KIGOMA YAANDIKA HISTORIA: Rais Samia kuzindua Ujenzi wa SGR Tabora-Kigoma

Tanzania Railways Corp

Govt Institution
Joined
Mar 23, 2018
Posts
292
Reaction score
690
Katosho 1 Layuot 2026.png

​
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, amesema ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma ni hatua ya kimkakati itakayoiunganisha Tanzania na masoko ya ukanda wa Maziwa Makuu kupitia mtandao wa kisasa wa reli.

Katosho layout b.png

​
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kigoma kuelekea uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo, Prof. Mbarawa amesema reli hiyo yenye urefu wa kilomita 506 na thamani ya takribani dola za Marekani bilioni 2.74 itaunganisha Kigoma na mikoa ya Tabora, Shinyanga, Mwanza, Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam, huku ikiimarisha usafirishaji wa mizigo na abiria ndani na nje ya nchi.

Katosho layout a.png

​
Aidha, amesema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Kigoma kutoka takribani saa 30 zinazotumika sasa kwa reli ya MGR hadi saa nane pekee kwa SGR, pamoja na kuandaa mazingira ya kuunganisha Tanzania na Burundi pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia mtandao wa reli wa kikanda.

Katosho layout c.png

Katosho layout d.png

Prof. Mbarawa amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono na kulinda mradi huo, akieleza kuwa SGR ni nguzo muhimu ya kukuza biashara, uwekezaji na maendeleo ya uchumi wa Taifa na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
 
Kuna haja gani maana jiwe la msingi lishakuwepo.Kwa hiyo hata mkibadilisha reli mawe mtamuita raisi
 
View attachment 3632667
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, amesema ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma ni hatua ya kimkakati itakayoiunganisha Tanzania na masoko ya ukanda wa Maziwa Makuu kupitia mtandao wa kisasa wa reli.
View attachment 3632669
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kigoma kuelekea uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo, Prof. Mbarawa amesema reli hiyo yenye urefu wa kilomita 506 na thamani ya takribani dola za Marekani bilioni 2.74 itaunganisha Kigoma na mikoa ya Tabora, Shinyanga, Mwanza, Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam, huku ikiimarisha usafirishaji wa mizigo na abiria ndani na nje ya nchi.
View attachment 3632676
Aidha, amesema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Kigoma kutoka takribani saa 30 zinazotumika sasa kwa reli ya MGR hadi saa nane pekee kwa SGR, pamoja na kuandaa mazingira ya kuunganisha Tanzania na Burundi pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia mtandao wa reli wa kikanda.
View attachment 3632681
View attachment 3632672

Prof. Mbarawa amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono na kulinda mradi huo, akieleza kuwa SGR ni nguzo muhimu ya kukuza biashara, uwekezaji na maendeleo ya uchumi wa Taifa na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
1000002256.jpg
1000002255.jpg
 
Back
Top Bottom