POTOSHI Kigoma waweka bango la 'Oktoba tunatiki kwa mama'

POTOSHI Kigoma waweka bango la 'Oktoba tunatiki kwa mama'

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha

0_qdaSq-J394HpMGXl.webp
 
Tunachokijua
Uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani.

JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. Rejea kiungo hiki kufuata hatua zote.

Mfano picha hii iliyopigwa mkoani kigoma ikionesha bango lililopo pembezoni mwa barabara lenye ujumbe unaosomeka "Oktoba tunatiki kwa mama"


Je, picha hiyo ni halisi?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia google reverse image search umebaini kuwa picha hiyo iliwahi kuchapishwa mtandaoni mwaka 2009 na imeendelea kutumiwa na vyanzo mbalimbali mpaka 2025 ambapo sehemu ya bango husika linahusu huduma za unyoaji wa nywele (Kinyozi).

Hivyo picha yenye maneno "Oktoba tunatiki kwa mama" imepotoshwa uhalisia kwa kuondoa ujumbe halisi uliokuwapo awali na kupachika ujumbe huo ambao haukuwepo kwenye bango hilo.​
kigoma.jpg
Back
Top Bottom