Kigamboni planning authority

Kigamboni planning authority

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI DARAJA LA KIGAMBONI

Thursday, September 20, 2012



* Aonya 'wenye viwanda' vya kutunga uongo kuacha tabia hiyo na kuelekeza nguvu kwenye maendeleo
* Asema viongozi wa vyama vya upinzani badala ya kupigania maendeleo, wapo tayari nchi iyakose
*Asema tukio la kuwekwa jiwe la msingi ujenzi huo, leo litawanyima usingizi badala ya kufurahi

DAR ES SALAAM, TANZANIA

Rais Jakaya Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 20, 2012, ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Dar es Salaam, huku akiwaonya watu ambao amewaeleza kuwa wanavyo viwanda vya kutunga uongo kuacha tabia hiyo na kuelekeza nguvu kwenye maendeleo.


Aidha, Rais Kikwete amewahakikishia wakazi wote wa Kigamboni ambao wanaondolewa katika maeneo yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa daraja hilo na ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni kuwa watalipwa stahili na haki zao zote.


Daraja hilo la Kigamboni ambalo wazo la kujengwa kwake lilibuniwa kwa mara ya kwanza zaidi ya miaka 30, tokea mwaka 1978, wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, linajengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 214.6 na litakuwa tayari katika muda wa miezi 36 ijayo, ingawa muda huo unaweza kupungua na kubakia miezi 30.


Daraja hilo ambalo litakuwa na urefu wa mita 680 linagharimiwa kwa pamoja na Serikali na Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF ambalo litachangia kiasi cha asilimia 60 na Serikali asilimia 40.


Daraja hilo ambalo litakuwa na barabara sita za kupitisha magari kwa wakati mmoja linajengwa na kampuni mbili za China ambazo ni China Railway Construction Engineering Group na China Railway Major Bridge Engineering Company na mhandisi msimamizi wa ujenzi huo ni Kampuni moja ya Misri.


Daraja hilo linatarajiwa kupunguza adha ya usafiri kati ya Kigamboni na Dar es Salaam ambao kwa sasa unategemea vivuko au boti ndogo, mitumbwi ama wenye magari kulazimika kufanya mzungumo wa kilomita 52.


Kwa uamuzi wa sasa, wavuka kwa miguu ambao watakuwa na njia maalum kwenye daraja hilo pamoja na waendesha baiskeli watavuka bure bila malipo yoyote.


Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali haiwezi kudhulumu wananchi wake na hivyo watu wote ambao wanastahili fidia kutokana na ujenzi wa daraja hilo na mji mpya wa Kigamboni watalipwa haki na stahiki zao.



Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake haitaruhusu mtu yoyote kuzuia ama kuchelewesha miradi ya maendeleo ambayo inalenga kunufaisha watu wengi.


Rais Kikwete pia amewaonya watu ambao wamelifanya suala la kutunga na kusema uongo kama sehemu ya utamaduni wao. “Watu wana viwanda vya kuzalisha uongo. Wanashinda wanasambaza uongo kwenye mitandao, kila mahali. Wamepata hata kusema kuwa mimi nimemuuzia George Bush eneo la Kigamboni. Bush aje kufanya nini Kigamboni?”

Haya yaweza kuwa kejeli kwa madai ya msingi ya wanakigamboni kuwa Sheria haijafutwa na wao kama waathirika na miradi hii hawajahusishwa katika mchakato unaoendelea.
Hakuna mwanakigamboni wanao pinga mradi bali madai yao ya msingi kuhusu masilahi yao kulindwa hayajapewi nafasi.
Haijalishi imetajwa kuwa ni Bush anataka kununua au la!,lakini ukweli ni kwamba wakaazi watarajiwa wa huo mjipya ni wa aina ya BUSH na hata mpango uliopo kwa mujibu wa Ramani unasomeka hivyo kwa kuwa Wakaazi waliopo watahamishwa na Kupelekwa Zoo(Eneo tengefu Karibu na Kibada ili kuwapisha wanene.

Uhalisia wa mpango na ujenzi na majengo yanayotarajiwa kujengwa Kigamboni kwa mujibu wa Mpango wenyewe hata mtoto wa darasa la tano anaweza kung`amua kuwa familia yao haitaweza kuishi maisha ndani ya mji kama ule na kwa maana hiyo wanaona wazi wao lazima waondoke na kwamba kutakuwa na mtu mwingine atakaye kuja kuishi humo(Kigamboni new City)

Wanakigamboni wanataka zoezi zima lifuate sheria na liwe zoezi la wazi na washirikishwe hatua kwa hatua na lisiliwe suala la kisiasa kama Raisi anavyotaka lionekane na madai ya msingi wanakigamboni yaonekane ni hoja dhaifu .

