Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,503
Wabunge wa CCM ndiyo kina nani na Wabunge wa CHADEMA ndiyo wapi hao kwenye maswala yanayowagusa wananchi?.Mh.Hamisi Kigwangwala amesema si sahihi kuweko ukomo kwa mbunge kugombea jimbo fulani kwani wenye maamuzi ni wananchi.
Katika kutetea hoja yake hiyo,mh.Kigwangala amesema hata mataifa ambayo ni vinara wa demokrasia duniani kama Marekani na Uingereza,mbunge anaweza kudumu(kuchaguliwa) hata kwa muda wa miaka 30.
Wakati huo huo, mh.Mnyika ameunga mkono kuwepo kwa ukomo wa vipindi vitatu.
Kuhusu posho,Kigwangala amekataa kabisa kuzungumzia posho kwa maelezo sio hoja ya msingi.Kwa upande wa Mnyika,yeye amepinga posho hiyo ya 300,000 na kusema wasihukumiwe wabunge wote kwa hoja hiyo.
CHANZO:Star tv
MY TAKE:
kuna tofauti kubwa sana ya wabunge wa CCM na CHADEMA.
Tafakari na utajionea mwenyewe ni nani mbunge kimeo hapo.
Kwenye swala la posho za Wabunge wa JMT ambapo wanajikusanyia kama milioni 12 kwa kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano, wote wako pamoja ila kwenye swala hili la posho ya siku 90 ambayo kwa Wabunge wa JMT inakuwa ni kama mengineyo (top up) kwa vile bado wanaendelea kupokea mishahara yao ndiyo maana unawasikia wakitaka kujiosha kisiasa.
Wabunge wote ni wasanii ila usanii wao unazidiana kulingana na mazingira.
Hii hoja ya kusema kusiwepo ukomo wa wabunge ni muflisi hasa ikichukuliwa kuwa wanaweza kuwepo kwa vipindi 3 vya uhai wa bunge. Kuna wengine kwa sasa wanazeekea kwenye bunge na wakati waliingia wakiwa ni vijana. Ndiyo maana hata siasa zetu hazibadiliki kwa sababu kila mwaka mawazo ni yale yale na watoa mawazo ni wale wale.