Kigogo sio mtu wa kumuita Tundu Lissu mshamba, akemewe

Kigogo sio mtu wa kumuita Tundu Lissu mshamba, akemewe

Genius Mzee

Member
Joined
Jul 29, 2021
Posts
50
Reaction score
222
Mshamba ni nani?

Mshamba ni yule anayejificha nyuma ya kibodi na kuwashambulia wengine au anapambana kwa kujitokeza na kuongea bila kupepesa macho kama Tundu Lissu anavyofanya?

Mshamba ni nani yule aliyeanza kupigania haki toka akiwa shule ya msingi, Sekondari, JKT na kuendelea au yule aliyeanza kujificha nyuma ya kibodi baada ya serikali kuvunja nyumba yake Kimara?

Mshamba ni yupi? Ambaye anaweza kumtukana kila mtu kisa tu kamkosoa au ni yule anayetumia hoja kujibu hoja za wale wote wanaomshambulia?.

Kuwablock watu wanaomkosoa kwenye post zake sio ushamba? Yaani mtu anapokukosoa ni adui yako wewe ni malaika Mbona Tundu Lissu hata Siro hajawai kumtukana ila uwa anamjibu kwa hoja?

Kwangu Mimi mshamba ni yule asiyejua anafanya nini, Anataka nini, Anapataje lini na wapi? Kumtukana kila mtu ni ushamba sana.

Imagine mtu anamtukana na kumzalilisha mtoto kama Zuchu au Nandy watu ambao hawaelewi maana ya siasa ni nini baada ya kuwapa elimu ya uraia wewe unatoka kuwatukana tu and you don't care!

Kwa taarifa Kigogo ni mtoto mdogo mno kwenye siasa za nchi hii harakati zako hazijafikisha hata miaka 10 wakati Tundu Lissu ameanza harakati miaka ya 1990 wewe jiulize ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini?

Kigogo awaulize waliokuwepo kwenye utawala wa Mkapa walivyopambana na Tundu Lissu na Lissu kushinda miaka huyo hata twitter ilikuwa hakuna.

Waulize waliojaribu kumhonga Tundu Lissu kwenye utawala wa Mkapa ili aache kuwatetea watu waliokuwa wanatolewa maeneo ya migodi kwa nguvu kwenye mikoa ya Shinyanga, Mpanda, Tabota, Geita, Mara na Kagera watakupa majibu.

Lissu angekuwa mshamba si angechukua tu pesa za wazungu na kuachana na kuwatetea wananchi?

Tundu lissu miaka yote amekuwa akifanya kazi field tena akiwa sambamba na mke wake akiwa front line kabisa nafikiri hata mwaka Jana alipokuja kufanya kampeni bado mliona alivyokuwa akisumbuana na Police kule Nyamongo na kwingine.

Sasa wewe ndugu yetu unamuita mtu mshamba ambaye yupo ulaya kwa kufanyiwa operation zaidi ya 25 baada ya kupigwa risasi halafu wewe upo ulaya nyuma ya kibodi.

Afadhari Lissu hata akifa leo Mungu akipenda historia ya Maisha yake tayari kashaimaliza historia aliyonayo ni kubwa mno.

Washamba ujificha, Washamba upanic, Washamba ujifanya wanajua kila kitu ili wasikosolewe, Washamba uzusha, hakika Washamba wakikosa ajenda ya kusimamia uwa wanaona kila binadamu ni adui wa maendeleo yao.

Wanaharakati wote duniani uwa hawapambani na mtu uwa wanapambana na mifumo, Jifunze kwa wanaharakati kama wakina Martin Luther King JR na wengine walipambana na mifumo na wakaja kushinda hata kama walikuwa hawapo tena.

Yaani unamtukana Tundu Lissu halafu unamsifia Mbowe? Wakati Mbowe na Tundu Lissu ufahamu hata walikutana vipi?

Kama wewe ni mwanamageuzi kweli njoo na I'd yako original na uje front line uongoze maandamano unayoyapigia kelele, njoo uanzishe chama ukiendeshe kiwe kikubwa kama angalau ACT.