Mapungufu yanazunguka zoezi hili la Mjimpya yamefanyiwa dokezo na Haki ardhi na ingependeza Raisi akapata muda wa kupitia na kufanya mlinganisho na anachoelezwa na wataalamu wa wizara pamoja na waziri mwenyewe(Prof.Tibaijuka).
View attachment THE NEW KIGAMBONI CITY, PROSPECTS AND CHALLENGES(6) 2012.pdf



Rais pia amesema kuwa wapo watu ambao hawapendi maendeleo ya nchi. “Wanatamani kila siku tushindwe kuwaletea wananchi maendeleo.
Maendeleo bila kutenda haki si maendeleo.Tatizo Serikali imebaki kuabudu miungu watu (Wawekezaji)na huku baadhi ya maofisa wakiona Kigamboni mahala pakustaafia kimasilahi kwa kushiriki kwenye uporaji wa Ardhi kwa bei poa na kwa jina la Uwekezaji.
Suala la kuwahamisha watu na kusema unawaletea maendeleo si haki hata kidogo.
Mradi huu ungependeza na wala usingekuwa na Kelele kama Serikali itabaki na Suala la Miundo mbinu na ikawashirikisha watakao athirika na miundo mbinu hiyo na hao wanaowaita wawekezaji wakabaki wanakubaliane na wenye maeneo/ardhi kwa upande mwingine KDA inayotaka kuundwa ikawa msimamizi ilikulinda haki ya Wenye Ardhi na pia kusimamia ujenzi unaoendana na Mpango Wenyewe.

Lakini watakufa kwa kihoro kwa sababu hatutashindwa. Kila tulilosema tutalifanya, litafanyika”.


Amesema kuwa thamani kubwa ya vyama vya siasa ni maendeleo ya wananchi. “Lakini wapo wenzetu ambao wanaudhika wakiona maendeleo. Wanapenda hata daraja hili lisijengwe. Leo hawatalala usingizi. Kazi ya vyama vya siasa ni kuweka maslahi yetu sote mbele.”


Posted by Bashir Nkoromo at 7:43 AM 0 comments Email This
 
Kaka umeongea vizuri zaidi, mimi nikiwa mmoja wa waathirika ki ukweli sijui undani ya mpango huu, naambiwa nitashirikishwa how? je nitaweza kumudu kuishi mji huo mpya na wanangu wakati kipato changu ni chini ya dola moja kwa siku? mji unaojengwa ni kwa ajiri ya wafanyabiashara matajiri, viongozi wa serikali na watu maarufu au ni wetu sisi watu maskini tunaomiliki maeneo haya?

Je wananchi hawa ambao JK alikuwa anawahutubia watakwenda kuishi wapi? maana nina uhakika hawataweza kuishi na wazungu katika mji huu mpya wa kihistoria.
 
Tuendelee kupata maoni ya wananchi mbalimbali.


Source;

www.raiamwema.co.tz/
Nani anasema kweli kuhusu Kigamboni?
Mwandishi Wetu
Toleo la 260
26 Sep 2012
RAIS Jakaya Kikwete amekanusha kutouza ardhi ya Kigamboni kwa George Bush. Sawa, lakini hajakanusha kuuzwa kwa eneo la Kigamboni. Kama halijauzwa kwa Bush basi tuambiwe limeuzwa kwa nani.

Habari hii ya Kigamboni inarejesha suala la Richmond: nani alijua na nani alitaka kuchukua hatua kuzuia mkataba ule usiingiwe.
Leo tunapoambiwa habari ya Kigamboni mradi wa mji mpya uliojaa ubabe na usiri mkubwa tunapata tabu sana kuamini kauli hizi.
Mambo haya yanauma sana kwa wahanga wa zoezi hilo la mradi wa mji mpya Kigamboni. Sisi Kigamboni tunajua tumeuzwa lakini pengine hatuna uhakika tumeuzwa na nani na kwa nani. Mawakala wengi wanapitapita kurubuni wananchi waukubali mradi, tena wengine ni viongozi.

Madiwani wa Kata za Tungi, Vijibweni, Kigamboni-Ferry na Mjimwema wana mahusiano mabaya sana na wananchi wao tangu siku ile walipoonekana kwenye runinga bungeni Dodoma. Wanatuhumiwa kuendesha uwakala wa uuzaji wa Kigamboni. Wapo wengine pia wakijinadi kama wawekezaji wa upanuzi wa bandari, wajenzi wa kiwanda cha samaki, wawekezaji wa mafuta, kuna watoto wa vigogo pia wanarandaranda huku wakitumia majina ya wazazi wao, nk.

Hatua ya kutimuliwa kwa Mbunge wa Kigamboni kwenye Bunge iliwafanya wakazi wa Kigamboni kuamini kuna jambo linaendelea kuhusiana na suala zima la utwaaji wa ardhi ya Kigamboni.
Wananchi hao wa Kigamboni walimtuma Mbunge wao akaukatae mradi wa mji mpya wa Kigamboni bungeni kutokana na kugubikwa na utata, usiri na ubabe. Kitendo cha kumtimua Mheshimiwa Faustine Ndungulile bungeni kilionyesha juhudi za kumshona mdomo na hivyo kuhalalisha dhuluma dhidi ya wakazi wa Kigamboni.

Kama hiyo haitoshi, wakazi wa Kigamboni tuliandaa mkutano mkubwa wa mapokezi ya Mbunge wetu pale uwanja maarufu wa Machava. Walihudhuria wananchi kutoka Pembamnazi, Yaleyale Puna, Kimbiji, Kibugumo, Mwongozo, Gezaulole, Chekeni Mwasonga, Tundwi Songani, Mikwambe, Kibada, Kisarawe II, Mbagala yote hadi Mbande, Chamazi na Mvuti.

