Kigoma yaipiku Dar na madaraja yake ya waenda kwa miguu ya Manzese na Buguruni, yajenga kivuko chini ya Barabara

Mzee je ikingiaa kwenye ma subways za wenzetu si utapagawa

Ova
 
Kigoma ni Chibokoo!
Kabisa
Nimepita jana kuna soko pale eneo la mnazi moja kabla hujafika CBE koko jirani na mates ya kuongoza magari asiwe umati unaovuka pale zebra crossing kutoka pande zote mbili hadi watu wanapigana vikumbo yaani pale nafikiri panahitaji traffic light za kuongoza watu sio magari wanapovuka kuruhusu upande mmoja mmoja !!!

Pale ukweli panahitaji njia ya chini ya barabara ya wavukaji watu ni wengi na ni full time kunasababisha jam ya watu na magari
 
Mainjinia washirikishe chuo cha ardhi huo ujenzi wa vivuko
Hapo nadhani kwa sababu ndio wataalamu wanapikwa ndio maana wamefanya hivyo chuo kisije dhalilika ingekuwa kosa kubwa kama wangejenga kama Manzese na Buguruni kingeonekana chuo ni bogus
Wakati konoike wanajenga barabara ya Morogoro miaka ya mwanzoni mwa 90, walitaka kujenga kivuko cha chini cha waenda kwa miguu, pale Manzese. Hata hivyo walishauriwa kuwa pale kuna wezi wengi, wakifanya hivyo watu wengi watakabwa, ndiyo wakaamua kujenga daraja.
 
Aliyeshauri kichwa chake kibovu umati wa watu ulio pande zote mbili pale mtu anakabwaje? Kibaka anakimbilia wapi? Sasa lile daraja mtu mzima kweli aweza panda kuvuka barabara? Kuliko dormant lile chukulia una mdogo kichwani hivi waweza panda na mzigo kichwani you mdaraja? Anyway nadhani barabara zingine za mijini zikijengwa waweke umuhimu wa vivuko vya chini ya barabara
 
Waliangalia usalama wakati wa usiku, kumbuka Manzese ya 1993 ilikuwa inatisha.
 
Hii ndio kitu inashangaza kuhusu engineers wa kitanzania. Vivuko vya chini ya barabara ndio practical vya juu havina motivation kuvifuata. Cha manzese kipokipo tu ni mapambo hakitumiki ipasavyo. Suala la drainage kwa vivuko vya chini ya barabara wala sio shida kushughulikia. Hebu tutumie akili dar tunataka vivuko vya chini ya barabara kwa wingi kuokoa ajali za waenda kwa miguu.
Maengineer wanafikiria upigaji tu ndio maana hata miji midogo kama kigali ina flyovers nyingi kuliko dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…