Kigwangala usilete mgogoro Simba, lazima tuwaamini uongozi uliopo

Kigwangala usilete mgogoro Simba, lazima tuwaamini uongozi uliopo

Sometimes nadhani Hawa wakezaji wanna mambo yao tu na sio kukuza mpira kama tunavyodhani...

Hapa alipofika ni mbali Sana ...bwana mudi.. in short simba ishakuwa kakitu kake ka kupotezea muda na kumkeep busy.. Sasa akipewa hadidu nzito nzito anaona sio starehe tena Ni karaha .. kwa namna hii anakuwa na control ya hadidu..

[emoji16][emoji16][emoji16]Halafu mudi asivyokuwa muongo mzuri.. hata kabla hajaulizwa kashakana ..hajamchagua yeye..Ni Kikao kizuri ndio kimefanya yake[emoji16][emoji16]

Na taarifa hajatoa afisa habari katoa yeye.. [emoji16][emoji16][emoji16] mudi anatuona mandezi Sana.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Utakua popoma Kama huoni mchango was GSM na Mo kwenye mpira wa Tanzania, wewe unadhani ule umati wa Siku ya mwananchi umekuja kumwangalia kibwana makapu na boxer?
 
Issue sio uzoefu wake, issue ni conflicts of interest.
Hii ni pisi ya Mudi, ni mfanyakazi binafsi wa mudi leo anakua CEO kwenye taasisi ambayo Mudi ni muwekezaji mwenye hisa hamuoni kuwa atakua anafavor maslahi ya Mudi zaidi kuliko maslahi ya taasisi??
Yaani ni akili ya kawaida kabisa hii, sijui wanafeli wapi hawa viumbe.
 
Huyo Kingwangala si alikuwepo kwenye mkutano wa mabadiliko ya katiba na uwekezaji?
Alitoa maoni yake?
Personal vendetta zisimfanye sasa ajidai ni mtetezi wa maslahi ya Simba .Yeye ameisaidia nini Simba?
Au mkopo umeleta nongwa?
Atofautishe biashara na mambo yanayohusu Simba.
 
Dharaurini hoja za Kigwangala ila ipo siku na ninyi mtakuja kutembeza bakuli uwanjani.
Ziweke hapo hizo hoja. Unafuata mkumbo au nyumba ya jirani kwa mwarabu koko?
 
Utakua popoma Kama huoni mchango was GSM na Mo kwenye mpira wa Tanzania, wewe unadhani ule umati wa Siku ya mwananchi umekuja kumwangalia kibwana makapu na boxer?
It's football ..not war.. relax and have fun Chief.

Hata hivyo mie sijapinga mafanikio.. au wewe umeitoa wapi hii notion ya mimi kutokuuona mchango wao!?

Wewe mchango wa Senzo uliuona!? Was there a need to replace him ikiwa timu ilikuwa inafanya vizuri!? With absolute certainty, unaweza kusema CEO mpya ana sifa za ubora kuliko Senzo!?

Tumezoea shamrashamra kwenye habari kubwa Kama hizi ndani ya klabu.. hints, tambo (ukizingatia anakuwa CEO wa kwanza Mwanamama) why this is so gloomy!?

Huu mpira wa Yanga na Simba unakazi nyingine nyingi kuliko kuleta burudani Uwanjani tu.. na watu wakihoji sio hawapendi..hapana... ukianza kuwakandia huo sio ushabiki unakuwa ni uzwazwa.. utashabikiaje to the point huoni flaws tena!! Ndugu yangu!!

Sote tunaitakia Simba mema.. na tunapohoji lengo letu ni kuboresha. Tujadiliane tuondoane sintofahamu.. sio kuwekana lebo kisa mtu kahoji. It's not the Simba way.

Simba & Yanga day zitakuwa more fun siku tukiwa tunakipiga fainali za Champion League.. Tunaenda klabu Bingwa ya Dunia.. maana kufungana sisi haipaswi kuwa lengo pekee kuu.. tutoke nje ya hiyo bubble.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hoja ya kingwa ya msingi but ajatoa mbadala,

Alitakiwa aseme wakurugenzi wote wajiuzulu na more atoke then timu itoe Namba za wanainchi kuchangia
Nadhani hujazielewa hoja zake

Anachohoji yeye ni kua inakuaje mo hajalipa 20b ambazo ndo zinazomfanya awe na uhalali wa 49% ya hisa na tayari ashakua mkurugenzi na anafanya maamuzi inawezekanaje?
 
Kumbuka Kaduguda ndiyo anayeshikilia record ya kuongoza Simba iliyotwaa ubingwa bila kupoteza hata mechi moja.
Kaduguda amechaguliwa na nani? Kweni kuna mkutano mkuu uloitwa?
 
