Kigugumizi cha CHADEMA juu ya akina Halima Mdee kinatokana na nini? Sikilizeni Rufaa na mtoe uamuzi wa mwisho

Kigugumizi cha CHADEMA juu ya akina Halima Mdee kinatokana na nini? Sikilizeni Rufaa na mtoe uamuzi wa mwisho

Mshahara wa Katibu na Posho ya Gaidi Mbowe italipwaje lipwaje wakiwafukuza sasa?
 
Msimamo wako au ni msimamo wa katiba,sheria,kanuni!!!???? Yaani mwanasheria/wakili unaacha kufuata katiba,sheria ya vyama vya siasa, kanuni za bunge, sheria ya uchaguzi, na kuwa na msimamo wako!!!?????
Mi nilitegemea yeye kama wakili awe wa kwanza kwenda mahakamani ku-challenge uvunjifu wa katiba, sheria na kanuni lakini yeye anakuwa wa kwanza kushabikia uovu. Shame on him. TLS nayo sahivi ni tawi kuu la CCM
 
Chama kina Siri ambazo hazitakiwi ziwafikie mambugila mbugila

Endelea kufanya yako, yao waaachie wao
 
Mleta mada, hoha uliyoileta ni hoja dhaifu.

Suala la rufaa waliyokata akina Halima halina nguvu yoyote ya kusababisha wabunge hao kuendelea kuwa wabunge. Chama kimekwishatimiza wajibu wake wa kuwafukuza uanachama. Mbona mfungwa akikata rufaa bado anaendelea kukitumikia kifungo gerezani?

Lakini kama hiyo haitoshi, ni Mtanzania yupi mwenye akili timamu hajui kama wabunge hao walipatikana kwa njia haramu.

Chadema walikwishathibitisha kwamba taarifa ya kufukuzwa kwa wanachama hao ilipelekwa ofisi za Bunge kwa dispach.
Mnataka nini kifanyike.

Sophia Simba alipofutiwa uanachama mara moja alikoma kuwa mbunge,lkn kwa CDM mbali na chama kuwafukuza,lkn wao bado ni wabunge kama sio biashara kichaa.
 
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho...
Mademu wengi wa Mbowe ndio hao COVID, wanapata posho ya ubunge wanampunguzia gharama za kuwatunza, halafu hao ndio Chadema wenyewe, Mbowe anawafukuzaje?

Wana secret agreement na wamepigiwa mihuri ya chama kuwathibitisha, na Mbowe amesaini pamoja na Mnyika, wale halali wametenguliwa
 
Back
Top Bottom