Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
“Wananchi wa Nzega Vijijini walishatoa msimamo Mh. Rais alipotembelea pale kwamba hawana la kuomba zaidi ya kumshukuru Rais “
Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamis Kigwangalla amewataka Watanzania wote popote walipo kutumia hashtag ya ‘Nasimama na Mama’ wanapoweka picha zao au machapisho mengine mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni sehemu ya kuonesha kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais wa Tanzania-Samia-Suluhu Hassan.
Pia soma Hamis Kigwangalla: Ukiposti kitu chochote Mtandaoni weka na Hashtag ya 'Nasimama na Mama'
‘Nasimama na Mama’ na hii ni kwasababu Rais Samia anafanya kazi nzuri” “ Rais Samia amechukua Nchi kwenye kipindi kigumu na kaisimamisha Nchi vizuri kwahiyo lazima tufurahi, unaenjoy na amani na utulivu, Wabunge wote, Wana CCM wote, Watanzania wote popote ulipo hashtag yetu iwe ‘Nasimama na Mama”
#Wana-Tabora nyumba za udongo ni saizi yao!