Kigamboni New City Master Plan

Kigamboni New City Master Plan

waheshimiwa, nafikiri itakuwa nimepitwa kama iliwahi kutolewa hapa.hivi huu mpango tunaosikia kuhusu kujengwa upya kigamboni, na wenyeji kuhamishwa,hatima yetu nini? maana hela zetu za misimu na mpaka sasa hata banda la uwani sijamaliza. na huenda vikangia vijisenti vingine ni busara kuendelea kujenga au bora kusubiri kwanza.? maaana ile plani inavoonekana kwenye mtandao ni big city sijui mjengaji nani maana dododma makao makuu mpaka leo bado!!!!!!, waheshimiwa mnashauri nini.
 
Hapo sasa ila sishangai mana tanzania ndivyo ilivyo
 
usijenge kaka . hawa wanamgojea watu wajenge ili waje kubomoa so cool down tafuta maeneoo mengine yaliyopimwa kaka

Ahsante mkuu,na nimeelimika mnoo!.ahsante mod kwa kuniunganisha huku pia. haya mambo sijui yatakuwaje.naona invisible kashindilia msumari.
 
[h=3][/h][h=2]Thursday, April 7, 2011[/h][h=3]Ujenzi daraja la Kigamboni kuanza[/h]


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), John Msemo (kulia) katika eneo la Kurasini Vijibweni Dar es Salaam, kuhusu ujenzi wa Daraja la Kigamboni eneo hilo. NSSF inatarajia kuanza ujenzi wa Daraja hilo mapema mwaka huu baada ya zabuni kutangazwa na kumpata mhandisi. Daraja hilo litagharimu zaidi ya bilioni 130 hadi kukamilika kwake.
 
jamani mji huu unaanza lini?,maana hatuelewi kila kukicha mambo yanazidi kuwa mabaya,kuna nini? Hapa
 
Mpaka atakapokuja Mwana wa Adamu kuwahukumu wazima na wafu.Au mpaka SISIMU itakapong'olewa madarakani.
 
Hukumbuki ilitoka taarifa hyo kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu Mdau!
 
ile ilikuwa ni gia ya kura kwa hiyo swala la mji mnatakiwa msahau.. mji bila umeme ni sawa an kugawa vyandaria huku umeme ukiwa hakuna an mbu wanaongezeka matokeo yake ni sifuri
 
Nasikia utakuwa wa ki marekani zaidi na wataweka base yao maeneo ya huko
 
Jamani hyo master plan ni kweli ipo na kuna video yake kabsa, kwa kfupi kigambon itakuwa kama NY. Na phase ya kwanza ya ujenz inaanza mwaka huu na ukamilika kamili kwa ujenz ni 2025.
 
ile ilikuwa ni gia ya kura kwa hiyo swala la mji mnatakiwa msahau.. mji bila umeme ni sawa an kugawa vyandaria huku umeme ukiwa hakuna an mbu wanaongezeka matokeo yake ni sifuri
Mkuu umenichekesha sana na hiyo signature yako hapo chini bahasha la jairo lina nini? Kigamboni city is coming mazee believe it
 
The Kigamboni new city master plan is designed to build a core for accommodating new land demand such as residential, commercial, trade and business, industrial, educational and recreational facilities in Dar Es Salaam.

The first purpose is to create well-organized connection between old urban centers and the new city.

The second purpose is to build future-oriented new model city with ICT base and excellent living environment.

The third purpose is to develop urban economic competitiveness through supplying new opportunities in advanced industry fields.

Through the Kigamboni new city project, Tanzania can reinforce the leading position in the African Continent.




Nina Video ya hii master plan toka wizara ya Ardhi si mchezo, pateni picha za hiyo video kwa ufupi.

KigamboniNewCityA_Page_10.jpg

KigamboniNewCityA_Page_04.jpg

KigamboniNewCityA_Page_08.jpg

KigamboniNewCityA_Page_06.jpg

KigamboniNewCityA_Page_09.jpg


makaratasi yataozea ofisini?
 
Last edited by a moderator:
samahani wadau! kama hii kitu imeshapita humu naomba mnionyeshe thread yake!
Kuna watu wanasema mk.wer.e amesha sign mkataba na wazee wa US!
Nimejaribu kuicheki hiyo video kwenye link hapo chini nikachoka kabisa!
Kigamboni New City
 
duh huu mji utakuwa pouwa ingawa wanadai pameuzwa hapa kigamboni!
 
akili fupi za kusema nchi imeuzwa huwa sipendi hata kusikiliza. hata mlimani city mlipiga sana kelele kuwa tumeuza sehemu ya udsm, lakini sasaivi mmejaa pale kusukuma tolori zimejaa vitu mnavyonunua....watu kama ninyi ni wa kuwapuuzia tu, msema mlieee hadi mchoke, lakini kitu ambacho selikali inaona kuwa kinafaa, bora kifanyike tu.

Umeahidiwa 10% siyo!

Kwa akili yako ya kiwerefu kusukuma toroli na kuwa na maduka ya kuuzia dodoki kama walivyoyageuza magodown na viwanda vyetu toka enzi ya Kambarage kuwa Supermaket kwa ajili ya bidhaa toka China na Ulaya kwako ni deal kubwa na Maendeleo siyo!



Acheni ubinafsi ,Elimu yetu,badari,tanesco,Reli,Hospitali na mengineyo mengi yanahitaji pesa nyigi kuyaweka sawa ilikuwezesha Uchumi kusonga mbele na sikupitia Majengo ambayo hakuna Mtanzania wa Kawaida ataweza kuishi humu na kuendesha maisha zaidi ya Mafisadi unaowashabikia na pengine umoja wao!


Serikali yenye kutenda sawa ingechukua hatua ya kuwalipa watakaoathirika uwekaji wa miundobinu kama barabara,mitaro ,madaraja ,shule,Hospitali ,umeme,maji na kwa ujumla vitu vyote amabvyo kiutendaji ni shughuli ya Serikali ,huku ikiweka miongozo ya aina ya mji unaofaa kuwa mahala hapo na ikaacha soko huru la biashara na maendeleo itawale shughuli husika na si kufanya udalali, ununuzi na uuzaji wa Ardhi ya wananchi kwa mbinu ya eti ujenzi wa Mjimpya.

Na mbaya zaidi wanaendesha zoezi hili kifisadi ,wameshindwa kufuata Sheria na wanachokifanya ni kuwatapeli wananchi-Nenda Kibada -Kigamboni utayasika na kujionea.
 
Back
Top Bottom