abiria kwani usipochukua wanarudisha wanauza tena,ndiyo maana ata wanamaliza vyuo vikuu wanagombania pale,Mhe mwakembe upo?
 
Waache watimuliwe kwani huoni hata mbunge wao ametoka kwenye chama cha kifisadi:laugh: madhara ya kupigia kura sisiem watayaona
 
Mimi navyo elewa kuna Development Company ya Marekani inataka kutengeneza mji wa kisasa na wana partner na serikali. Hii ni kitu cha kawaida na huku sio kuuzwa kwa namna yeyote!!. Inabidi tuache tabia ya kufikiri kila development inayofanya na kampuni ya nje ni kuuza nchi kwani serikali haiwezi kufanya kila kitu. Kama itawanufaisha Watanzania je kuna ubaya gani kwa kampuni hii kushirikiana na serikali na kujenga sehemu za kuishi za kisasa, office, hospitali, Hotels, shule etc!!
 
Back
Top Bottom