Kigezo cha kuwa Sheikh (Shehe) ni nini?

Kwenye ukristo kuna vyuo vya theology.
Nasubiri jibu.
 
Kwa kifupi ni kujua mambo yote yaliyomo kwenye mazingira yake yanapotokea na kuyatatua Kwa kutumia mwongozo wa Furqan.kwa mfano mtu anapokufa ajue taratibu zake,Ndoa na talaka,kuamrisha mema na kukataza mabaya.

Na sisi waislam muda flani ni tatizo kuliko hata shweitwan,akisoma Aya mbili tatu,akivaa kanzu na kofia yaani mtaani hapakaliki.
 
Kwa hiyo na wewe ni Sheikhe?
 
😀😀😀🤣🤣. .am out
 
Waislam walioishika dini yao huwa ni wastaarabu sana. Si rahisi kumkuta anaunanga ukristo namna hiyo tena kwa mabaya lukuki.

Huwa naangali sana Mahaasin Tv hasa mawaidha, huwa hawana ujinga wa namna hii.

Ila huko mitandaoni naonaga clips za baadhi ya hotuba wanawadis viongozi wa dini wa kikristo waziwazi na kwa kuwataja majina kabisa, hii sio sawa kabisa. Wakati uislam unajitosheleza kabisa bila kuunanga au kuusema vibaya ukristo, hata hao mashekhe wabobevu wengi husema usemeni wema wa uislam na sio kuisema dini nyingine na kujenga chuki na sio urafiki.

Watu kama wewe ndio hufanya uislam uonekane ni ugaidi, chuki ya wazi, maneno ya kejeli na vijembe.
 
Sasa kama hao Masheikh wanajikita kwenye elimu ya dini pekee, hayo maarifa kuhusu elimu dunia huwa wanayapata wapi?

Ifikie wakati muwaige Wakatoliki. Kabla ya kufikia hatua ya upadre, lazima usome siyo chini ya miaka 10!
Na katika miaka yote hiyo, utafanyishwa mitihani ya elimu dunia, na ile ya elimu ya dini! Na mitihani yote ni ile yenye mchujo! Yaani ukifeli wastani wao, unafukuzwa. Na lengo ni kuhakikisha huwi Padre Kilaza.

Sasa nyinyi ndugu zetu! Dah!! Mnasikitisha sana kwa kweli. 🙁 Yaani ukiimudu tu elimu ya dini, unakuwa Sheikh!!
 
Wakristo mara nyingi wamekuwa wakijifanya wasomi.

Wanaenda mbali zaidi kwa kuwadharau waislamu kwamba ni 'wazee wa mdarasa' hawana elimu.

Cha ajabu usomi wao upo mdomoni tu huku nchi ikizidi kufubaa na wao wasomi wakiangalia tu.

Ofcourse ni wasomi kweli. Record zinaonyesha na isitoshe muundo wa dini huwez kuwa kiongozi kama hujasoma kweli kweli
 
Umejibu swali?
 
Ndio tunaomba kujua wanatakiwa wawe na vigezo gani?
 
Tatizo hamjui kusoma!

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

[ AL - JUMUA' - 2 ]
Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.
 
Oh Tate nanee,,wabwanga tushikamane.

Hao wanaosoma miaka 10 nawafananisha na msafiri anayepita nyikani Toka mwanzo wa safari mpaka anafika Hajawahi geuka nyuma.

Hao waliokaa miaka 10 darasani,Sasa hivi wanazurura na waraka madhabauni ilihali wakijua au la tatizo ni Katiba.Yaani wamekaa darasani ila tatizo hawalijui.

Mvua inanyesha inapeleka maji baharini Kisha mnaagiza mafuta ya alizeti Toka Uikrane,,,miaka 10 darasani imewasaidia Nini?

Awamu ya kwanza mlikua na RC mbobezi,Taifa mmelisaidia Nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…