Kigoma ya sasa siyo kama ya zamani

Kigoma ya sasa siyo kama ya zamani

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Rais Samia Suluhu anaandika historia ya kuwa mmoja kati ya viongozi nchini waliopeleka miradi mikubwa ya kimaendeleo Kigoma na kuubadilisha mkoa wa kigoma kutoka mkoa uliokuwa nyuma kimiundombinu na kuwa mkoa wa kisasa.

Hiyo inatokana na Rais Samia Suluhu kupeleka miradi mikubwa ya barabara, viwanja vya ndege na madaraja, Miradi hii imekuwa na mafanikio makubwa kiuchumi, kuleta maendeleo kwa wananchi pia kwenda kuubadilisha mkoa huo ambao ulikua na adha ya usafiri na usafirishaji.

Kupitia uboreshaji wa miundombinu wananchi wa kigoma wananufaika na kurahisishiwa shughuri za kiuchumi maana kigoma ni mji wa biashara kuna uvuvi na kilimo hivyo sasa wataweza kusafirisha biashara zao kwa urahisi zaidi.

KIGOMA YA SASA SIO KAMA YA ZAMANI KIGOMA YA LEO INASONGA MBELE
 
Muache sasa kurogana mkae hapo hapo kigoma muitumie hiyo miundo mbinu. Sio mjengewe na bado mjazane kwenye treni kwenda daresalama.
 
Vipi kipande cha barabara cha Uvinza - Kaliua kimepigwa lami? Au bado vumbi?
 
Mpaka umenikumbusha ule wimbo wa "Leka dutigite" ngoja nidownload
 
Rais Samia Suluhu anaandika historia ya kuwa mmoja kati ya viongozi nchini waliopeleka miradi mikubwa ya kimaendeleo kigoma na kuubadilisha mkoa wa kigoma kutoka mkoa uliokuwa nyuma kimiundombinu na kuwa mkoa wa kisasa...
Kigoma hii ninayoijua mimi? Samia unamsifia hapa wakati barabara ya kutoka Nguruka Tabora-Uzinza Kigoma mkandarasi anesimama mda mwingine acheni kuendekeza ujinga wa wanasiasa!

Shukruni tu hata utawala wa Magufuli kuwajengea barabra za mitaa na barabara ya Nyakanazi Kakonko kuja mpaka Kibondo kukamilika pia ulijitahidi sana kuanza ufufuaji wa Meli ya MV Liemba na upanuazi wa bandari project ambzo zimelala hata dalili ya kuanza sijaona!

Hata hivyo Kigoma kibaishara bado sana mfano ni kubomolewa kwa soko la wafanya biashara eneo la Mwanga mkono wa kushoto kama unaekelekea barabara ya kigoma ujiji na baadae kubainika kuwa eneo hilo halitakiwi kujengwa maana chini ya ardhi kuna mkondo wa maji!

Cha kujiuliza wakati wanawabomolea wafanya biashra hao wakandarasi na wahandisi wa halmashauri hawakupima na kubainia kuwa chini ya ardhi hiyo kuna mkondo wa maji?

Pia kwa sasahivi upande wa Congo wachina wanajenga viwanda vya simenti,mabati na vyakula mbalimbai hasa upande ya Kalemi Na mji mdogo wa Kabimba!

Biashara hizo za vifaa vya ujenzi kama sementi na nondo na baadhi ya bidhaa za vyakuala kutoka Tanzania vitapungua sana kwenda Congo na kupelekea biashara na makusanyo ya bandari ya Kigoma klupungua!
Fursa hii ya kuifanya kigoma kuwa lango la biashara ilikuwepo hasa kipindi cha Mkapa na JK ila hatukuchangamkia fursa hiyo!

Kigoma kwa sasa kama bandari ni kuhakikisha inajiimarisha sana katika eneo ya biashra ya mafuta ya magari na machine mbalimbali maana ndo bidhaa pekee ya uhakika kusafirisha kutoka Dar mpaka Kalemi na Kabimba!
 
Mkuu Kigoma hii ninayoijua mimi haiwezi kupiga hatua kwa propagnda za wanasiasa!

Sasa kwa upande wa DRC wachina wanajenga viwanda vya kuzalisha material na vifaa vya ujenzi pamoja na vyakula tafisri yake tunaenda kupoteza makusanyo na mzunguko wa pesa kigoma maana watu wa DRC hawatahitajika kuagiza baadhi ya bidhaa walizokuwa wanaziagiza kwetu kwa wingi kama simenti nondo na mabati!
 
Rais Samia Suluhu anaandika historia ya kuwa mmoja kati ya viongozi nchini waliopeleka miradi mikubwa ya kimaendeleo kigoma na kuubadilisha mkoa wa kigoma kutoka mkoa uliokuwa nyuma kimiundombinu na kuwa mkoa wa kisasa.

Hiyo inatokana na Rais Samia Suluhu kupeleka miradi mikubwa ya barabara, viwanja vya ndege na madaraja, Miradi hii imekuwa na mafanikio makubwa kiuchumi, kuleta maendeleo kwa wananchi pia kwenda kuubadilisha mkoa huo ambao ulikua na adha ya usafiri na usafirishaji.

Kupitia uboreshaji wa miundombinu wananchi wa kigoma wananufaika na kurahisishiwa shughuri za kiuchumi maana kigoma ni mji wa biashara kuna uvuvi na kilimo hivyo sasa wataweza kusafirisha biashara zao kwa urahisi zaidi.

KIGOMA YA SASA SIO KAMA YA ZAMANI KIGOMA YA LEO INASONGA MBELE
Miradu ipi mikubwa aliyopeleka?, pathetic, everything was on process,katembelea nyota ya Magufuli
 
Miradu ipi mikubwa aliyopeleka?, pathetic, everything was on process,katembelea nyota ya Magufuli
Yaani kigoma kaka hakuna mradi mpya uliojenga mradi pekee alojenga Samia ni hospital lile jengo la hela za UVICO hakuna upamuzi wa bandari wala ujenzi wa soko kama nilivyoelezwa soko walibomoa sasa mwaka wa pili hakuna kilichofanyika na sababu wanayotoa kuwa chini ya ardhi kuna mkondo wa maji!

Mtu anakuja kusifia ujinga hapa wakati sie tunaokaa na kwenda Kigoma kila mara tunajua hali halisi ya mkoa huo na unakoelekea!
 
Back
Top Bottom