Kigogo sio mtu wa kumuita Tundu Lissu mshamba, akemewe

Kigogo sio mtu wa kumuita Tundu Lissu mshamba, akemewe

Nilitaka nisimjibu huyo jamaa Ila umasaidia kumjibu
Huyo jamaa either amelewa au hajui lolote kuhusu CCM
Yaani kabisa anaamini mama Samia alikuwa na nia nzuri na chadema? Ili ?
Anasema eti mama alikuwa na nia nzuri, lakini kasahau kuwa mama Samia huyohuyo alipiga marufuku mikutano ya siasa ambayo ipo kikatiba.
Kwani Katiba ni swala la Chadema? Mama kasema swala la katiba apewe muda kidogo sisi wengine tumemuelewa ila Mbowe kashindwa kumuelewa anavuna alichopanda
 
Mimi huyo kigogo hata sijawahigi ku mu follow maana siko Twitter hata kumshambulia sana magufuli baadhi ya vitu vya magufuli alikuwa ananikera kweli kweli hasa kushabikia ugonjwa wake, na baada ya magufuli kufa ili asipotee akajifamya timu CDM damudamu vile nao walikuwa Wana mchukia magufuli. So mtu yoyote anayeshambulia wengine ukiwa rafiki naye ni swala la mda tu na yeye kukugeuka.
weraweraaaaa! Wamegeukana. Mfyuuuuuuu!
 
Mshamba ni nani?

Mshamba ni yule anayejificha nyuma ya kibodi na kuwashambulia wengine au anapambana kwa kujitokeza na kuongea bila kupepesa macho kama Tundu Lissu anavyofanya?

Mshamba ni nani yule aliyeanza kupigania haki toka akiwa shule ya msingi, Sekondari, JKT na kuendelea au yule aliyeanza kujificha nyuma ya kibodi baada ya serikali kuvunja nyumba yake Kimara?

Mshamba ni yupi? Ambaye anaweza kumtukana kila mtu kisa tu kamkosoa au ni yule anayetumia hoja kujibu hoja za wale wote wanaomshambulia?.


Kuwablock watu wanaomkosoa kwenye post zake sio ushamba? Yaani mtu anapokukosoa ni adui yako wewe ni malaika Mbona Tundu Lissu hata Siro hajawai kumtukana ila uwa anamjibu kwa hoja?

Kwangu Mimi mshamba ni yule asiyejua anafanya nini, Anataka nini, Anapataje lini na wapi? Kumtukana kila mtu ni ushamba sana.

Imagine mtu anamtukana na kumzalilisha mtoto kama Zuchu au Nandy watu ambao hawaelewi maana ya siasa ni nini baada ya kuwapa elimu ya uraia wewe unatoka kuwatukana tu and you don't care!

Kwa taarifa Kigogo ni mtoto mdogo mno kwenye siasa za nchi hii harakati zako hazijafikisha hata miaka 10 wakati Tundu Lissu ameanza harakati miaka ya 1990 wewe jiulize ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini?

Kigogo awaulize waliokuwepo kwenye utawala wa Mkapa walivyopambana na Tundu Lissu na Lissu kushinda miaka huyo hata twitter ilikuwa hakuna.

Waulize waliojaribu kumhonga Tundu Lissu kwenye utawala wa Mkapa ili aache kuwatetea watu waliokuwa wanatolewa maeneo ya migodi kwa nguvu kwenye mikoa ya Shinyanga, Mpanda, Tabota, Geita, Mara na Kagera watakupa majibu.

Lissu angekuwa mshamba si angechukua tu pesa za wazungu na kuachana na kuwatetea wananchi?

Tundu lissu miaka yote amekuwa akifanya kazi field tena akiwa sambamba na mke wake akiwa front line kabisa nafikiri hata mwaka Jana alipokuja kufanya kampeni bado mliona alivyokuwa akisumbuana na Police kule Nyamongo na kwingine.

Sasa wewe ndugu yetu unamuita mtu mshamba ambaye yupo ulaya kwa kufanyiwa operation zaidi ya 25 baada ya kupigwa risasi halafu wewe upo ulaya nyuma ya kibodi.

Afadhari Lissu hata akifa leo Mungu akipenda historia ya Maisha yake tayari kashaimaliza historia aliyonayo ni kubwa mno.

Washamba ujificha, Washamba upanic, Washamba ujifanya wanajua kila kitu ili wasikosolewe, Washamba uzusha, hakika Washamba wakikosa ajenda ya kusimamia uwa wanaona kila binadamu ni adui wa maendeleo yao.

Wanaharakati wote duniani uwa hawapambani na mtu uwa wanapambana na mifumo, Jifunze kwa wanaharakati kama wakina Martin Luther King JR na wengine walipambana na mifumo na wakaja kushinda hata kama walikuwa hawapo tena.

Yaani unamtukana Tundu Lissu halafu unamsifia Mbowe? Wakati Mbowe na Tundu Lissu ufahamu hata walikutana vipi?

