Kigeugeu Cha timu za Kariakoo na mashabiki zao

Kigeugeu Cha timu za Kariakoo na mashabiki zao

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Habari za muda huu.

Msimu wa 2019/2020 ,Simba walimsajili Onyango na Yanga wakamsajili Mwamnyeto.

Mashabiki wa Simba walidai kuwa Mwamnyeto alikuwa dhaifu na alifichiwa madhaifu na AME , viongozi wakapambana haraka Ame akasajiliwa ili kupigia mstari hoja zao.
Yanga wakadai Onyango ni mzee.
Miaka miwili baadae Kuna tetesi za Simba kumtaka Mwamnyeto na Yanga kumtaka Onyango Tena mashabiki wameanza kuwapamba kwa maneno mazuri.

Hawa majamaa hawana tamaduni za kusifiana Ila huwa wanazodoana na Mambo yakibadilika kidogo hugeuka uadui mkubwa sana.refer kaseja na simba
 
Onyango huyuhuyu?
 
Mwamnyeto hawezi kuchukua hata namba ya Kennedy...Usimlinganishe 'Ochieng'
 
Sasa mwamnyeto akacheze simba....????? basi simba hawako siriasi kabisa!!
 
Mwamnyeto na Simba wapi na wapi

Mwacheni akuze kipaji kwanza pale jangwani kwa kupata muda mwingi wa kucheza kisha baada ya misimu miwili tutaona maendeleo yake. Vinginevyo ataua kipaji Simba kwa benchi japo mshahara mzuri.
 
Hiyo ni mind game ya mawakala wao kwasababu hao wachezaji mikataba wote inakaribia kwisha.
 
Mwamnyeto hana kiwango cha kuanza first eleven ya Simba.
 
Haya maneno tuliyasikia kwa Morrison. Iho atacheza namba ya nani ohoo hata benchi hapati namba ohoo mwizi wa magari sisi wa nini. Lakini leo wote mashuhuda ndio muokozi wa Simba yaani ndio tegemeo la Simba asipokuwepo utasikia wanamlsumu pablo waeleze huyu mtu kwanini hayupo hata benchi
 
Mwamnyeto labda apewe kazi ya kufua bips za wachezaji wa Simba.
 
Onyango aende Yanga ipi? Labda yangayanga, ila sio Young Africans..
Yaani ikatokea Viongozi wa Yanga wakamuacha Mwamnyeto na kumsajili Onyango, basi nitawadharau sana.

Hata hivyo natambua fika, mtoa mada atakuwa ameandika tu kwa kujifurahisha.
 
Back
Top Bottom