Kigwangala usilete mgogoro Simba, lazima tuwaamini uongozi uliopo

Mo simba katudhulum timu yetu. Haturuhusiwi kusema chichote tena. Kweli simba anaigeuza kuwa kongo kwa demu wake.
 
Kwani huyo Poyoyo alipoteuliwa kuwa naibu waziri wa Afya alikuwa na experience gani? Au alitoa rushwa kwa mh rais? Je alipoteuliwa kuwa waziri wa maliasili alihonga mkewe kwa viongozi wa juu? HANA LOLOTE MSHAMBA TUU. Ameanza kuota meno. Ajiangalie atakuja juta. Baraza lijalo hatumpi nafasi. Haijui simba ya sasa huyo. Aache kuanzisha chokochoko "KUBWAJINGA"
 
@kibaravumba

Ivi mtu akihoji kuhusu makubaliano ambayo hayakutekelezeka kuhusu timu yake ni dhambi?

Dr.kigwangala yupo sahihi kabisa,maana inaenda mwaka wa 4 huu tangu Mo alipoingia makubaliano na simba juu ya uwekezaji wa bilioni 20.

Em fikiria ile logo yetu ya Simba ambayo ilikua na slogan ya timu imebadilishwa,kwenye jezi ya timu kuna brands kibao ambazo kimsingi legally hazitakiwiii kuwa pale..
 
Bwana Hamisi anataka kutuharibia furaha yetu maisha yatuchape na mpira nao utuchape kisa bwana Hamisi alikosa boxer
 
Ni kweli kabisa ila kama shabiki wa Simba kipi unataka kwa sasa, Mwamedi atoke?
 
Sawa ila mashabiki wa Simba tunataka ushindi tu.
@Cvez

Ushindi haujii tu boss Kama unavyozania,ushindi ni mipango,uwekezaji,kujitoa n.k au we unapenda daily tuchukue haya makombe ya ndani?

I hope Kama zile b20 zingewekwa,ile quarter final tuliyotolewa na TP mazembe tusingetolewa maana TP mazembe alituzidi quality players..

Na kupata quality players,pesa ndefu inatakiwa kuwekwa
 
Simba tunatumika kumuingizia kipato Mudi bila kujua, hajatuwekea senti zetu ila kila mali yetu kuna nembo za Mudi. Hahahaaaaa umaskini ni upofu wa kudumu.

Naona hili suala ni nyeti ila kwa vile kipofu huwa haoni anakokwenda ngoja tutulie maana shimo la mauti linakaribia
 
Mkuu heshima kwako, naomba unisaidie kujibu maswali haya :

1. Kwenye Makubaliano ya uwekezaji, hiyo hela ilikuwa itolewe yote kwa mkupuo au ni kwa instalments?

2. Toka MO apewe 49% ya share za Simba, hadi sasa ameshatumia gharama kiasi gani? je gharama hizo ni Sehemu ya ile 20B?

3. Toka MO apewe team, je kuna mabadiliko yoyote kwenye performance ya team?

Simba ilishatoka kwenye enzi za migogoro ya kina Mzee Kilomoni, huu ni muda wa kujadili mipango ya maendeleo na sio fitna zisizokuwa na tija yoyote
 
Toka uongozi wa Mo Dewji Simba imezidi kusonga na kuimarika. Leo hii ndiyo club kubwa East Afrika. Wapuuzi wachache wanaleta chokochoko sababu hawana. 51% zipo wazi nunua na wewe share uwekeze sio kupiga domo mitandaoni hujui hata Bwalya kapatikanaje
 
Kumbuka kuwa moja ya watu watakaomfanyia hiyo appraisal Mo ni mmoja wao na ndio Boss wa Timu. Je, kutakuwepo na transparency ya uhakika wakati wa zoezi hilo. Maana anawajibika kwa Boss mmoja mara 2. Lazima atabebwa tu kwa vile analinda maslahi ya Boss wake. So, bila ubishi Kuna conflict of interest hapo.
 
Mkuu hoja zako zimejengwa kwenye hisia na udhanifu, kwenye performance Apraisal tunaangalia objectives, apewe muda kama hana uwezo itajulikana tu kwa kuangalia trend ya overall performance ya team
 
Nataka zile b20 ziwekwe afu Mambo yaendeleee
We shabiki wa simba au mwanachama? Kama shabiki unaujasiri gani wa kudai kitu ambacho hakikuhusu? Na kama mwanachama we umechangia sh ngapi kwenye hayo makubaliano maana wanachama mna 51% zenu lakini hadi hamjatoa chochote.
Ko mnataka MO atoe hizo 20b ili zikiisha wakati 51% zenu hamjatoa MO apate hasara?
 
Kiuhalisia yeyote anaempinga Mo kuna issue zake binafsi na si kama ana mapenzi makubwa sana na Simba
 
Anahoji tweeter?Amekosa nauli ya kuwaona wahusika kutaka ufafanuzi?
Au ana agenda ya kuivuruga Simba kwa maslahi yake binafsi?
 


Bwana Hamisi anataka kusema Mwamedi si bilionea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…