Kigoma: Inakuaje Jeshi la Polisi Kuhifadhi Jina la Muhalifu na Amekamatwa

The Eric

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
6,446
Reaction score
10,976
Wana muungano eeeh

Tunaomba Mh. Raisi Samia aliangalie hili mara mbili yaani polisi kigoma wamemkamata muhalifu wa ujambazi na wanasema wamehifadhi jina lake.

Kuna uhalifu wa majambazi kuwapora abiria wa gari njiani uliotokea barabara ya kibondo kasalu, polisi wanasema wamehakiki tukio hilo kutokea na kusadikika ni abiria wa gari aina ya bus kampuni ya scorpion. Abiria waliporwa mizigo yao baada ya gari kuzuiliwa na magogo barabarani.

Licha ya yote polisi walifanikiwa kumnasa jambazi mmoja miongoni mwao walio husika na uhalifu lakini polisi wamesema jina la mtuhumiwa limehifadhiwa.

Now why wasitaje jina lake awajibishwe kama muhalifu.

Source ya taarifa ni ITV media wakuu.
 
Bado najiuliza maswali...je hawa jamaa miaka mitano yote walikuwa likizo kwa kukimbia sauti ya JPM? Maana sasa hivi ni kama fungulia mbwa. IGP ni yule yule, RPCs ni wale wale, ni nini kimetokea mpaka iwe namna hii?
 
Wakimtaja wenzake watasikia na kukimbia mbali. Anakaa mahabusu akihojiwa na kutaja wenzake ambao si tu wa tukio hili. Anakamatwa mmojammoja kimya kimya.
 
Mambo ya kiuchunguzi hayo
Hata ulaya,marekani mambo kama
Hayo yanafanyikaga

Ova
 
Sasa hivi taarifa zinatoka.
Utofauti wa sasa na enzi za utawala wa marehemu meko ni kuwa enzi za meko ujambazi ulishamiri kweri kweri, kilichozuiliwa ni taarifa kwa umma., Watu wakamsifu jiwe kadhibiti majambazi kumbe kadhibiti taarifa za matukio ya ujambazi
Utawala wa mama matukio yameanza kuripotiwa kwenye media
 
Wana muungano eeeh

Tunaomba Mh. Raisi Samia aliangalie hili mara mbili yaani polisi kigoma wamemkamata muhalifu wa ujambazi na wanasema wamehifadhi jina lake.

Kuna uhalifu wa majambazi kuwapora abiria wa gari njiani uliotokea barabara ya kibondo kasalu, polisi wanasema wamehakiki tukio hilo kutokea na kusadikika ni abiria wa gari aina ya bus kampuni ya scorpion. Abiria waliporwa mizigo yao baada ya gari kuzuiliwa na magogo barabarani.

Licha ya yote polisi walifanikiwa kumnasa jambazi mmoja miongoni mwao walio husika na uhalifu lakini polisi wamesema jina la mtuhumiwa limehifadhiwa.

Now why wasitaje jina lake awajibishwe kama muhalifu.

Source ya taarifa ni ITV media wakuu.
Kisheria, Polisi hawana haki wala jukumu la kusema nani ni mhalifu.

Wao wanamshika mtu kama mtuhumiwa, mpaka mahakama ihakiki uhalifu ndiyo mahakama inasema huyu mhalifu.

Hivi ndivyo katiba ya nchi inavyosema. Na si katiba ya Tanzania tu, hiki ni kipengele kipo karibu nchi zote zinazofuata misingi ya haki za kisheria.Kinaitwa "presumption of innocence".

Kifungu hiki ndicho kinazuia Polisi uliyemzidi kutongoza mwanamke kukusema wewe mwizi nakufanya wananchi wenye hasira wakupige mawe na kukumaliza bila makosa.

Tatizo ninaloliona ni la upande wa pili. Polisi wa Tanzania wamezoea kuwahukumu watu kuwa wahalifu kabla ya mahakama haijatoa hukumu, mpaka watu wanategemea Polisi waseme nani mhalifu, kitu ambacho si kazi ya Polisi, ni kazi ya mahakama.

Kwa hivyo, inawezekana Polisi wanamtunzia faragha huyo mtuhumiwa mpaka mahakama imhukumu kwa haki kama ilivyoainishwa kwenye katiba.
 
Broo nmejifunz kitu kipya kupitia comment yako tank u so..
 
Back
Top Bottom