Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Watendaji wa serikali mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia miongozo ya matumizi ya fedha za umma ili kufanikisha mipango ya serikali inayolenga kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Rugwa, baada ya mkoa huo kushika nafasi ya tatu katika kipengele cha mikoa kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandaaji wa Hesabu za Fedha kwa mwaka 2022/2023.
Tuzo hizo, zinazoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), zinalenga kutambua taasisi zinazozingatia viwango vya kimataifa vya uhasibu. Rugwa amewapongeza watendaji wote wa mkoa kwa ushirikiano wao uliowezesha Kigoma kuendelea kuwa miongoni mwa mikoa bora kwa kipindi cha miaka sita mfululizo.
"Kwetu tuzo hii inatoa tafsiri pana na kuonesha kuwa tunatekeleza majukumu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Matumizi ya Fedha kuanzia upangaji wa bajeti na mlolongo wa utekelezaji wa bajeti hiyo katika mkoa na mamlaka za Serikali za Mitaa" amesisitiza Rugwa.