Kama wewe ni mwanamageuzi kweli njoo na I'd yako original na uje front line uongoze maandamano unayoyapigia kelele, njoo uanzishe chama ukiendeshe kiwe kikubwa kama angalau ACT.

Lissu mageuzi na mapambano aliyoyafanya yanatosha kabisa hata leo akistaafu siasa ila najiuliza kigogo ameshafanya kitu gani zaidi ya kutukana watu?

Mambo ya kuita watu washamba ni ushamba pia.
View attachment 1879158View attachment 1879160
UGAIDI hautawaacha salama-mchoma nyumba yenu moto- jitazameni.
 
huyo kigogo2014 kama anajiamini atoke hadharani asijifiche nyuma ya keyboard 😎
 
Mkuu

Acha uongo

From school mpaka sasa,everybody knows Lissu's reputation kwenye analytical skills

Kigogo kaongea mataputapu yake just one Lissu responce watu wameona difference kabisa.

Lissu is a rare nigga,a scholar,he is a wonder,rare breed....

Inapokuja kwenye kutumia akili,high brain power,Lissu beats Kigogo with easy kabisa

Tatizo Lissu is quiet ahead of him brainwise,thats the problem..he cant argue shit with him,yeye anaishia kutukana!
Lissu kama angekuwa IQ kubwa asingeunga mkono suala la kijana wetu DIAMOND ambalo chadema iliishia KUAIBIKA,
Asingeuingia mkenge wa MAKANIKIA suala ambalo liligusa moja kwa moja kwenye taaluma yake.
LISSU ana IQ ya kawaida sana,ila kama una IQ ndogo ndio utaona ana IQ kubwa
 
TOO LATE,,KWANI AMETENGEZA CHUKI HADI MAGUFURI HADI AKAUWAWA,,HUKU AKINA SSH WAKIMUAHIDI VYEO ,SAAA HATA VYEO AMEKOSWA NA CAHEDMA HAWAMUUNGI MKONO WAMEBAKI KUBANANA..HADI WANAANZA KUMKUMBUKA MAGUFURI
Vema ukarudi MEMKWA huenda ukaeleweka!
 
Lissu kama angekuwa IQ kubwa asingeunga mkono suala la kijana wetu DIAMOND ambalo chadema iliishia KUAIBIKA,
Asingeuingia mkenge wa MAKANIKIA suala ambalo liligusa moja kwa moja kwenye taaluma yake.
LISSU ana IQ ya kawaida sana,ila kama una IQ ndogo ndio utaona ana IQ kubwa
Rudi shule maana unawaabisha walimu wako!
 
Kigogo lazima akubali alichemka kuhemka kuhusu violence wakati anajua upo mtego wa kisheria ambao ccm na msajili angetumia Kama kigezo Cha kuanza kutaka kuifuta Chadema. Na alipata wafuasi wengi ila Mnyika alivyotoa ufafanuzi watu wakamgeuka kigogo na kumwona Kama anatumika kuwapumbaza Chadema. Lakini pia njia ile aliyotumia Kigogo kwa kuwa hakuna anayemjua na kwa kuzingatia baada ya JPM kuondoka ni kama ameishiwa hoja na anaonekana kumsapoti aliyepo au watu aliotaka wapate madaraka wamepata ndiyo maana Tundu Lissu akamchana.

Kuchanwa ndo kamaindi na watu wamemkacha amebaki kujibizana na kujibu mtu mmojammoja kitu ambacho zamani alikuwa hana muda.

Chadema kukataa ushauri wa Kigogo wametumia mbinu kubwa Sana na Kigogo alipaswa kuwapongeza kwakuona mbali zaidi yake.
Kigogo alijua watu wangemuunga mkono kumtukana Lissu,Alichokiambulia naona kabadili upepo na kuanza kuandika maneno ya kutaka huruma,The guy huwa analewa sana sifa na yupo overrated.
 
Mzee hujui hata kuandika parandesi ya fungu la sentensi mbalimbali iliyokamilika na kuleta maana halafu unasema Lissu ana IQ ndogo?

Pangilia sentensi zako kwanza ndio uje na hoja sasa!
Najua hajanielewa ila narudia tena
LISSU ana IQ ya kawaida sana ila kama IQ yako ni ndogo ndio utaona LISSU ana IQ kubwa.
Habari za sijui parandesi sijui sentensi mi siandiki INSHA hapa
 
Umeandika ukweli sahihi mbowe siku zote alikuwaga na busara na hekima ila licha ya kusikilizwa na kuheshimiwa sijui mbowe ni kichaa gani kilimpanda na kutaka kumfanya Samia aonekane dhaifu ona sasa yuko jela pekee yake. CDM kwa Samia walitumia wrong approach kiasi mama hasikilizii yoyote na CDM itapotea wasipobadilika na kuendeleza harakati bila good calculations, sio siri napenda mabadiliko ila mbowe na CDM walikosa vision ya jinsi ya ku deal na Samia, nchi hii inahitaji upinzani makini usio na mihemko kusaidia taifa.
Unataka upinzani wa aina gani?.Hebu tupe mifano.maana sidhani kama mbowe ana mihemko yoyote zaidi ya kuongea straight kitu ambacho wenye madaraka hawakitaki kwasababu hawana tena uwezo wakujibu hoja kwa hoja ndo maana unaona hizi nguvu zikitumika.Vinginevyo labda unataka upinzani kama wa kina mrema na lipumba ambao haupati misukosuko kwa serikali kwasababu hanaga hoja kinzani na serikali.kama ni hivyo huo unakua tena sio upinzani na nchi inakua haina maana yakua na upinzani.
 
