Kigwangalla: Chama kimerudi kwa wenyewe

Kigwangalla: Chama kimerudi kwa wenyewe

hamisi_kigwangalla

SEKRETARIETI ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapindunzi (CCM), ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi @daniel_godfrey_chongolo jana imehitimisha ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 na kuimarisha Chama mashinani katika mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Katavi na Tabora. Pichani wajumbe wa Sekretarieti hiyo wakizungumza katika kikao cha majumuisho mkoani Tabora. Kwa hakika Chama kimerudi kwa wenyewe. CC: Komredi @shaka_hamdu_shaka. #HK #KaziIendelee #SiasaNiVitendo

View attachment 2021524
View attachment 2021525
View attachment 2021526

My take: Kwani Chama kilitekwa?
Ni ajabu Sana,
Watu wasahaulifu,
Chama kilioza mikononi mwa hao anaowaita wenye chama, kikadharauliwa na jamii yote ya watanzania
Wanachama hawakuweza Tena kuvaa kofia za CCM mitaani
Yule mwamba amekichukua chama kikaheshimika, kura zote kwa CCM, ingawa wasiopenda kukiri wanatangaza kura kuibiwa! Tushawazoea!
Lakini anyway chama kweli kimerudi kwa wenyewe!
Subiri tuone 2025 watu wakinyang'anywa majimbo yao
 
hahahahaha mmezoea laini laini.... mmepigwa mchakamchaka chinja miaka 6 tu hapa hoi.....
Ule haukuwa mchaka mchaka, ulikuwa uhuni!! Mchaka mchaka ilibidi upigwe kwa watu wote, siyo kuchagua baadhi ya watu/makundi ya kuwaonea
 
Ule haukuwa mchaka mchaka, ulikuwa uhuni!! Mchaka mchaka ilibidi upigwe kwa watu wote, siyo kuchagua baadhi ya watu/makundi ya kuwaonea

unapoamua kuweka nchi sawa lazima kuwe na kundi aminifu kwako....hili kundi hakuna namna litaishi vizuri tu...la msingi ni kazi ikamilike na malengo yatimie..
 
Ni ajabu Sana,
Watu wasahaulifu,
Chama kilioza mikononi mwa hao anaowaita wenye chama, kikadharauliwa na jamii yote ya watanzania
Wanachama hawakuweza Tena kuvaa kofia za CCM mitaani
Yule mwamba amekichukua chama kikaheshimika, kura zote kwa CCM, ingawa wasiopenda kukiri wanatangaza kura kuibiwa! Tushawazoea!
Lakini anyway chama kweli kimerudi kwa wenyewe!
Subiri tuone 2025 watu wakinyang'anywa majimbo yao
Hata 2020 watu walinyang'anywa majimbo yao, yakaporwa kifirauni!! Inaonesha ulifaidika na yale yaliyokuwa yanafanywa kwenye chaguzi from 2016-2020
 
unapoamua kuweka nchi sawa lazima kuwe na kundi aminifu kwako....hili kundi hakuna namna litaishi vizuri tu...la msingi ni kazi ikamilike na malengo yatimie..
Kundi lenyewe ndiyo liwe la majambazi na matapeli? No way
 
Hama wewe mtabanana humohumo..who knows after samia atakuja nani?
Ameshajulikana tayari, ni mtu aliyelelewa ndani ya chama, mwenye kujua misingi ya uongozi! Kosa la 2015 halitorudiwa tena
 
Originally CCM kilianzishwa na wazalendo watupu(hao ndio wenye chama)

Baadae kikavamiwa na wezi mbwa, kina Nyerere wakasema CCM si mama yangu, wakatishia kukaa pembeni

Tangu hapo CCM hakijawahi kurudi kwa wenyewe(wazalendo) hadi Magufuli alipojaribu kufanya hivyo na akashindwa

Kigwangala anaposema CCM kimerudi kwa wenyewe wakati tukiangalia sura za mbele za viongozi wake ni wezi watupu(ukimtoa mwenyekiti)

Anakua ana maana gani?

Au anataka kutuaminisha CCM ni chama cha wezi?
 
Ameshajulikana tayari, ni mtu aliyelelewa ndani ya chama, mwenye kujua misingi ya uongozi! Kosa la 2015 halitorudiwa tena

Hakuna kitu kama hicho siasani 24hrs ni mda mrefu sana sembuse more than 5years to come...wapi edo, wapi membe, wapi malicela? Wote walijua njia ni nyeupe kwenda enzini ila wakaishia kula nyundo..
 
Hakuna kitu kama hicho siasani 24hrs ni mda mrefu sana sembuse more than 5years to come...wapi edo, wapi membe, wapi malicela? Wote walijua njia ni nyeupe kwenda enzini ila wakaishia kula nyundo..
Hao uliowataja wote wana sifa nilizozitaja hapo juu, and yeyote angeweza kuwa....But mwisho wa siku ni mmoja tu anahitajika, Come 2030 huyo atakayeteuliwa lazima awe na hizo sifa, hataokotwa tena "wakuja" from nowhere
 
Haya kuishi kwa matumaini ni jambo jema. Ila 2030 utafurahi mwenyewe
 
Back
Top Bottom