Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
HakiweziKifupi ndicho kinakuweka mjini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HakiweziKifupi ndicho kinakuweka mjini
Sasa wewe imagine wasomi wenyewe ndo design yako. Unadhani wazazi watahamasika kusomesha watoto?Hali hii inasikitisha sana, yaani nilidhani Wazazi walishabadilika kumbe Bado watu wanaona Elimu Haina maana hadi leo hii, duu.
My Take: Kwa Hali hii, sidhani kama kuna siku wajinga watakuja kuisha hapa Tanzania.
========
KIGOMA; WAKATI wanafunzi wa darasa la saba wakimaliza mtihani wa elimu ya msingi nchini kote leo, imeelezwa kuwa mkoani Kigoma nusu ya wanafunzi hawakuweza kufanya mtihani huo kwa sababu mbalimbali ikiwamo utoro.
Ofisa Elimu wa Mkoa Kigoma, Paulina Ndigeza akizungumza mjini hapa jana alisema kuwa wanafunzi 53,000 walifanya mitihani yao kati ya wanafunzi 102,948 waliotarajiwa.
Ndigeza alisema pamoja na changamoto hiyo ya idadi kubwa ya wanafunzi kushindwa kufanya mtihani, alibainisha kuwa mwamko mdogo wa wazazi kuwasimamia watoto wao imekuwa changamoto kubwa na kwamba mkoa umeshaanza kutekeleza mikakati ya kupambana na changamoto hiyo.
HabariLeo