Nadhani hujazielewa hoja zake

Anachohoji yeye ni kua inakuaje mo hajalipa 20b ambazo ndo zinazomfanya awe na uhalali wa 49% ya hisa na tayari ashakua mkurugenzi na anafanya maamuzi inawezekanaje?

Mbona maamuz ya uwanja aja hoji?
Mbona usajiri na mishahara hajaoji?
 
Mbona Engineer wenu feki hamulalamiki?Yupo kwenye kamati ya mashindano kama kiongozi wa Utopolo na pia ni mwajiriwa wa GSM?Analinda maslahi ya nani?Umeona akisema Yanga imesajili au huwa anasema GSM tumesajili na Yanga watalipa mshahara??
Au uweledi na madai ya kijinga ya conflict of interest hayawahusu?
Mwenyekiti wenu aliajiriwa na nani?
Hivi mna viongozi na GSM kwenye mfumo upi?
Kweli mna hadhi ya kuhoji?
Jezi za msimu mpya zimefika au matatizo ya usafiri wa ndege kwa sababu ya Corona?
Mnathubutu kuuliza??
Eng. Feki kivipi? Una taarifa na vyeti vyake?
Katiba ya Yanga haikatazi mjumbe wa kamati kuwa mwajiriwa.
Kuwa serious mwenyekiti anaajiriwa? Mwenyekiti kwa katiba ya Yanga bado anachaguliwa.
Gsm ana tenda ya kuipatia Yanga jezi na pia ni mzamini.
Jezi zimechelewa ndio sasa unataka tufanyaje ? Tugome? Au tuandamane? sababu hata zikichelewa na kuwahi bado wajibu wa shabiki unabaki palepale ni kununua tu.
 
Nyani ni Nyani tu.Haoni kundule. Utopolo kweli una moral athourity ya kuzungumzia Simba wakati mmepakatwa na mwarabu koko wa GSM na msomali pori.
Wanasajili wao tena kwenye sitting room zao huku mkiwa na klabu bila nembo wala ushuzi.
Unafikiri Shija alijiuzulu kwanini?
Sasa hivi GSM wamesema wamesajili ila nyie Utopolo mlipe mishahara. Wakijua hamna uwezo huo ili mzidi kuwaachia klabu.Hiyo ni blackmail.Mmekazia shingo Simba huku nyumba ya mabua inauungua.
Thamani ya binadamu ni kujitambua.
 
Marina CEO wa Chelsea alikuwa PA wa Abromovich mbona hakuna conflict of interest. Hata CEO aliteuliwa na Kigwa kea pesa aliyonayo Mo akiamua apewe upendeleo atapewa tu
Akili kisoda.. sasa hapo kuna shida?? Maana hiyo chelsea inamilikiwa na Abramovic lkn simba inamilikiwa na MO hata amlete PA wake?
 
Inawezekana ana hoja lakini kwanini anamu attack zaidi Modewji? Kwanini katika kipindi hiki? Mi nadhani kwa nafasi yake kama Waziri alikuwa na nafasi ya kulipeleka hili suala katika mkondo sahihi, ambao hautawagawa mashabiki na wanachama hatimaye kusambaratisha uimara wa timu kwa migogoro isiyo na kichwa wala miguu!
Kama anatafuta umaarufu zaidi wa kisaisa wakati huu wa kampeni hakukuwa na ulazima wa kuitimia Club ya Simba.
Kama kanuni na taratibu za kumpata CEO wa Club hazikuzingatiwa naamnini bodi wanaweza kuwa na majibu mahsusi na sio kwenye mitandao ya kijamii,! Waziri unapojibiza na muwekezaji ambae lengo lake ni kuboresha soka katika Nchi yako ambalo linaleta ajira kwa vijana! Ikiwa ndio lengo kuu la serikali yenu umekusudia kukatisha tamaa wengine?
Ni sawa inawezekana kuna mapungufu ya huo uwekezaji je mahali sahihi pa kukosoa ni kwenye mitandao ya kijamii?
Naamini Hamisi kigwangalla anatukosea sana wanasimba wenzie..
Kigwangala na wengineo wote ni wakupuuza kwa sasa....kwani timu inamafanikio chini ya Mo....tukiona hakueleweki huko mbele tutajua tu haina haja ya kuelezwa na Kigwangala anatafuta Kiki za kisiasa kwa sasa na makasiriko mengine ya kukosa mkopo wa Pikipiki...wengine ni either wanafaidika timu ikikosa udhamini au wanahisi Mo anamake sana kutoka simba so ni kawivu flani hivi...ni wakupuuzwa wote hao until further notice.
 
Back
Top Bottom