Wanachi walikuwa wamechangishana mamilioni ya shilingi kumkabidhi Mbunge huyo kama posho kufidia ile aliyonyimwa kufuatia kutimuliwa bungeni na hivyo kumfanya kukosa posho za vikao. Cha kushangaza sana na kwa masikitiko ya wana-Kigamboni, makaribisho hayo yalisambaratishwa na jeshi la Kamanda Suleiman Kova saa chache kabla ya makaribisho hayo kufanyika.
Lakini kwa mshangao mwingine, kuna viongozi Kigamboni wanapitapita na kujitapa kwamba wao walihusika "kulishawishi" Jeshi la Polisi kusambaratisha makaribisho hayo ya mbunge kwa madai kwamba alikuwa anataka kuwachafulia hali ya hewa kwa kuwahamasisha wananchi kuukataa mradi wa Mji Mpya Kigamboni.

Viongozi hao ni wale mawakala wa mradi ambao wametajwa hapo juu. Hivi katika hali ya kawaida kiongozi wa kata au serikali ya mtaa anapata wapi ujasiri na mamlaka ya kuamrisha Kanda Maalumu bila kuwa na msimamizi huko juu? Hii haiwezi kuingia na kutulia tuli kwenye akili inayofanya kazi maridhawa, vinginevyo itakuwa ni bongolala.

Wakazi wa Kigamboni tumepewa katazo (stop order) la kutoendeleza maeneo yetu tangu Oktoba 2008 kwa hoja kwamba ni eneo la mradi. Ilisemekana kuwa ramani za satellite zilishachukuliwa kubaini kuna nini, wapi, na kwa nani.
Ukweli ni kwamba hakuna mkazi wa Kigamboni aliyeshirikishwa katika zoezi hilo. Na nikiri tu hapa, kwamba hata hicho kilichomo kwenye hiyo ramani hakuna anayejua. Mungu ni mkubwa akatuongoza vema, ramani hiyo maarufu kwa jina la "Kigamboni: The Blue Diamond" ikaonekana kwenye mitandao ya huko kwa George Bush. Ni fafanuzi (documentary) moja inayofanyiwa maelezo (commentary) na mtu mwenye lafudhi ya Kimarekani akisifia kuwa Kigamboni ni lango/kitovu (hub) ya "maendeleo" ya Tanzania. Siwezi kuamini kwamba mwelezaji (commentator) yule ni Mmatengo au Mhaya, na wala si Mndengereko au Mzaramu. Wasamaria wakatuvuta masikio tukaiona hiyo documentary mtandaoni.

Nikueleze tu ndugu msomaji kulikuwa na mwitiko (rush) mkubwa wa kuipata hiyo documentary miongoni mwa sisi wadau wa Kigamboni. Tulikuwa tunanunua hiyo fafanuzi ili kupata taarifa ambayo ni haki yetu kupata lakini wahusika serikalini wakawa wanatuficha. Hata mimi binafsi niliuziwa na msamaria mwema Dar es Salaam na ikawa bidhaa adimu hapa Dodoma.
Hayo ndiyo mazingira yaliyosababisha kujitokeza maneno (uvumi?) kwamba Kigamboni imeuzwa kwa George Bush.
Kwa mshangao wa tulio wengi, mara baada ya nusanusa yao serikalini kugundua kwamba suala hilo liko hadharani kwa haraka sana Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikatoa kilichoitwa TAMKO LA SERIKALI kwenye gazeti la Mwananchi Jumapili moja ya mwaka 2008 lililokataza uendelezaji wa ardhi katika maeneo ya mradi kwa mujibu wa sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007. Katazo hilo lilitakiwa liishie Septemba 2010 ambapo mradi ungekuwa umeanza awamu ya kwanza.

Hadi leo niandikapo makala haya hakuna kinachoendelea ukiachia mbali kuwarudisha nyuma wakazi wa Kigamboni. Tumerudishwa nyuma kwani tunatishwa (intimidated) kwamba chochote tutakachoendeleza kinakula upande wetu. Choo kikianguka usikarabati maana itakula kwako. Na huo wimbo wa fidia kwa mali za watu wa Kigamboni ni nyimbo za kila mwanasiasa asiye makini. Nakumbuka mwanasiasa mmoja aliliambia Bunge la Bajeti kwamba waathirika wa daraja la Kigamboni wameshathaminiwa mali zao hivyo bado malipo tu. Mimi ni mmoja ambaye napitiwa na barabara ya hilo daraja, lakini hadi leo niandikapo makala haya sijathaminiwa kilicho changu.

Halafu anakuja mtu anasema watu wa Kigamboni wamechochewa na wapinzani kupinga ujenzi wa daraja. Nachukia kauli za aina hiyo maana ni za kudhalilishana.
Hivi Kigamboni kuna ma-tabula rasa (wajinga) wanaosubiri wajuaji kutoka upinzani au chama tawala kuja kuwaelekeza cha kufanya? Wote wenye fikra za aina hiyo wanajidanganya na kama walizoea kunadi sera za aina hiyo sehemu nyingine, Kigamboni wameula wa chuya. Wamuulize yule "mwekezaji" wa kiwanda cha samaki pale Vijibweni mwaka 2004 akisaidiwa na kupigiwa debe na aliyekuwa mkuu wa mkoa wakati huo aliishia wapi.
Tulikomaa pale hatukutoka hadi leo tunapitiwa na barabara, nao wakituletea gozi gozi, wembe ni uleule uliomnyoa "mwekezaji" wa kiwanda cha samaki.
Huwezi kusimama bungeni unadanganya umma umethaminisha mali za wananchi pale Vijibweni wakati si kweli, halafu mtu anatarajiwa achekewe chekewe tu. Mtu wa aina hii lazima aitwe kwa jina lake (call a spade a spade) yaani kama ni mwongo basi aitwe hivyo bila kuumauma maneno.

