GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Wonders shall never end ndio ninachoweza kusema, Wana CCM waliuaminisha uma wa watanzania kuwa nyungu, malimao na tangawizi vinatibu Corona.
Kheri Gwajima ameamua kusimamia msimamo ule waliokubaliana enzi za John Pombe Magufuli kuwa chanjo hazifai.
Wanafiki na wachumia tumbo wanatumia kauli ya Gwajima waliokubaliana wakati ule kuwa chanjo ni tatizo, Na wazungu hawatupendi hivyo hakuna kitu cha bure toka kwa beberu.
Mimi Gussie ni mwana CCM na nilishapigwa chanjo ya Pfizer kwa ajili ya korona, Na amini Katika sayansi toka kwa madaktari.
Tetekuwanga watu walipiga chanjo utotoni lakini bado kuna watu wazima wanaumwa, Je Tuache chanjo ya Tetekuwanga kwa kuwa baadhi wanapata ukubwani?
Wana siasa Waache kuingilia taaluma za afya. Wengine elimu zao ni za hapa na pale, Hiyo taaluma ya afya wametoa wapi?
Dkt Faustine Ndugulile aliposimamia taaluma ya udaktari kuwa kufukiza ni shida akatumbuliwa na wana ccm walishangilia.
Hakika Dunia ni duara na sio tambarare, ukizunguka unarudi pale pale kwenye sayansi.
Kuna muda inabidi uruhusu kichwa chako kifanye kazi ya kufikiria mambo na sio kukibeba kichwa juu ya mabega kama mizigo mingine na kujitoa ufahamu.