Uchaguzi 2020 Kigoma: Viongozi watano wa CHADEMA mbaroni kwa kukutwa na kadi 14 za mpiga kura

Uchaguzi 2020 Kigoma: Viongozi watano wa CHADEMA mbaroni kwa kukutwa na kadi 14 za mpiga kura

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Polisi Kigoma wanawashikilia watu watano (Viongozi wa Chadema) Kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko kwa kukutwa na vitambulisho 14 vya kupigia kura kinyume cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.

RPC Kigoma James Manyama amesema wanachunguza malengo ya kuwa na kadi zisizo za kwao ni yapi.

------

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma imewatia mbaroni watu watano viongozi wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kakonko wakituhumiwa kukutwa na kadi 14 za mpiga kura huku ikielezwa haijabainishwa madhumuni ya kukutwa na kadi hizo.

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, James Manyama alisema hayo akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari Mjini Kigoma Jana ambapo alionya wananchi kutokubali kutoa kadi zao za kupigia kura kwa mtu yeyote.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Hezron Vicent (45), Ezekia Samakere (40), Sheby Kasuka (21), Helson Miniho (38) na Denis Lubuye (30) ambao wote ni viongozi wa CHADEMA kata ya Gwanumpu.

Kamanda Manyama alisema kuwa watuhumiwa walifanyiwa mahojiano lakini hawakuwa majibu yenye mashiko kisheria kuonyesha kwanini walikuwa wanahifàdhi hizo kadi.

"Baada ya mahojiano watuhumiwa walieleza kuwa walikuwa na hizo kadi kwa ajili ya kwenda kutoa kopi kwa ajili ya kupeleka kwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa Jimbo la Buyungu kwa ajili ya mchakato wa kuandikisha vitambulisho vya mawakala wa chama hicho Jambo ambalo kisheria halikubaliki," Alisema Kamanda Manyama.

Hata hivyo Kamanda Manyama alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343 marejeo ya mwaka 20202 kifungu Cha 90(2) ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kumiliki kadi ya kupiga kura ya mtu mwingine bila kufuata taratibu.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa watuhumiwa ambao wawili hawakuwa na kadi za kupiga kura walikuwa na Nia ovu ya kuwanyima wamiliki wa kadi hizo haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.

Akizungumzia kadi hiyo Katibu wa CHADEMA mkoa Kigoma,Shaban Madede alisema kuwa hakukuna na Nia yeyote ovu katika kadi hizo na kwamba viongozi hao walikuwa wakisaidia suala la kutoa nakala kadi hizo waweze kuziwasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi kwa ajili ya mchakato wa vitambulisho vya mawakala.

" Kule kijijini hakuna sehemu ya kutoa nakala (Photo Copy) hivyo viongozi walikusanya hizo kadi kuja nazo Mjini wasaidie kutoa nakala na kurahisisha mchakato lakini mwisho wa siku wamekamatwa kwa madai ya kutaka kuzifanyia hujuma wakati siyo kweli," Alisema Madede.

Chanzo: Habari Leo
 
Cdm hawawezi kuwa wamenunua hizo kadi Kama wafanyavyo maccm,Kuna uwezekano zilikuwa ni kadi za wanawake wamezihold ,si unajua wanawake akili zao,la sivyo tusubirie uchunguzi
 
Polisi Kigoma wanawashikilia watu watano (Viongozi wa Chadema) Kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko kwa kukutwa na vitambulisho 14 vya kupigia kura kinyume cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.

RPC Kigoma James Manyama amesema wanachunguza malengo ya kuwa na kadi zisizo za kwao ni yapi.
Safi sana jeshi la police
 
Hapo kuna maswali mengi yasiyo na majibu.

Pindi polisi wanapokuja kupekua kwako ni sharti wao kukaguliwa kabla ya kuingia kupekua,kwa wananchi wengi hawajui huu utaratibu hivo kama polisi wana mission yao ni ngumu kwa wananchi wengi kufanya hivo,hivo kujikuta wameingia kwenye mtego.

Endapo mtuhumiwa atakana mahakamani,na kusema hajui chochote kuhusu hiyo mikadi,na akambana polisi kuwa ulipo ingia ndani kwangu nani alikufanyia checkup kujiridhisha hujaja na haya makadi yako,polisi atakuwa matatani
 
Chadema hawawezi kuwa wamenunua hizo kadi Kama wafanyavyo maccm, Kuna uwezekano zilikuwa ni kadi za wanawake wamezihold si unajua wanawake akili zao,la sivyo tusubirie uchunguzi
Kwanini wasiweze
 
Cdm hawawezi kuwa wamenunua hizo kadi Kama wafanyavyo maccm,Kuna uwezekano zilikuwa ni kadi za wanawake wamezihold ,si unajua wanawake akili zao,la sivyo tusubirie uchunguzi
Kuna Makamanda wanawake wengi tu humu wapambanaji. Kwahiyo unashauri washikiwe kadi zao? Ngoja waje.😀
 
Hii habari imekaa ki udaku zaidi. Kama ndivyo ilivyotolewa, basi hiyo RPC ana tatizo.
 
Back
Top Bottom