Kigoma: Wanafunzi wajisaidia vichakani, vyoo vya shule vyatitia

Kigoma: Wanafunzi wajisaidia vichakani, vyoo vya shule vyatitia

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Wanafunzi katika Shule ya Msingi Kasaba, Kata ya Kidahwe, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia msituni kufuatia shule hiyo kutokuwa na huduma ya vyoo tangu mwaka 2020 baada ya kutitia.

Wakielezea adha hiyo wanafunzi wamesema kwanza hawana maji wala vyoo kwani vilititia na shule ilichimba mashimo machache ya muda ili yawasitiri, ambayo hata hivyo asilimia kubwa hawayatumii kwa kuhofia usalama wake kwani yamekuwa yakibomoka mara kwa mara.

Aidha, wanafunzi hao wameongeza kuwa shule hiyo pia inakabiliwa na upungufu wa madarasa ambayo hulazimisha wanafunzi kurundikana huku kukiwa na vyumba vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi ambavyo hadi sasa havijakamilishwa.

Source: EATV

VYOOOO.jpg
 
Hii ni aibu kubwa sana,
Choo kama choo mpaka waje wengine watusaidie? Ndio maana magu aliweza sana,
Mambo kama haya unakamata tu tajiri moja na kuliamrisha jenga choo fasta vinginevyo
Tunakupigia hesabu, hii mitajiri ina hela ila ni migumu kweli
 
Back
Top Bottom