Mpaka unajiuliza nini kimewapata hawa watu ambao kwa Mwendazake waliufyata miaka 5. Mwendazake kawapiga risasi, kavunja Bilicanas na kavunja na mashamba yake, kamchukulia na fedha kwenye akaunti. Hajawahi hata kulalamika.

Samia kamrudishia akaunti, kesi zao za kubambika zikapigwa chini pamoja na ya MDUDE. Halafu wao ndiyo wa kwanza kusema HATUWEZI KUMBEMBELEZA Samia. Shenz taipu Bladifakeni Mbowe
Wewe sema una chuki binafsi na mbowe maana sioni kama una hoja yoyote ya maana.Hiyo cdm unayosema iliufyata kipindi cha magu ni ipi na kesi unazozizungumzia zilitokea kipindi gani kama sio kipindi cha magu.Kipindi cha magu ndio kipindi cdm walikua na wakati mgumu lakini chama kilipambana hadi sasa kipo na ata sasa chama kitatoboa maana haya yanayotokea sasa sio mapya duniani dhidi ya upinzani.Kwahiyo usijifanye cdm ndo inafufuka baada ya samia kua rais wakati cdm haijawai kufa wala kulala.
 
Rais huyu kasema Katiba isubiri apange uçhumi kwanza. Mwendazake alisema Katiba mpya siyo ahadi yake ya kampeni. Hakuna mtu alimuuliza mpaka anakufa.

Huyu ana siku 120 kwenye ofisi kiungwana kabisa kaomba muda. Kwa ushauri wangu tungemuacha hadi mwaka mmoja uishe ndipo tumuulize tena.

Kitendo cha kujifanya tunaijua nchi kuliko yeye na wakati Mbowe na Lissu walishiriki kula Mabilioni ya Bunge la Katiba mwaka 2014 na wasitupatie Katiba siyo FAIR
Kwani hiyo katiba ni kwa ajili ya Chadema?.Mbona kama unawatupia cdm lawama wakati mchakato ulikua chini ya serikali ya chama cha mapinduzi.Hoja ya chadema kuhusu katiba mpya ni hoja kama hoja zingine zinazoweza kutolewa wakati wowote kwasababu ata wakikaa kimya hawana kitakachopungua maishani.Lakini kwasababu ni hoja za maendeleo ya nchi na wenyewe ni platform kuna shida gani ikichokoza hoja la uhitaji wa katiba mpya.mambo mengine peleka lawama kwa Ccm nasio cdm maana hadi hapa cdm imefanya mambo mengi sana ya msingi kama chama.
 
Mpaka unajiuliza nini kimewapata hawa watu ambao kwa Mwendazake waliufyata miaka 5. Mwendazake kawapiga risasi, kavunja Bilicanas na kavunja na mashamba yake, kamchukulia na fedha kwenye akaunti. Hajawahi hata kulalamika.

Samia kamrudishia akaunti, kesi zao za kubambika zikapigwa chini pamoja na ya MDUDE. Halafu wao ndiyo wa kwanza kusema HATUWEZI KUMBEMBELEZA Samia. Shenz taipu Bladifakeni Mbowe

Kesi ya ugaidi nayo utakuwa umeisahau ungeendelea kuiunganisha humo kwenye legacy kabambe ya SSH.
 
Najua hajanielewa ila narudia tena
LISSU ana IQ ya kawaida sana ila kama IQ yako ni ndogo ndio utaona LISSU ana IQ kubwa.
Habari za sijui parandesi sijui sentensi mi siandiki INSHA hapa

Kwa hiyo mwenye IQ kubwa kuliko Lissu ni wewe mkuu?
 
Wewe sema una chuki binafsi na mbowe maana sioni kama una hoja yoyote ya maana.Hiyo cdm unayosema iliufyata kipindi cha magu ni ipi na kesi unazozizungumzia zilitokea kipindi gani kama sio kipindi cha magu.Kipindi cha magu ndio kipindi cdm walikua na wakati mgumu lakini chama kilipambana hadi sasa kipo na ata sasa chama kitatoboa maana haya yanayotokea sasa sio mapya duniani dhidi ya upinzani.Kwahiyo usijifanye cdm ndo inafufuka baada ya samia kua rais wakati cdm haijawai kufa wala kulala.
gigabyte niletee hapa jibu au kauli ya KIFEDHULI yeyote ambayo Mbowe ambayo Mbowe amewahi kutamka au kuandika dhidi ya Magufuli. Leta clip tuione.
 
Back
Top Bottom