Lissu mageuzi na mapambano aliyoyafanya yanatosha kabisa hata leo akistaafu siasa ila najiuliza kigogo ameshafanya kitu gani zaidi ya kutukana watu?

Mambo ya kuita watu washamba ni ushamba pia.
View attachment 1879158View attachment 1879160
 
Sijawahi kumuona Kigogo mtu wa maana tangu awali, baada ya kumaikiliza kwenye space ya Maria Sarungi, nikamjua ni mtu wa hivyo anajazba sana, aliongea pumba sana issue ya CDM wafanye siasa za msituni
 
Nasimama na Kigogo, katika siku 100 za kwanza CDM walikuwa ndiyo wanufaika wakuu wa uongozi wa Samia mpaka humu ndani kuna thread inasema "Je Samia ni CHADEMA".

Na wakamsifia kuwa anaupiga mwingi. Kama Mbowe angekuwa na busara kidogo alipaswa amu handle Rais SSH kwa namna alivyo. Yaani kama mtu ni brutal na wewe unakuwa brutal. Kama mtu ni muungwana unampinga kiungwana. Wame mu approach Mama kwa kiburi na dharau sana mpaka wanataka wampangie ratiba ya lini akutane na CDM.

Hiyo miscalculation imeirudisha CDM miaka 10, take it from me
 
Sawa ni maoni ya mwanakijani mmoja katili anayeamini katika ukatili na anayefurahia bambikabambika, kwake haki ni shubiri. Ni maoni tu.
 
Hahahaaaa...... Kigogo anawataka wananchi ndio wadai Katiba mpya siyo Chadema!
Huyu mtu ni mwehu nakwambia mimi
Screenshot_20210803-132913.jpg
Screenshot_20210803-133948.jpg
 
Nasimama na Kigogo, katika siku 100 za kwanza CDM walikuwa ndiyo wanufaika wakuu wa uongozi wa Samia mpaka humu ndani kuna thread inasema "Je Samia ni CHADEMA".

Na wakamsifia kuwa anaupiga mwingi. Kama Mbowe angekuwa na busara kidogo alipaswa amu handle Rais SSH kwa namna alivyo. Yaani kama mtu ni brutal na wewe unakuwa brutal. Kama mtu ni muungwana unampinga kiungwana. Wame mu approach Mama kwa kiburi na dharau sana mpaka wanataka wampangie ratiba ya lini akutane na CDM.

Hiyo miscalculation imeirudisha CDM miaka 10, take it from me
Umeandika ukweli sahihi mbowe siku zote alikuwaga na busara na hekima ila licha ya kusikilizwa na kuheshimiwa sijui mbowe ni kichaa gani kilimpanda na kutaka kumfanya Samia aonekane dhaifu ona sasa yuko jela pekee yake. CDM kwa Samia walitumia wrong approach kiasi mama hasikilizii yoyote na CDM itapotea wasipobadilika na kuendeleza harakati bila good calculations, sio siri napenda mabadiliko ila mbowe na CDM walikosa vision ya jinsi ya ku deal na Samia, nchi hii inahitaji upinzani makini usio na mihemko kusaidia taifa.
 
Nasimama na Kigogo, katika siku 100 za kwanza CDM walikuwa ndiyo wanufaika wakuu wa uongozi wa Samia mpaka humu ndani kuna thread inasema "Je Samia ni CHADEMA".

Na wakamsifia kuwa anaupiga mwingi. Kama Mbowe angekuwa na busara kidogo alipaswa amu handle Rais SSH kwa namna alivyo. Yaani kama mtu ni brutal na wewe unakuwa brutal. Kama mtu ni muungwana unampinga kiungwana. Wame mu approach Mama kwa kiburi na dharau sana mpaka wanataka wampangie ratiba ya lini akutane na CDM.

Hiyo miscalculation imeirudisha CDM miaka 10, take it from me
Sijawahi kuona mahali popote uongozi wa Chadema ulipomsifia Samia anaupiga mwingi, kama una ushahidi niwekee hapa niuone, maneno ya pembeni (hasa mitandaoni) ya wanachama wa Chadema yasichukuliwe kama tamko rasmi la chama.
 
Back
Top Bottom