Kigoma ni sawa na Makete dini iliingia mapema lakini wamechelewa sana kupata maendeleo, Waha na Wakinga matajiri wa Kariakoo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nimeliangalia jimbo la Muhambwe na kule Kibondo kwa kweli pamoja na mbwembwe za Zitto na Kafulila lakini Kigoma bado ni maskini sana.

Naweza kuufananisha mkoa wa Kigoma na wilaya ya Makete mkoani Njombe kwa akina Jah People, yaani full umaskini

Ila ukipita mitaa ya Kariakoo matajiri ndio hao Waha na Wakinga ila ukirudi vijijini mwao kunatisha.

Nikiukumbuka mjengo wa rip Mengi kule kijijini Machame natamani Wakinga na Waha wangeenda kujifunza somo la kukumbuka nyumbani maana si kwa vijumba vile vya Muhambwe na Kibondo.

Mungu wabariki Waha!
 
Kafulila .....Uvinza
Zitto....Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini
Buhigwe ilimegwa toka Kasulu
 
Wapinzani walituchelewesha sana, Joni
 
Kigoma imetengwa kimaendeleo na serikali kwa muda mrefu, mkoa ambao hata kufika tu kwa bus ni shida unategemea wazawa watajenga kweli huko?
 
Hakuna Waha wa kusema ni kundi noticeable kariakoo Kama ilivyo Kwa wachaga na wakinga

Ubaya wa Waha huwa hawataki kabisa kurudi kwao Kwa hofu za uchawi.Yani kuna Watu nilimaliza nao chuo miaka 10 iloyopita hawajawahi kurudi kabisa
 
Lumumba st wamejaa Waha.

Pale katikati karibu na Ujiji G/H ndio usiseme ni waha watupu.

Nenda msikiti wa Manyema utajua kama ni wachache!
 
Mkuu sina uhakika kama unaijua vizuri historia ya makabila ya mkoa wa Kigoma. Ukweli ni kwamba kabila lililowahi kufika na kujenga zaidi kariakoo ni wamanyema ambao wengi wao wanatokea ujiji, mwanga, buzeba zeba na sehemu zingine za Kigoma mjini.

Hao waha unaosema hapa, wengi wao wanaishi au wanatokea Kigoma vijijini na ni moja kati ya makabila yaliochelewa kuja mjini na sio tu Dar hata huko Kigoma mjini kwao kwenyewe wameanza kufika miaka hii.

Nimeshawahi kufanya biashara mkoani Kigoma, kwahiyo naifahamu sana historia ya mkoa huo na makabila yake kwa ujumla.
 
Lumumba st wamejaa Waha.

Pale katikati karibu na Ujiji G/H ndio usiseme ni waha watupu.

Nenda msikiti wa Manyema utajua kama ni wachache!
Mkuu hiyo mitaa yote unayosema imejaa kabila la wamanyema, na hata huo msikiti wa "manyema" waliupa jina la kabila lao kwa vile ndio walikuwa wengi kariakoo na ndio pia waliotangulia kufika mjini.
 
Lumumba st wamejaa Waha.

Pale katikati karibu na Ujiji G/H ndio usiseme ni waha watupu.

Nenda msikiti wa Manyema utajua kama ni wachache!
Waha wa Kkoo wengi ma Ostadhi. Wengi wao Wana asili ya Ujiji. Ni wanazuoni wazuri wa dini lakini Elimu dunia hawana. Ni wabishi, na wapenda Uongozi.
Suala la maendeleo kwa mkoa wa Kigoma in general, linasababishwa na serikali ya CCM. Wakati Kilimanjaro wana barabara za lami mpaka mashambani Marangu, Kigoma hakuna hata lami ya kuunganisha mkoa na mikoa/nchi jiraani.
Wakati mfuko wa sementi unauzwa Elf 14000/- Mikoa mwingine, Kigoma Bei yake ni 23-24k. Bei ya mabati ndo usiseme. Ni Mambo mengi tuu ambayo yameifanya Kigoma ibaki Kama ilivyo.
 
Nikiukumbuka mjengo wa rip Mengi kule kijijini Machame natamani Wakinga na Waha wangeenda kujifunza somo la kukumbuka nyumbani maana si kwa vijumba vile vya Muhambwe na Kibondo.
Inawezekana hao waha wa Kariakoo siyo wa Muhambwe ni wa Kigoma mjini
 
Nimeliangalia jimbo la Muhambwe na kule Kibondo kwa kweli pamoja na mbwembwe za Zitto na Kafulila lakini Kigoma bado ni maskini sana.

