Kigogo avujisha video ya wizi wa kura ulivyokuwa ukifanyika 2020

Kigogo avujisha video ya wizi wa kura ulivyokuwa ukifanyika 2020

Status
Not open for further replies.
Kwani kura zinapigwa kwa kuwekewa alama ya X au tick? Sijaelewa hapo
Sheria ya uchaguzi inatambua alama yeyote kwenye karatasi ya kupigia kura kama iko ndani ya chumba cha Mgombea!
 
2020 karatasi iliyokua na wagombea wengi ilikua ya Uraisi na Wagombea wote walipangwa Horizontally waliiba ila hii video haina ukweli. Vile vile mgombea aliepita uliambiwa uweke alama ya Vema .
 
Kumbuka kuna Wagombea Urais,Ubunge na Udiwani kwa hiyo huyo bwana anachokifanya ni kuweka alama kwa mgombea anayemtaka yeye!
2020 karatasi iliyokua na wagombea wengi ilikua ya Uraisi na Wagombea wote walipangwa Horizontally waliiba ila hii video haina ukweli. Vile vile mgombea aliepita uliambiwa uweke alama ya Vema .
 
Mbona kama sio Tanzania? Halafu mfumo wetu wa kupiga kura huwa tunaweka alama ya tiki (✅) badala ya kosa (❌) kama anavyofanya huyo hapo kwenye video.

Hao wagombea nimeshindwa kuwatambua…
Sahihi na hiyo video itakuwa Zimbabwe au Afrika Kusini sio Tanzania.
 
Kwani kura zinapigwa kwa kuwekewa alama ya X au tick? Sijaelewa hapo
Mbona anamark kila mahali
Mbona anaweka X badala ya
Kura zipo za udiwani, ubunge na urais, so kila moja anaifuata ilpo.

Kuhusu kuweka X, alama yoyote ikiwa ndani ya box au picha ya mgombea bila kuvuka kwa mwingine, hiyo ni kura halali. Kwa hiyo ukiweka ✓ au X au herufi yoyote au jina hata nukta, ujue umempigia kura mgombea ambaye alama hiyo ipo kwake (ingawa wapiga kura huko nje wanaambiwa waweke ✓).

Usije ukamuwekea mgombea alama ya X ukidhani unamkomoa, ukweli ni kwamba utakuwa umempigia kura
 
Video hii si ya Tanzania

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search ulibaini kuwa video hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza mtandaoni mnamo tarehe 1 Novemba, 2020.

Aidha video iliambatanishwa na maneno (Caption) yaliyo katika lugha ya kifaransa, "Présidentielle en Côte d'Ivoire : Les preuves d'un bourrage d'urne" ambayo kwa lugha ya kiswahili yametafsiriwa, "Uchaguzi wa Urais nchini Côte d'Ivoire: Ushahidi wa kujazwa kwa masanduku ya kura"

Pia video hiyo ilichapishwa Novemba 03, 2020 katika mtandao wa X, ikiambatana na ujumbe unaosomeka "Scrutin présidentiel en Côte d’Ivoire .Véritable mascarade. Regardez par vous même." ambao kwa kiswahili umetafsiriwa, "Uchaguzi wa Urais nchini Côte d’Ivoire: Sarakasi halisi. Tazama mwenyewe."

Hivyo Video imebainika kuwa ni kutoka nchini Ivory Coast wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Oktoba 31, 2020. Aidha moja kati ya vigezo vilivyobainika katika ni pamoja na Karatasi ya kupigia kura inayoonekana ambayo inafanana na karatasi halisi zilizokuwa zikitumika katika upigaji wa kura katika uchaguzi huo.
 
Na wakala wenu wa vyama vya upinzani ndani ya vituo huwa nini wazushi nyie?
unaweza ukawaita watu majina yoyote ili ufurahishe nafsi yako na wanaokutuma ila ukweli unabaki palepale kwamba na sisi tunaishi Tanzania tena wengine wapo Halmashauri huko wewe ukiendeleza ujinga tu hapo lumumba.
mwaka 2020. kura zilipigwa siku mbili kabla pale ccm mkwajuni. walioshiriki walikuwa watoto waliotcfutwa toka mikoani na waliahidiwa kulipwa 5000/
huko wilayani walimu makada wa chama waliteuliwa kusimamia uchaguzi 2020. waliingiza kura zilizopigwa kwenye masanduku saa 9 usiku kabla vituo havijafunguliwa.
wewe unakata viuno hapo lumumba unaita uzushi . karabaho
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom