Kigwangalla aambiwe amefika alipofika kwa mbeleko zaidi, aache kudharau vijana mafukara.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Huyu mwanasiasa huwa anajiweka hustler mpambanaji sana wakati kila mtu anajua amefika hapo alipo kwa mserereko na kubebwa, mzazi wake alikuwa mtu wa chama, kuupata ubunge mara ya kwanza yeye mwenyewe alishindwa kura za maoni akabebwa na baadaye jimbo likagawanywa ili aendelee kubaki mbunge.

Inashangaza sana anapojifanya ameyapatia maisha kwa upambanaji na juhudi zake binafsi huku akiwananga vijana waliopigika kila siku.
 
Huwa nikimuangalia namuona mchafu mchafu tu...!
 
Watu wanakimbilia serikalini kwakuwa huko kuna job security ni hilo tu.

Sio kila mtu anaweza kujiajiri, hivyo acha watu wafanye wanavyoona ni sahihi kwao.
 
Yale yale ya mwisiraeli na mbeleko za mmarekani mamburula wasizotaka kuziona.

Mnapomwambia huyo mwamba ya mbeleko, msimsahau na huyo mwana mpendwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…