Kama hakuna malipo hakuna barabara kupita pale Vijibweni na wala hatuhitaji mwanasiasa wa upinzani au chama dola kuja kutusemea. Sisi wahanga wa mradi huo tunajua kujisemea wenyewe. Tangu lini funza anikae mimi halafu wewe ndiye uonyeshe wapi funza aliko mwilini mwangu? Hizo ni falsafa zenye mtindio wa mwelekeo.
Badala ya kulaumu wapinzani, Serikali ifanye wajibu wake kuhusu utata wa mji mpya Kigamboni kwa kuwashirkisha wananchi katika hatua zote kama alivyopendekeza Mbunge Ndungulile na kuungwa mkono na wana-Kigamboni.

Kule Kigamboni wakazi wameunda kamati yao ya kufuatitlia maendeleo ya mchakato mzima wa mradi mji mpya. Wameshaongea sana kwenye mikutano ya hadhara, wameongea na waziri, naibu waziri, katibu mkuu na watendaji wengine serikalini na hata NGOs.
Mara nyingi viongozi wa kamati wametokea kwenye runinga mbalimbali. Wafuatiliaji wa vipindi hivi watakumbuka kwamba kamati ilihitimisha kwamba mradi wa Kigamboni ni EPA, Richmond, Dowans, Deep Green, Tangold na miradi mingine ya kifisadi.
Mpaka leo hakuna aliyekanusha na kujenga hoja ya uhalali wa mradi huo.
Halafu si mara moja maofisa kutoka wizarani wameshatimuliwa na wananchi kule Kigamboni lakini hakuna aliyesimama kuwatetea. Mambo (beacons) zilizowekwa na mkandarasi bila wananchi kushirikishwa zimeshang'olewa na wananchi, mbona hawachukuliwa hatua za kisheria kama beacons zile ziliwekwa kihalali?

Kamati imeshatafiti na kugundua kuwapo uvunjaji mkubwa wa sheria za nchi kwa upande wa Serikali katika kutekeleza mradi huo. Hakuna aliyesimama kule serikalini na kutetea utawala wa sheria unavyotumika katika kutekeleza mradi wa mji mpya kule Kigamboni. Ni katika mazingira hayo mbunge wa Kigamboni Faustin Ndungulile alisimama pale bungeni kutoa tamko la wakazi wa Kigamboni kwamba mradi uanze upya kwa kufuata sheria ambazo Bunge limetunga. Akaishia kutimuliwa bungeni kwa sababu ya kutetea haki za watu wa Kigamboni lakini pia kutetea hadhi ya Bunge lenyewe.

Lakini mheshimiwa huyo ni Mbunge wa chama dola si wa upinzani. Kwa mantiki hii hoja ya kusema wapinzani wanapinga mradi wa mji mpya Kigamboni naiona ni dhaifu sana na haina mashiko. Ukweli ni kwamba wananchi wa Kigamboni kwa utashi wetu bila kusukumwa na chama chochote ndio tunaopinga mradi huo unaoendeshwa kinyemela.

Hoja ya kuendeleza Kigamboni kwa faida ya wananchi ni dhaifu na haina mashiko. Kama ukifanikiwa kuziona zile picha (model impessions) za jinsi mji utakavyokuwa nadiriki kusema hapa ni mji ambao wananchi wa Kigamboni hawamo katika makadirio yake. Kule kuna eneo la viwanda, kuna eneo la utalii na burudani, kuna eneo la biashara za kimataifa, kuna eneo la shule na vyuo vya kimataifa na eneo la makazi ni asilimia kama 7% tu hivi. Wengine wamelibatiza eneo hilo la makazi kuwa ni concentration camps.
Majengo yake ni maghorofa yanayofikia 20 hadi 100. Mitaa yake hakuna njia za guta wala mikokoteni. Bustani zake ni za maua si bamia, matembele, viazi wala embe. Nyumba zake si za kupikia kwa kuni wala mkaa, hamna mabanda ya kuku, mbuzi, nguruwe, njiwa wala ng'ombe.

Kwa mazingira hayo wananchi wa Kigamboni itabidi wawapishe wageni na wao wasonge mbele huko Chekeni Mwasonga na Tundwi Songani wanakoweza kulima, kufuga na kuendesha mikokoteni.
Tuache kudanganyana hapa eti kuna mtu ana uchungu na watu wa Kigamboni. La msingi tu watu walipwe vizuri, si kama walivyodhulumiwa wenzetu wa upande wa Kurasini. Serikali iliwalipa shilingi milioni 20 kwa eka yenye wakazi 10 hadi 20. Serikali imeuza maeneo yale baada ya miezi isiyozidi sita kwa wawekezaji kwa shilingi milioni nyingi.
Na wala watu wasitukumbushe yaliyojiri mwaka 2005 kuhusu daraja hilohilo. Juhudi za kuanza ujenzi Oktoba 2005 zilikwamishwa na kwa sababu ambazo hazijawahi kuwekwa wazi. NSSF nadhani wanakumbuka kilichotokea wakati ule licha ya maandalizi yote kuwa yalikuwa yamekamilika.

