Kigoma: Nusu ya wanafunzi hawajafanya mtihani wa Darasa la Saba, utoro watajwa

Mungu atunusuru,wengi wao wamekimbilia mikoani kuwa wadada wakazi na machinga...
Wamejazana mitaani wakiuza chai na mitumba..wengine wanadeki na kuosha vyombo mijini tu..
Yaani kigoma,ukerewe,kagera,na visiwa vyote vya kanda ya ziwa ...ilo ni tatizo
 
Ukweli elimu inayotolewa na serikali haina maana....umfanyishe nani mitihani ya kukaririshwa na maisha yenyewe haya....
 
Elimu yenyewe hata kama wewe ni msomi huoni hamasa ya kumshawishi na mwingine asome. Ni mwendo wa kusoma historia ya vitu badala kujifunza kuvifanya vitu vitokee. Kwa historia hizi zinazoendelea kufundishwa nawashngaa hata wanaosema elimu ni Ufunguo wa Maisha. Elimu ya bongo inachosha
 
Kama wamesoma na hawajafanya mtihani unahitimishaje kuwa watabakia wajinga?

Nyie ndiyo mnaoamini kufanya mtihani na kufaulu ndio kuondoa ujinga.

Unataarifa kuwa kunahatua mitihani inatarajiwa kufutwa kabisa?
 
Elimu ya msingi ni lazima kwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule. Sasa nafikiri kuna haja ya kuwawajibisha wazazi wa watoto ambao watatega kufanya mtihani au kuonesha utoro wa namna yoyote ile.
Kama wazazi watawajibishwa inabidi na serikali pia iwajibishwe kwa kushindwa kutengeneza fursa za kutosha za ajira kwa vijana waliosoma,,, sheria iwe ni msumeno isimbane mtu mmoja
 
Matokeo ya kudharau sekta binafsi na wadau wa maendeleo kwenye kutafuta solution ya matatizo ndio matokeo yake haya..

Nakiri kwamba niliwapelekea tamisemi mfumo wa kudhibiti mahudhurio ya watoto wa shule tena bure kwa kuwashirikisha wazazi wao kila siku ila walichonijibu ni kuwa wanao teyari sasa hii idadi kubwa hivi imeshindwa kufanya mtihani kisa utoro kwann huo mfumo wao usingesaidia kuzua haya..

Hii nchi watendaji wa serikali mna mapuuza sana
 
Harafu huu ni mkoa, makamu wa, raisi anatokea, kuna mwanasiasa machachari wa huko,
Wote wapo bize kushangilia ulaji wa ccm.
 
Hakina maana ni useless takataka kabisa wala sina muda nacho
Unaona takakata si kwa sababu ni karatasi unayomiliki ila kwa sababu ya kile kilichobaki kichwani baada ya kukitafuta kwa zaidi ya robo ya maisha yako!

Kifupi ndicho kinakuweka mjini
 
Kama wazazi watawajibishwa inabidi na serikali pia iwajibishwe kwa kushindwa kutengeneza fursa za kutosha za ajira kwa vijana waliosoma,,, sheria iwe ni msumeno isimbane mtu mmoja
Serikali inaweza kusema haikusomeshi ili ikuajiri.
 
Ni ukweli unaosikitisha sana. Nilikuwa mkoa fulani nikakuta fundi anafanya finishing nyumba fulani na ana vibarua. Nikamuuliza alisomea wapi kazi hii. Akanijibu nikasome ili iweje ikiwa vibarua wangu hawa wawili ni graduate wa sheria?

Niliumia sana.
Hii imenikumbusha mbali aiseeee.
 
Very true
 
Wengi ni wakimbizi kutoka congo na Burundi wazazi wao wanawaza vita tu sasa elimu ya kibongo itawasaidia nini? Wale watanzania wanajua umuhimu wa elimu na ndiyo waliofanya mtihani
 
Elimu imekuwa useless ukijua kusoma, kuandika na kuhesabu inatosha.

Hakuna bright future kwenye elimu ya bongo.
Kuna point hapa Ila nashauri mtoto afike angalau kidato Cha nne,kwani ndio elimu ya msingi kwa Sasa.
 
Jamaa wamekanusha wakati taarifa ikitokea na Habari Leo 🤪🤪

Sio Kila kitu ni kukanisha Ili kificha tatizo

View: https://www.instagram.com/p/CxNXsvCgcmU/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Umenena, japo wapo wanaoponda ooh mkwere Mbaya, wakati watu wamelamba kazi bwelee, watoto walisoma kwa Moyo wanajua nikimaliza nipo kazini, Leo hii wasomi waendesha bodaboda,masaidia fundi yaumiza Moyo kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…