Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia kijana Helman Jonh (23) kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi Selina William (63).
Akizungumza leo Jumanne Februari Mosi 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema kuwa kijana huyo alikuwa akimdai mama yake Sh300, 000.
Amesema tukio hilo limetokea Januari 05 katika kijiji cha Kinonko wilayani Kakonko ambapo kabla ya mama huyo kufariki dunia alijeruhiwa kwa kupigwa na mpini wa jembe na kijana huyo.
Amesema kuwa tukio hilo la mauaji ya Selina ni moja kati ya watu 10 ambao walipoteza maisha katika mkoa huo kwa mwezi Januari kutokana na matukio mbalimbali.
Kamanda Manyama amesema watu wengine tisa walifariki dunia kutokana na matukio tofauti ambayo yamesababishwa na wivu wa mapenzi, ulevi pamoja na watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuuawa na Jeshi hilo katika majibizano ya risasi baada ya kuvamia soko la kijiji cha Nyarugusu kwa lengo la kupora mali.
"Katika hatua za kuzuia uhalifu tumekamata silaha zilizo kuwa zikitumiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika kufanya uhalifu pamoja na kuwashikilia watu sita akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Kabulazwili kutokana na kumiliki silaha aina ya gobole zilizokuwa zikitumika katika uhalifu," amesema Kamanda Manyama.
Chanzo: Mwananchi