Tulitangaziwa ya kuwa imepatikana kampuni ya Kichina iliyojenga huko kwao daraja la urefu wa kilomita 30. Watu wakajinadi kwamba Wachina hao wangeweza kutumia muda mfupi sana kujenga daraja la Kigamboni. Lakini mradi uliyeyuka kama theluji kwenye kiangazi.
Walawale waliokwamisha ujenzi wa daraja huko nyuma leo wanatamba hadharani na kudai Dk. Ramadhani Dau apewe nishani ya utendaji bora. Historia ni hakimu makini sana, watu wasifikiri wanaweza kujifanyia watakavyo halafu historia ikawasamehe.
La msingi ni kwamba, kama vile tunavyojinadi kuwa tunafuata utawala wa sheria basi zoezi lile la mji mpya Kigamboni liende kwa kufuata sheria zilizopo. Hiyo ni pamoja na wananchi kushirikishwa kama sheria zinavyotaka. Lakini kwa usiri na ubabe huu unaotawala zoezi zima la mradi wa mji mpya Kigamboni, lazima hoja za kwamba eneo ameuziwa Bush zitaendelea kujitokeza.

Kama si kweli Bush kauziwa eneo la Kigamboni, usiri na ubabe, na hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja vinatoka wapi? Ukweli (reality) unaiishi independent of the subject, si hoja nani anasema; rangi yake, cheo chake, umri wake nk. Hivyo basi, ukweli kuhusu mazingira yanayozunguka mradi wa Kigamboni kama ilivyokuwa kwa EPA, Richmond, Dowans, Simbion, Tangold, Deep Green na mingine mingi utakuja kujipambanua na hatimaye kujulikana tu.
Ole wao wanaojifanya manabii wa injili hii ya Blue Diamond. Watu wasije kulia na kusaga meno ufunuo utakapofunika sayari hii na hila zao kuwekwa hadharani.

Mwandishi wa makala hii anaitwa Osmund Kapinga ni msomaji wa Raia Mwema wa muda mrefu
 
Kaka umeongea vizuri zaidi, mimi nikiwa mmoja wa waathirika ki ukweli sijui undani ya mpango huu, naambiwa nitashirikishwa how? je nitaweza kumudu kuishi mji huo mpya na wanangu wakati kipato changu ni chini ya dola moja kwa siku? mji unaojengwa ni kwa ajiri ya wafanyabiashara matajiri, viongozi wa serikali na watu maarufu au ni wetu sisi watu maskini tunaomiliki maeneo haya?

Je wananchi hawa ambao JK alikuwa anawahutubia watakwenda kuishi wapi? maana nina uhakika hawataweza kuishi na wazungu katika mji huu mpya wa kihistoria
.

Mkuu kwa kipato kipi waweze kuishi katika mji kama huu
+l9Xq6gVXStKEAAAAABJRU5ErkJggg==

Wengi wa watakao hamishwa kwa watakao bahatika kufika ndani ya mji mpya ni kwa kufanya kazi za ufagizi wa mitaa na mayaya wa kulea au kusindikizia watoto wao shule.Na tusipo angalia hata hizi nafasi zitachukuliwa na Wamalawi kama ilivyo nyumba nyingi masaki ambapo House girl au Shamba Boy kati ya nyumba kumi hukosi nyumba Nne ni wamalawi hasa hasa nyumba za Wageni toka Nje.
 
Mkakati wa kudhulumu ardhi za walala hoi unaendelea.Serikali katika kutimiza ndoto yake ya kuwa dalali wa Ardhi kwa mwaka huu 2013 taarifa za chini chini zinadai wizara inapanga kupandisha gharama ya kufungulia madai ya kudai haki mbele ya chombo kinachotoa haki.

Jisomee mwenyewe na hii yaweza kuwa maandalizi ya kufanyikisha mambo mengine yaliyonyuma ya pazi toka kwa Serikali Sikifu !


[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 668"]
[TR]
[TD="width: 730"] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
[TR]
[TD]
Gharama za ardhi kuwaliza wananchi
jumamosi, 5 januari 2013

na Edson Kamukara


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 730"] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
[TR]
[TD] WANANACHI wa kawaida wenye vipato vya chini huenda sasa wakaikosa haki yao ya kufungua madai ya ardhi au makazi kutokana na serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupandisha mara dufu ada za kufungulia mashtaka hayo.

Tayari viwango hivyo vipya vimeanza kutumika kuanzia mwaka huu wa fedha hatua ambayo wadau wa masuala ya ardhi wanadai kuwa ni mkakati wa serikali kujaribu kuwazuia wananchi wa kipato cha chini kuufikia usawa huo kisheria.

