PreGE2025 Kigoma: CCM yawatembeza mabalozi mia sita wa serikali za mitaa kukagua miradi ya maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Karibu mabalozi mia sita wa Chama cha Mapinduzi CCM katika manispaa ya kigoma Ujiji wametembelea miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika mji wa Kigoma ili kujionea maendeleo ya miradi hiyo.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma Cde. Christopher Palangyo akizungumza na mabalozi hao amesema Chama kimeweka mkakati wa kuwawezesha mabalozi mkoa mzima kutembelea miradi ili kuona kazi ambayo imefanywa na serikali ya awamu ya sita.

Pia soma: Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

"Watu wengi wakiwemo wana CCM wanahitaji kujionea ili tunaposema Mama aliahidi na ametekeleza watu waelewe kuwa ni kweli kazi imefanyika na inaonekana" amesema.

Mabalozi hao walipata nafasi ya kutembelea ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya kigoma ambayo tayari imeanza kutoa huduma huku majengo mengine yakiendelea kujengwa, Mradi mwingine uliotembelewa ni ujenzi na ukarabati wa uwanja wa ndege Kigoma ambao unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 46.

Pia walitembelea mradi wa Ukarabati wa meli kongwe Duniani yenye zaidi ya miaka 100 MV. Liemba ambayo inakarabatiwa kwa zaidi ya Shilingi bilioni 36 pamoja na meli ya mafuta MT.Sangara ambayo inakarabatiwa kwa Shilingi bilioni nane pamoja na ujenzi wa soko la Mwanga unagharimu shilingi Bilioni 16.

Mmoja wa mabalozi kutoka kata ya Kitongoni Hussein Abbas amesema hii ni mara ya kwanza mabalozi kupata nafasi ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Serikali na wamejionea kazi kubwa ambayo imefanywa na Serikali.

Akizungumzia ukarabati wa meli, mhandisi Ngenja Dave kutoka wakala wa meli nchini TASHICO amesema Ukarabati wa meli ya kusafirisha mafuta MT. Sangara umefikia asilimia 99 huku wa meli ya abiria na mizigo MV.Liemba ukarabati ukiwa umefikia asilimia 19.

Naye msimamizi wa ujenzi na ukarabati wa uwanja wa ndege Kigoma, Mhandisi Mussa Njengwa amesema katika mradi huo kunajengwa jengo la abiria ghorofa moja, mnara wa kuongozea ndege, sehemu ya kuegesha magari na majengo mengine maalum kwa ajili ya uwanja huo.

 
Sasa Waulize Wakazi Wenyewe Wa Kigoma Wanakwambia Hakuna Lolote "ZILONGWA MBALI, ZITENDWA MBALI "
 
Mabalozi ni wazee ,ila wanajipanga kuhujumu vijana kwa kuwachagulia mafisadi na wezi kuwaongoza vijana
Idadi ya Mabalozi tu wa CCM Manispaa ya Kigoma inawazidi wanachama wote wa Chadema Mkoa wa Kigoma, halafu unadai unahujumiwa kwenye Uchaguzi Mkuu? PUMBAVU!!!
 
HONGERENI SANA CCM. HATA SISI CHAUMA TUTATEMBEZA WAJUMBE WETU WOONE WANAOKULA KWA UREFU WA KAMBA YAO
 
Miradi Gani Sasa hiyo ya maendeleo.Kwa Nini hatuioni hiyo miradi?
Miradi inafanywa kwa kupitia kodi za wananchi ila maCCM yanafikiri yanafanya kwa kutumia hela za SSH "ama kweli CCM ni janga la kudumu!! "👿
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…