Uchaguzi 2020 Kigoma: Viongozi watano wa CHADEMA mbaroni kwa kukutwa na kadi 14 za mpiga kura

Uchaguzi 2020 Kigoma: Viongozi watano wa CHADEMA mbaroni kwa kukutwa na kadi 14 za mpiga kura

Cdm hawawezi kuwa wamenunua hizo kadi Kama wafanyavyo maccm,Kuna uwezekano zilikuwa ni kadi za wanawake wamezihold ,si unajua wanawake akili zao,la sivyo tusubirie uchunguzi
Unamaanisha akili za wanawake wa chadema ni nzito kama futari ya magimbi?
 
dah Cdm hapa imekua tatizo hilo kosa kubwa sana la.kutaka kuviruga elcntioin.
 
haya sasa ule msemo wa nyani halioni kundule...
 
Thibitisha kamanda
Unaishi nchi gani? Hukuziona fomu hapa jamvini zilizokuwa zinatembezwa na viongozi wa CCM wa vitongoji na mitaa wakiorodhesha wapiga kura na namba zao za simu.
 
Maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi 2020kifungu cha 9.8(ii) Kinasema yafuatayo:

(ii) Utambulisho wa Mawakala wa Vyama vya Siasa

Kwa mujibu wa kanuni ya 50 (6) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na

Wabunge za mwaka 2020 na kanuni ya 43 (6) ya Kanuni za Uchaguzi wa

Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2020, barua ya

utambulisho wa kila wakala itakayowasilishwa na chama iainishe kituo

alichopangiwa na iambatishwe na picha mbili (Passport size) zilizopigwa si

zaidi ya miezi mitatu.

Aidha, kwa mujibu wa kifungu 57 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,

Sura ya 343 chama kitaruhusiwa kuteua wakala mbadala endapo

aliyeteuliwa awali amefariki au ameshindwa kutekeleza majukumu ya

uwakala. Katika kurahisisha utekelezaji wa suala hili, sambamba na

orodha ya mawakala wa vituoni, vyama viwasilishe majina mawili ya

mawakala wa ziada kwa kila kata ambao watatumika kama mawakala

mbadala iwapo itahitajika.

Endapo wakala hana picha anaweza kuwasilisha nakala mbili za

mojawapo ya vitambulisho vifuatavyo: -

(a) Kadi ya mpiga kura;

(b) Kitambulisho cha Taifa;

(c) Leseni ya udereva; au

(d) Pasi ya kusafiria

Kama walikuwa wanaenda kutoa copy kwa madhumuni ya utambulisho wa mawakala, kuna kosa gani hapo? au kiueledi kila wakala asafiri kilometa kadhaa kwenda penye huduma ya kutoa copy!
 
Polisi Kigoma wanawashikilia watu watano (Viongozi wa Chadema) Kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko kwa kukutwa na vitambulisho 14 vya kupigia kura kinyume cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi....
Habari leo sio chanzo sahihi cha habari. Liko biased sana
 
Polisi wakinikuta na kadi ya mke wangu watanikamata?

Hoja ya Polisi haina mashiko, hao wameshajieleza vizuri sababu za kuwa na hizo kadi. Polisi Wangethibitisha kama hao ni mawakala au la halafu tuanzie hapo. Polisi watawakosesha hao mawakala haki yao ya kuja kusimamia uchaguzi kwa niaba ya vyama vyao.
 
Dah...mkuu kama unajua wapi wananunua kadi za kupigia kura nielekeze...yangu nauza buku 3 tu 🤭
Kama wewe ni mpigakura wa Upinzani watafute ccm hukohuko uliko watainunua ilimradi ilimradi wagombea wa ccm wasiwe wanakubalika.
 
Jeshi la Polisi linawashikilia viongozi watano wa Chadema katika kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko kwa tuhuma za kukutwa na vitambulisho 14 vya wapigakura, kinyume cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.

Akizungumza Oktoba 21, kamanda wa polisi wa mkoa, James Manyama amesema tukio hilo lilitokea j Oktoba 20, saa 10:00 jioni katika duka la kuuuza vifaa vya shule na ofisi katika kijiji cha Kakonko.

Amesema polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ambao walikuwa katika operesheni ya kuzuia na kukamata wahalifu, walikamata watuhumiwa hao watano wakiwa na kadi hizo.

Amesema watu hao wamevunja Sheria ya Uchaguzi, sura ya 343 na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Akizungumzia suala hilo, katibu wa Chadema mkoa, Shaban Madede amesema viongozi hao walienda kutoa nakala za vitambulisho vya kupigia kura vya mawakala wao na kwamba wangevirudisha baadaye.
 
Back
Top Bottom