Wadau hao wanasema kuwa hata awali kabla ya ada za kufungulia mashitaka kupanda, bado watu wa chini walikuwa wakishindwa kupata fedha za kufungulia madai yao hali iliyosababisha wengi wao kuamua kumuachia Mungu awapiganie.

Kwa mujibu wa gharama mpya, fomu ya maombi itapanda kutoka sh 500 hadi 4,000 wakati kufungua madai ya mali isiyozidi sh milioni 10 mwananchi atapaswa kulipia sh 40,000 badala ya 5,000 ya awali.

Kufungua madai ya mali inayozidi sh milioni 10, mhusika sasa atagharimika sh 120,000 badala ya sh 15,000 za awali, huku kupeleka hati ya utetezi kwa maandishi malipo yake yamepanda kutoka sh 2,500 hadi sh 20,000.

Gharama hizo zinaonesha kuwa, wale wanaotaka kufungua maombi madogo watalipia sh 40,000 badala ya sh 5,000 na kupeleka hati ya kiapo itakuwa sh 12,000 badala ya sh 1,500 za awali.

Kuingiza viambatanisho vya utetezi kwa kila kimoja gharama yake itakuwa sh 4,000 badala ya sh 500 wakati kufungua rufaa kutoka Baraza la Kata kwenda Baraza la Ardhi na Nyumba sasa imepanda kutoka sh 2,000 hadi sh 16,000.

Mwananchi atakayetaka kupata nakala ya mwenendo wa kesi kila kurasa atagharamika sh 4,000 badala ya sh 500 na kuchukua nakala ya hukumu atalipia sh 16,000 badala ya sh 2,000 ya awali.

Kwa mujibu wa chanzo chetu hicho, nakala ya amri ya Baraza inapanda kutoka sh 500 hadi 4,000 na malipo ya mpeleka hati ya madai, maombi madogo, hati ya kiapo, ama hati ya utetezi sehemu ya jiji au manispaa yameongezeka kutoka sh 3,000 hadi 24,000.

Malipo ya mpeleka hati ya madai, maombi madogo, hati ya kiapo, ama hati ya utetezi katika sehemu nyingine yoyote isiyo ndani ya jiji au manispaa yameongezeka kutoka sh 2,000 hadi 16,000 wakati kutoa maombi ya shahidi itakuwa sh 4,000 badala ya 500.
Kufungua gharama za kesi, mdai atapaswa kulipia sh 40,000 badala ya 5,000 ya awali na kufungua maombi ya utekelezaji ya hukumu imepanda kutoka sh 2,000 hadi 16,000.

Nazo gharama za kufungua/kupata hati/maandiko yoyote ambayo hayakuoneshwa katika utaratibu huu zitaongezeka kutoka sh 500 hadi 4,000.
Mjadala sasa unabaki kuwa pamoja na ada ya awali kuwa ndogo, bado walikuwepo watu waliokuwa wakishindwa kupata fedha za kulipia ada za kufungulia mashauri yao katika mabaraza. Sasa je kama hali ilikuwa hivyo kwa sasa itakuwaje?

Ni wazi kuwa gharama hizo zitakuwa zinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 24 (1) ambayo inamruhusu kila mtu kuwa na haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali aliyonayo.


Juhudi za kupata kauli ya Wizara ya Ardhi, hazikuzaa matunda jana licha ya msemaji wake kusisitiza kuwa wanaandaa taarifa ya ufafanuzi, lakini hadi tunakwenda mitamboni hakukuwa na majibu yoyote.


C:\DOCUME~1\HR\LOCALS~1\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif



[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mhe.Tibaijuka.
Wakati Wizara inaota ndoto ya Kufanikisha mji Mpya wa Kigamboni inatakiwa kuweka wazi masilahi na thamani/viwango vya malipo kwa kwaazi watakaoathirika na mradi kwa kutumia thamani/msukumo wa Soko.
rejea baadhi hapo chini kama kianzio.


https://www.jamiiforums.com/member.php?u=60189

Plot inauzwa yenye ukubwa wa square meter 1540, ipo maeneo ya sinza kumekucha opposite lion hotel.

Now inatumika kama garage, na hamna structure yoyote iliyojengwa,suitable for a hall,hotel or yard. Bei yake ni mil900 maongezi yapo.
Hii kwa hesabu za haraka One square Meter. 900,000,000 /1540= 584,415.6tzs na eneo hii liko kilomita kadhaa na pwani.



Home

A dream behind the plush Kigamboni .By Stella Barozi .31st May 2009.

Kati Kerenge, who works with Tanga Cement, has bought one of the South Beach plots and plans to rent it out to cover the $1,300 a month, 15-year mortgage.

The three-bedroom house cost $130,000
, but Kerenge anticipates it being worth far more in the future. "I figured I might get into it now because I think later Kigamboni would be unaffordable. I was told it was going to be the new Masaki," she says.

Kerenge had also been inspired to buy in the Kigamboni area because she knew the planned bridge connecting Kigamboni and the city centre would draw far more residents, tourists and merchants. She has since lost faith, as years after the bridge was proposed the project has stalled.

Je waathirika kama hawa kweli Serikali imejianda sawa kukabiliana na matatizo haya na ni lazima kiasi kama hiki cha pesa kutumika wakati tuna miradi mikubwa yenye kuhitaji pesa kwa haraka mfano Umeme,Hospitali ,Elimu na mengine mengi ambayo ni aibu kufikiri na kutumia trilioni kadhaa kujenga mji.

