Kigwangalla: Baada ya mipango mizuri iliyotengenezwa kumuangusha Gekul na Chongolo, nani anafuata? Kuna wengine wanakuja!

Kupitia X (zamani Twitter), Anaandika Hamisi Kigwangalla, Mbunge wa Nzega Vijijini

Hivi baada ya a very carefully planned and executed mission ya kumuangusha Mhe. Gekul na Ndg. Chongolo, unaweza ku-guess anayefuata ni nani?

Competitive intelligence imejikita kwenye kujua kitakachotokea kabla hakijatokea (fore knowledge).

Tunaishi kwenye dunia ya ushindani mkali, dunia ya mashambulizi makali ya kiteknolojia - je, tuko aware? Ama tunapigwa halafu tunajifunza baada ya kupigwa? Tunaanza kujadili matokeo?

Niliandika hapa juzi kuwa, kwenye uwanda wa siasa kuna mambo mengi sana yanaweza kutokea, na kwamba siyo lazima yawe halisi ama kweli; yanaweza kutokea kwa kupangwa (kama yale yaliyonikuta mimi, ama haya ya Gekul na Chongolo) na ama hata kwa ajali tu!

Kuna pattern naiona. Sijui kama na wewe unaiona! Kuna victims wengine wanakuja. Tafakari! Chukua hatua.

Gekul anaonekana shetani, katili, jambazi asiye na ubinadamu hata kidogo ndani yake, sababu kiukweli kitendo cha namna hiyo hakifai wala hakifikiriki!

Vipi ukijua ukweli kwamba kijana hakuwekewa chupa, utasemaje? Pengine Gekul acted too naively, Pengine amejiweka kwenye mazingira ya kushughulikiwa na hatimaye kupata hukumu ya jamii. Pengine.

Kwa mwanasiasa na kiongozi mkubwa, hukumu ya jamii inatosha kukupotezea sifa ya kuwa kioo cha jamii, haijalishi tuhuma ziwe halisi ama ama uzushi. Moja ya somo kubwa la uongozi tunalopata.

Somo lingine ni kuwa; mitandao ya kijamii ina nguvu sana. Ikitumiwa vibaya na watu wenye nia mbaya inaweza ikaangusha dola, achilia mbali kuangusha mtu mmoja mmoja.

Somo lingine: wanaCCM tuamke sasa, kazi imeanza. Vita vya kisiasa vinapiganwa huku sasa hivi. Kumekucha!

View attachment 2829996
View attachment 2829997
Asilaumu technology huku ujinga wanafanya na ujuha mkubwa hivyo wananataka wasiumbuliwe
 
kuhusu rushwa, uadilifu na udanganyifu wa viongozi, hakuna kiongozi wa CCM aliye msafi, narudia tena, aliye msafi!
Tena walio wachafu wana matumbo makubwa waliyoyapata baada ya kujitenga na usafi.

1701407908190.jpg
 
Mbunge mzima na waziri mstaafu na Dr wa binadamu unabandika maandishi ku confirm kuwa Gekul hajafanya kosa lolote ila kawa framed.

  1. Hapa kwanza unamdharau Rais Samia kwa ku act kijinga kwa kumtolea unaibu waziri wake wakati ni innocent.
  2. Unaiaminisha jamii kuwa TISS ni sio tu haifanyi kazi ila ni kama haipo tu kabisa.
  3. Unaiaminisha jamii kuwa watanzania ni mazezeta sana

Nikuulize bwana Daktari wa nzega, why Gekul? What is so special na Gekul atengenezewe hili zengwe akose ubunge wake?
 
Anataka kusema ni Wapinzani wa CCM au ni CCM kwa CCM wanaleteana mtiti? Kama ni Wapinzani itakuwa ni ushindi mkubwa sana kuweza kuimomonyoa CCM walau kidogo tu hapo.

Anyway, kwa Gekul hiyo ni ajali yake ya kisiasa kajiangusha mwenyewe haina haja kuumiza kichwa kutafuta mchawi.

Ya Chongolo picha liko wazi yule Kijana aliyejipa madaraka makubwa na sifa nyingi anaweza kuwa chanzo, hapo haitaji akili nyingi kujua hayo.

Ajali za kisiasa za kutengeneza hujulikana mapema tu. The way unapopanda juu kisiasa utelezi wa kuanguka nao huongezeka unaweza ukateleza mwenyewe ukaanguka bila kuangushwa na mahasimu/wapinzani
 
Nikuulize bwana Daktari wa nzega, why Gekul? What is so special na Gekul atengenezewe hili zengwe akose ubunge wake?
Ushaambiwa ni Vita ya kisiasa Mzee wahuni sio watu, usicheze na wahuni watakutoa kwenye reli
 
Kupitia X (zamani Twitter), Anaandika Hamisi Kigwangalla, Mbunge wa Nzega Vijijini

Hivi baada ya a very carefully planned and executed mission ya kumuangusha Mhe. Gekul na Ndg. Chongolo, unaweza ku-guess anayefuata ni nani?

Competitive intelligence imejikita kwenye kujua kitakachotokea kabla hakijatokea (fore knowledge).

Tunaishi kwenye dunia ya ushindani mkali, dunia ya mashambulizi makali ya kiteknolojia - je, tuko aware? Ama tunapigwa halafu tunajifunza baada ya kupigwa? Tunaanza kujadili matokeo?

Niliandika hapa juzi kuwa, kwenye uwanda wa siasa kuna mambo mengi sana yanaweza kutokea, na kwamba siyo lazima yawe halisi ama kweli; yanaweza kutokea kwa kupangwa (kama yale yaliyonikuta mimi, ama haya ya Gekul na Chongolo) na ama hata kwa ajali tu!

Kuna pattern naiona. Sijui kama na wewe unaiona! Kuna victims wengine wanakuja. Tafakari! Chukua hatua.

Gekul anaonekana shetani, katili, jambazi asiye na ubinadamu hata kidogo ndani yake, sababu kiukweli kitendo cha namna hiyo hakifai wala hakifikiriki!

Vipi ukijua ukweli kwamba kijana hakuwekewa chupa, utasemaje? Pengine Gekul acted too naively, Pengine amejiweka kwenye mazingira ya kushughulikiwa na hatimaye kupata hukumu ya jamii. Pengine.

Kwa mwanasiasa na kiongozi mkubwa, hukumu ya jamii inatosha kukupotezea sifa ya kuwa kioo cha jamii, haijalishi tuhuma ziwe halisi ama ama uzushi. Moja ya somo kubwa la uongozi tunalopata.

Somo lingine ni kuwa; mitandao ya kijamii ina nguvu sana. Ikitumiwa vibaya na watu wenye nia mbaya inaweza ikaangusha dola, achilia mbali kuangusha mtu mmoja mmoja.

Somo lingine: wanaCCM tuamke sasa, kazi imeanza. Vita vya kisiasa vinapiganwa huku sasa hivi. Kumekucha!

View attachment 2829996
View attachment 2829997
Huyu Kigwangala sijuhi ana nia gani kwa wananchi wa kawaida. Anatetea hata kile alichokifanya Gekul. Kwamba mwanchi akilalamika ni uongo hisipokuwa kila asemalo kiongozi ndio ukweli. Sishangai, kuna viongozi aina yake walidai Lissu alijipiga risasi ili apate political milage na baadhi ya wajinga wakamini hivyo.
 
Back
Top Bottom