Kigwangalla: Baada ya mipango mizuri iliyotengenezwa kumuangusha Gekul na Chongolo, nani anafuata? Kuna wengine wanakuja!

Asilaumu technology huku ujinga wanafanya na ujuha mkubwa hivyo wananataka wasiumbuliwe
 
Bora angefunga mdomo.. huyo Kijana uchi mbele yake alifanyiwa njama amvue nguo!!!!!
 
Mbunge mzima na waziri mstaafu na Dr wa binadamu unabandika maandishi ku confirm kuwa Gekul hajafanya kosa lolote ila kawa framed.

  1. Hapa kwanza unamdharau Rais Samia kwa ku act kijinga kwa kumtolea unaibu waziri wake wakati ni innocent.
  2. Unaiaminisha jamii kuwa TISS ni sio tu haifanyi kazi ila ni kama haipo tu kabisa.
  3. Unaiaminisha jamii kuwa watanzania ni mazezeta sana

Nikuulize bwana Daktari wa nzega, why Gekul? What is so special na Gekul atengenezewe hili zengwe akose ubunge wake?
 
Anataka kusema ni Wapinzani wa CCM au ni CCM kwa CCM wanaleteana mtiti? Kama ni Wapinzani itakuwa ni ushindi mkubwa sana kuweza kuimomonyoa CCM walau kidogo tu hapo.

Anyway, kwa Gekul hiyo ni ajali yake ya kisiasa kajiangusha mwenyewe haina haja kuumiza kichwa kutafuta mchawi.

Ya Chongolo picha liko wazi yule Kijana aliyejipa madaraka makubwa na sifa nyingi anaweza kuwa chanzo, hapo haitaji akili nyingi kujua hayo.

Ajali za kisiasa za kutengeneza hujulikana mapema tu. The way unapopanda juu kisiasa utelezi wa kuanguka nao huongezeka unaweza ukateleza mwenyewe ukaanguka bila kuangushwa na mahasimu/wapinzani
 
Nikuulize bwana Daktari wa nzega, why Gekul? What is so special na Gekul atengenezewe hili zengwe akose ubunge wake?
Ushaambiwa ni Vita ya kisiasa Mzee wahuni sio watu, usicheze na wahuni watakutoa kwenye reli
 
Huyu Kigwangala sijuhi ana nia gani kwa wananchi wa kawaida. Anatetea hata kile alichokifanya Gekul. Kwamba mwanchi akilalamika ni uongo hisipokuwa kila asemalo kiongozi ndio ukweli. Sishangai, kuna viongozi aina yake walidai Lissu alijipiga risasi ili apate political milage na baadhi ya wajinga wakamini hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…