Kigoma, Uvinza: Wananchi waua Askari wa akiba 3 waliodaiwa kutaka kufanya unyang'anyi wa ng'ombe

Kigoma, Uvinza: Wananchi waua Askari wa akiba 3 waliodaiwa kutaka kufanya unyang'anyi wa ng'ombe

Taarifa sahihi ya mdau aliyekuwa kwenye tukio huko Uvinza ni kama ifuatavyo: Siku ya tarehe 31.01.2023 timu ya doria kutoka Halmashauri ya wilaya ya Uvinza yenye jumla ya watu 22 ilienda kufanya doria kwenye misitu iliyohifadhiwa, ikiwemo msitu wa Kijiji cha CHAKULU. kwenye timu hiyo kulikuwa na maofisa kadhaa ikiwemo afisa misitu wa wilaya ya Uvinza na afisa utalii wa wilaya. Wengine ni maaskari kutoka TFS, VGS na migomba.

Timu ya doria ikiwa kwenye msitu wa hifadhi wa Kijiji cha CHAKULU ilikamata kundi kubwa la mifugo iliyokutwa hifsdhini. Baada ya mifugo kukamatwa wenye mifugo walianza kuitana kwa kutumia filimbi na kupiga mwano/mayowe. Wakati timu ya doria ikiendelea kuswaga mifugo kundi kubwa la wafugaji wa Kisukuma lilitokea likiwa na mawe, marungu, mapanga na silaha nyingine za jadi na kuanza kupambana na timu ya doria ili mifugo yao iachiwe.

Baada ya jitihada za kupiga risasi juu kutishia kutokuzaa matunda na wafugaji kuzidi kuongezeka timu ya doria iliamua kuachia mifugo na kuanza kukimbia yalipo magari yao. Wafugaji waliendelea na mashambulizi na hatimaye kufanikiwa kuwauwa watu 4 na kujeruhi kadhaa. Waliouwawa ni Afisa misitu wa wilaya ya Uvinza na migomba 3.
 
Dah!! Sasa Kwa nini walimuua huyo mfugaji badala ya kumkamata na kumpeleka kwenye mkono WA sheria!? Anyway Naona inabidi busara itumike zaidi kuliko kuwakamata na kuwatesa wananchi!! Dhuluma dhuluma dhuluma
Swali halijibika kirahisi hadi apatikane wakili makini
 
Taarifa sahihi ya mdau aliyekuwa kwenye tukio huko Uvinza ni kama ifuatavyo: Siku ya tarehe 31.01.2023 timu ya doria kutoka Halmashauri ya wilaya ya Uvinza yenye jumla ya watu 22 ilienda kufanya doria kwenye misitu iliyohifadhiwa, ikiwemo msitu wa Kijiji cha CHAKULU. kwenye timu hiyo kulikuwa na maofisa kadhaa ikiwemo afisa misitu wa wilaya ya Uvinza na afisa utalii wa wilaya. Wengine ni maaskari kutoka TFS, VGS na migomba. Timu ya doria ikiwa kwenye msitu wa hifadhi wa Kijiji cha CHAKULU ilikamata kundi kubwa la mifugo iliyokutwa hifsdhini. Baada ya mifugo kukamatwa wenye mifugo walianza kuitana kwa kutumia filimbi na kupiga mwano/mayowe. Wakati timu ya doria ikiendelea kuswaga mifugo kundi kubwa la wafugaji wa Kisukuma lilitokea likiwa na mawe, marungu, mapanga na silaha nyingine za jadi na kuanza kupambana na timu ya doria ili mifugo yao iachiwe. Baada ya jitihada za kupiga risasi juu kutishia kutokuzaa matunda na wafugaji kuzidi kuongezeka timu ya doria iliamua kuachia mifugo na kuanza kukimbia yalipo magari yao. Wafugaji waliendelea na mashambulizi na hatimaye kufanikiwa kuwauwa watu 4 na kujeruhi kadhaa. Waliouwawa ni Afisa misitu wa wilaya ya Uvinza na migomba 3.
Sio kwamba askari ndiye aliyeanza kumuua msukuma??
 
Back
Top Bottom