Ahaaaa ahaaaa nimecheka kwa nguvu, eti najitahidi kuchangia lakini nina ubora duni wa hoja. Inaonekana umekuja na marking scheme hapa jukwaani, hivyo maelezo yoyote yaliyo nje ya matamanio yako, ni Uduni wa hoja!
To be honest, nashukuru umeniquote kwa maelezo marefu, lakini sijui umetoa majibu yako kwenye post ipi, maana ulichoniquote kina uhusiano mdogo na hii post yako. Huenda umefanya hitimisho la kila post yangu kwenye uzi huu, ama kwa kughafilika umebeba post kadhaa za wachangiaji wengine, kisha ukafanyia hitimisho kwangu. Kwa maneno marahisi nimeona furushi la sentensi za kiswahili, zisizo na mahusiano yoyote na ulichoniquote.