Naweza kuufananisha mkoa wa Kigoma na wilaya ya Makete mkoani Njombe kwa akina Jah People, yaani full umaskini

Ila ukipita mitaa ya Kariakoo matajiri ndio hao Waha na Wakinga ila ukirudi vijijini mwao kunatisha.
Nikiukumbuka mjengo wa rip Mengi kule kijijini Machame natamani Wakinga na Waha wangeenda kujifunza somo la kukumbuka nyumbani maana si kwa vijumba vile vya Muhambwe na Kibondo.

Mungu wabariki Waha!
75% ya majimbo yote nchini yapo kama hilo la Muhambwe na CCM ndio waliotufikisha hapa! CCM ndio kikwazo cha maendeleo katika Nchi yetu!
 
Endelea kuvimbiwa Chipsi za viazi kutoka Makete. Nafhani Unazungumzia miaka ya 1975 ikiwa ni sehemu ya Wilaya ya Njombe. Wasalimie Lumumba FC
 
Kigoma imetengwa kimaendeleo na serikali kwa muda mrefu, mkoa ambao hata kufika tu kwa bus ni shida unategemea wazawa watajenga kweli huko?
Serikali nyingi za kiafrika zinapenda Sana kuifanya mikoa ya pembezoni na mipakani kama buffer zones....na bila Shaka wanasingizia sababu za kiusalama na Kwa hapa TZ huko ndio uperekwa wajeda kuongoza..kama Kambi vile...kama nchi hatujaona na kuzitumia fursa za kupakana na nchi nyingine instead sie tumekodolea bandari tuu..Damn! I wish I was a politician.
 
Nimeliangalia jimbo la Muhambwe na kule Kibondo kwa kweli pamoja na mbwembwe za Zitto na Kafulila lakini Kigoma bado ni maskini sana.

Naweza kuufananisha mkoa wa Kigoma na wilaya ya Makete mkoani Njombe kwa akina Jah People, yaani full umaskini

Ila ukipita mitaa ya Kariakoo matajiri ndio hao Waha na Wakinga ila ukirudi vijijini mwao kunatisha.
Nikiukumbuka mjengo wa rip Mengi kule kijijini Machame natamani Wakinga na Waha wangeenda kujifunza somo la kukumbuka nyumbani maana si kwa vijumba vile vya Muhambwe na Kibondo.

Mungu wabariki Waha!
Sehem. Zote alizopita mwarabu hazijawah baki salama mpaka leo kuanzia tabora unyanyembe moja uswahili magomeni , mwarabu analaana sana, anajua ugomvi na kupigana na kuoa wake wengi basi

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Lumumba st wamejaa Waha.

Pale katikati karibu na Ujiji G/H ndio usiseme ni waha watupu.

Nenda msikiti wa Manyema utajua kama ni wachache!

Zamani siku hizi hawana chao Kariakoo,sana sana wapo Msikitini wa Manyema.
 
Tatizo la watu wa kigoma kukosa maendeleo ni la wana kigoma wenyewe shida ya watu wa kigoma miaka ni imani potofu
 
Sehem. Zote alizopita mwarabu hazijawah baki salama mpaka leo kuanzia tabora unyanyembe moja uswahili magomeni , mwarabu analaana sana, anajua ugomvi na kupigana na kuoa wake wengi basi

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
Punguza ujinga na jazba. Jikite kwenye hoja ya msingi. Unajaribu kuchepusha mjadala kutoka kwenye mada ya msingi na kuleta "UARABU". Kwa yeyote mwenye kuifahamu historia atagundua mara moja nini unakusudia. Hapa Mimi sioni laana ya Mwarabu imetoka wapi? Naomba nitoe somo kidogo, Kilwa na Zanzibar enzi za mwarabu walipiga hatua kubwa ya maendeleo kiasi cha kumiliki sarafu yao wenyewe. Wafanya biashara walitoka pande mbalimbali za ulimwengu kuja Kilwa na Zanzibar lkn baada ya kuingia ukoloni na baadae uhuru kinachoendelea Kilwa na Zanzibar ni aibu. Ingefaa ndugu mchangiaji uwe mkweli, tatizo ni waarabu au ni wakoloni na baadae mfumo uliorithiwa na viongozi weusi kwa kudumaza maendeleo katika maeneo yaliyokuwa na waarabu wengi hapo awali?
 
Back
Top Bottom