Serikali ingeishia katika hatua ya Kutoa Ramani/Muundo wa Jinsi Mji utakavyo kuwa na Kuiachia Halmashauri husika ikishirikiana na City Council suala la Usimamizi wa Ramani husika huku Taasisi binafsi ,Mtu mmoja Mmoja au Taasisi za Umma kama (NHC) zenye kufanya Uendelezaji Majengo ichangamkie Kazi hii.
 
Hii ndiyo Serikali sikifu.Na haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania.
Kama kweli maendeleo ni kwa staili hii siamini wanaoimba kwamba wanataka kuwa nufaisha wakaazi wa maeneo husika ni ya kweli.

Kwa Serikali inayoamini utawala wa Sheria ingewapeleka mahakamani wahusika na sikuvunja Nyumba zao.
Je walikuwa na hati ya mahakama ?
Wanakigamboni wanatakiwa kujiandaa na hali hii .
← Shughuli za kichama kata ya Charambe

[h=2]Bomoa bomoa Mtaa wa Minondo, Somangila, Kigamboni[/h]
dscn0507.jpg




← Shughuli za kichama kata ya Charambe

[h=2]Bomoa bomoa Mtaa wa Minondo, Somangila, Kigamboni[/h] Posted on April 29, 2013 by Faustine
dscn0506.jpg
Hivi majuzi nyumba zipatazo 34 za wakazi wa eneo la Minondo, Amani Gomvu, Somangila walivunjiwa ili kupisha ujenzi wa nyumba za vyombo vya ‘ulinzi na usalama'. Kwa mujibu wa wananchi hawa walivamiwa saa kumi alfajiri na kuamriwa kutoka nje ya nyumba zao ili kupisha zoezi la ubomoji. Wananchi hawa wanadai hawakupewa notisi kuhusu zoezi la ubomoaji .
Kimsingi, wananchi hawa hawapingi mradi huu, ila wanalalamikia kubomolewa nyumba bila kulipwa fidia na wengine kupewa kiwango kidogo cha fidia ambacho ni tofauti na viwango vya soko.
dscn0507.jpg
Moja ya nyumba 34 zilizobolewa.
dscn0508.jpg

Nilifuatilia maelezo ya waathirika kuhusu sakata la bomoabomoa.

Nikipitia baadhi ya vielelezo walivyokuwa navyo waathirika.

Nyumba ya kisasa ya vyumba vitano ilibomolewa. Wahusika hawakupewa nafasi ya kukoa mali zao.
 
Suala la Mtaa wa Minondo, Somangila, Kigamboni

Wahusika wa wakuu wa unyama huu na ufisadi ni

Sadiq Meck Saidiq mkuu wa mkoa wa Dar,

Said Mwema, mkuu wa jeshi la polisi,

Mkuu wa wilaya ya Temeke,

Diwani wa Somangila almaarufu Mama Mpanjila


Hawa wamepigwa milioni 800 na mchina, wakauza ardhi ya wananchi kwa mgongo wa mji mpya wa kigamboni
 
Suala la Mtaa wa Minondo, Somangila, Kigamboni

Wahusika wa wakuu wa unyama huu na ufisadi ni

Sadiq Meck Saidiq mkuu wa mkoa wa Dar,

Said Mwema, mkuu wa jeshi la polisi,

Mkuu wa wilaya ya Temeke,

Diwani wa Somangila almaarufu Mama Mpanjila


Hawa wamepigwa milioni 800 na mchina, wakauza ardhi ya wananchi kwa mgongo wa mji mpya wa kigamboni

Mkuu funguka kidogo ili wadau waelewe unyama wanaofanyiwa na viongozi wao kwa Tamaa za fedha na mali kupitia kwa jasho la walalahoi.

 
Suala la Mtaa wa Minondo, Somangila, Kigamboni

Wahusika wa wakuu wa unyama huu na ufisadi ni

Sadiq Meck Saidiq mkuu wa mkoa wa Dar,

Said Mwema, mkuu wa jeshi la polisi,

Mkuu wa wilaya ya Temeke,

Diwani wa Somangila almaarufu Mama Mpanjila


Hawa wamepigwa milioni 800 na mchina, wakauza ardhi ya wananchi kwa mgongo wa mji mpya wa kigamboni



Mkuu habari hiyo inatisha.Je Ni Mchina wa Kampuni gani hiyo ?

Kweli naanza kuamini msemo wa serikali hii ni ya CHUKUA CHAKO MAPEMA-CCM
 
Hii ndiyo serikali kweli ni maajabu kwa kauli kama hii kutoka kwenye kinywa cha waziri tena profesa.
Haya ndiyo baadhi ya mambo tunataka Katiba Mpya iyatamke kuwa ni kosa na mhusika lazima awajibishwa au ajiwajibishe au aombe radhi.

Hivi kwenda Mahakamani ni kudanganyana? na Kama wanadaganywa siasubiri huo udanaganyifu!


[h=3]Prof Tibaijuka: Hameni Mivinjeni[/h]
Pia aliwaonya wakazi hao wasikubali kudanganywa na wanasheria wakiamini kuwa watawasaidia katika suala hilo.


