Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi mkoani Kigoma.
Watu hao wanaodaiwa kupanga kufanya unyang’anyi kwa kutumia silaha, wanadiwa kukutwa bunduki moja AK 47, magazine 1 ikiwa na risasi 10, bunduki iliyotengeneza kienyeji, visu viwili, panga na marungu matatu.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Julai 31, 2025 katika Kijji cha Kigendeka, Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma, ambapo askari waliokuwa katika doria walibaini njama za watu waliokuwa na lengo la kufanya unyang’anyi kwa kutumia silaha.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Philemon Makungu, watu hao waliofunga barabara walidhibitiwa na polisi baada ya majibizano ya risasi yaliyosababisha vifo vya watu watatu.
“Kwenye majibizano hayo ya risasi, majambazi watatu ambao bado hawajatambuliwa kwa majina wala anuani za makazi, wameuawa baada ya kujeruhiwa na risasi, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo kwa utambuzi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linaendelea kuwaomba wananchi kufanya shughuli halali za kujingizia kipato zinazotambulika kwa mujibu wa sheria, tutaendelea kuchua hatua za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na uhalifu.