Kigoma: Afisa Mtendaji ashtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha za Umma

Kigoma: Afisa Mtendaji ashtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha za Umma

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
TAKUKURU Mkoa wa Kigoma imefungua shauri la Uhujumu Uchumi Na. ECC. 22/2022 katika Mahakama ya Wilaya ya Kibondo, Agosti 29, 2022 dhidi ya aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyaruboya, Boniface Balishimura Kibada.

Bw. Kibada anatuhumiwa kwa makosa ya Ufujaji na Ubadhirifu wa Fedha za Umma pamoja na Kuisababishia Serikali Hasara ya kiasi cha Tsh. 8,640,620/=.

Shauri limepangwa kuendelea kwa uwasilishwaji wa hoja za awali hapo tarehe 13/9/2022 na mshtakiwa yuko nje kwa dhamana.
 
Ukiamua kuiba iba kweli

Yaani serious unafungwa kwa kuiba million yenye single digit kweli huu ni uboya
 
Milion nane inampeleka jela kuna majangili yanatorosha wanyama na wana vyeo
 
Back
Top Bottom