“Msidanganywe na wanasheria katika hilo, watakula pesa yenu na kesi hamtashinda na hatimaye mtabaki kulaumiana,” alisema Tibaijuka.
 
Taarifa zilizopo zinadai Kamati ya Ardhi ,Maliasili na Mazingira chini aJames lembeli itakutana na Kamati za Tibaijuka kuhusiana na Mji Mpya wa kigamboni .

Lakini kinachosikitisha Kamati ya Lembeli imekwepa kukutana na Kamati Kubwa ya Waakazi wa Kigamboni ambayo imekwisha kutana na Kamati hii ya Lembeli lakini safari hii inaonekana ujio wao eneo la Kibada na kuja kuonana na Kamati za mitaa zilizoundwa kupitia Waziri Tibaijuka pamoja na Wizara yake kwenye Mradi huu wa Mji Mpya na wakiwa walalamikiwaji inaleta shaka .

Kamati ya Lembeli kama kweli inakwenda kufanya kazi ya Uwakilishi wa Umma/Watanzani ingefanya pia jitihada ya kuonana na Kamati yenye kuwakilisha Masilahi ya Wakaazi Wengi wa Kigamboni
 
Asante Mhe.Mbunge.
Ujumbe huu umetulia ni wale wasiopenda haki ikitendeka ndio waanoweza kuziba masikio yao!


Kikwete visits the Kigamboni of Singapore


The President of the United Republic of Tanzania is currently touring Singapore with the aim of wooing investors to Tanzania.
One of the agenda in this visit is to invite real estate developers to Tanzania to invest in the Kigamboni New City Project.
The Kigamboni New City project which has been pipeline for about five years now, is cash strapped and enjoys very little support from the Kigamboni people due to the following reasons:



  1. Disregard of the rule of law the Ministry of Land officials;
  2. Poor stakeholders and landholders participation;
  3. Heavy handedness and use of threats to landholders from Ministry of Land officials
  4. Lack of transparency and non disclosure of people’s rights
  5. Corruption
The Kigamboni people hope that the energy expended in looking for investors, will also replicated in Kigamboni to get them informed and engaged .
 
Hivi kuna nini kinaendelea, mwenye info kama hii KDA imeshaanza kazi rasmi kisheria ya kuendeleza mradi huu hasa kuanza kulipa fidia wahanga wa ardhi watakaopisha ujenzi wa mji huu wa kisasa.
 
Hivi kuna nini kinaendelea, mwenye info kama hii KDA imeshaanza kazi rasmi kisheria ya kuendeleza mradi huu hasa kuanza kulipa fidia wahanga wa ardhi watakaopisha ujenzi wa mji huu wa kisasa.


Mkuu FUSO hao jamaa wako kazini tayari na wanaofisi Kigamboni. Ukitaka kuwa tembelea Ofisi yao iko karibu na Beach moja inaitwa Mikadi Beach ukifika hapo ulizia na kama unamacho mazuri utaona Kibao chao.

Na kwa taarifa Kibada maeneo ya Uvumba na Kivurugwe wamekwisha anza kuchakachua ardhi za wenyeji .
 
Last edited by a moderator:
we are excellent on papers, but utendaji nehi che

Kigamboni ni a very good sign on how inefficient and unproductive serikali imekua kwenye maeneo nyeti kama ardhi

kinachotakiwa ni executive order na kuanza implementation, in addition, serikali haiwezi na haipaswi kutekeleza transformation ya kigamboni, inatakiwa iandae sera, mipango na miongozo halafu iache private sector i drive the implementation
 
Haya naona kimya kimekuwa Kingi ni vizuri tukakumbushana .Mwaka umepita sasa hivyo wakati Bajeti ya Wizara husika ikiwa ni
NEW: PARLIAMENT TIMETABLE Click here to Download
21.JUMAMOSI 31/5/2014 • HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO
YA MAKAZI. Saa 3.00 Asb – 7.00 Mchana NA Saa 10.00 Jioni - 2.00 Usiku

kwa wale waathirika wa Mradi huu ni vizuri waka tega masikio vizuri !.

Maana hayo yaliyoahidiwa na Mhe.Tibaijuka ni mwaka umepita ,lakini pia ni miaka zaidi ya Mitano toka Mradi utangazwe na hakuna cha Maana kinachoendelea zaidi ya Kuundwa Taasisi na kuwapa Watendaji Ulaji.

Wabunge wetu Mpoo!!!!!!!!!.







Taarifa ya Waziri: Wakala wa Kusimamia uendelezaji wa Mji Mpya, Kigamboni

23/01/2013

4. Ili kutekeleza kusudio la kuendeleza eneo la Kigamboni, hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na:-


  • Kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa ya kuendeleza eneo la Kigamboni na taratibu za uendelezaji.
  • Kutafuta fedha za kutosha kutekeleza mradi.
  • Kupima maeneo husika na kuyaandaa kwa ajili ya uendelezaji.
  • Kujenga nyumba mpya za kuishi kwa ajili ya kuwahamishia wananchi ambao makazi yao yataathiriwa na ujenzi wa Mji Mpya; na
  • Kufanya uthamini wa mali na kuwafidia wananchi watakaolazimika kahama kutokana na ujenzi wa mji.


 
Back
Top Bottom