Kigwangwalla: Si sahihi kuweka kikomo cha ubunge!

Mh.Hamisi Kigwangwala amesema si sahihi kuweko ukomo kwa mbunge kugombea jimbo fulani kwani wenye maamuzi ni wananchi.

Katika kutetea hoja yake hiyo,mh.Kigwangala amesema hata mataifa ambayo ni vinara wa demokrasia duniani kama Marekani na Uingereza,mbunge anaweza kudumu(kuchaguliwa) hata kwa muda wa miaka 30.

Wakati huo huo, mh.Mnyika ameunga mkono kuwepo kwa ukomo wa vipindi vitatu.

Kuhusu posho,Kigwangala amekataa kabisa kuzungumzia posho kwa maelezo sio hoja ya msingi.Kwa upande wa Mnyika,yeye amepinga posho hiyo ya 300,000 na kusema wasihukumiwe wabunge wote kwa hoja hiyo.

CHANZO:Star tv

MY TAKE:
kuna tofauti kubwa sana ya wabunge wa CCM na CHADEMA.

Tafakari na utajionea mwenyewe ni nani mbunge kimeo hapo
.
Wabunge wa CCM ndiyo kina nani na Wabunge wa CHADEMA ndiyo wapi hao kwenye maswala yanayowagusa wananchi?.

Kwenye swala la posho za Wabunge wa JMT ambapo wanajikusanyia kama milioni 12 kwa kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano, wote wako pamoja ila kwenye swala hili la posho ya siku 90 ambayo kwa Wabunge wa JMT inakuwa ni kama mengineyo (top up) kwa vile bado wanaendelea kupokea mishahara yao ndiyo maana unawasikia wakitaka kujiosha kisiasa.

Wabunge wote ni wasanii ila usanii wao unazidiana kulingana na mazingira.

Hii hoja ya kusema kusiwepo ukomo wa wabunge ni muflisi hasa ikichukuliwa kuwa wanaweza kuwepo kwa vipindi 3 vya uhai wa bunge. Kuna wengine kwa sasa wanazeekea kwenye bunge na wakati waliingia wakiwa ni vijana. Ndiyo maana hata siasa zetu hazibadiliki kwa sababu kila mwaka mawazo ni yale yale na watoa mawazo ni wale wale.
 
mkuu hapa nadhani hawaelewi hoja ya Tume ya katika.RAsimu inazungumzia wabunge wa bunge la Muungano ambao wanatokana na Mikoa na sio majimbo ndo hawatatakiwa kugombea zaidi ya mara 2.Ila haijazungumzia wabunge watokanao na majimbo ya uchaguzi ambayo yatakuwa chini ya katiba ya Tanganyika.

Mkuu hivi unafikiri huyo mh. Kigwa kasoma hata hiyo rasimu!? Kwenye bunge la katiba wengi wanaingia wakiwa hawajaisoma rasimu ya katiba na kama wameisoma eidha watakuwa hawajaimaliza au hawajaielewa na ndo maana mch. Mtikila kawaita wahuni, tena ni zaidi ya wahuni na wamekosa hata mandate ya kuwa wabunge wa bunge la katiba
 
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, asubuhi nimemsikia Lukuvi anavyoongelea ishu ya ongezeko la posho, alichoongea ni kichefuchefu tupu.

Kigangwala kapigwa swali la posho anapanic.......ilimshinda nini kujibu tu kwa kifupi kama anaunga au haungi mkono.....tafsiri yake ni rahisi...anatamani matokeo ya kamati yawe chanya.

Mnyika naye sijamuelewa......sijaona uwazi wake wa kulaani huo ujinga wa kuomba nyongeza, zaidi analalama kuwa wanainchi wanapotezwa malengo .

Nionavyo haya majamaa yote ni yale yale tu..........MALAFI......
 
Mbona Urais una kikomo? Madaraka sumu. Sikutarajia mtu kama kIgwangalla kutamka maneno kama hayo. Huenda anasingiziwa.
 
linapokuja suala la pesa hakuna chadema wala ccm.pesa ina nguvu katika kubadili maamuzi ya mtu.wasitudanganye lao moja
 
Hoja ya kwamba tusiweke ukomo wa ubunge kwa sababu uamuzi ni wa wananchi haina nguvu kwa sababu hata urais ni uamuzi wa wananchi lakini ukomo upo. Pia kujaribu kuhalalisha ubunge wa maisha kisa eti Marekani wako hivyo ni makosa kwa kuwa changamoto zetu na zao ni tofauti. Si vema kuiga kila kitu kisa kinafanywa na wakubwa, mwisho tutahalalisha hata bangi na ushoga kwa huu mtindo wa kufyonza kila jambo linalofanywa na nchi zilizoendelea. Naunga mkono hoja ya ukomo!

Ndg. Alex,

Ninapotoa hoja nina misingi ifuatayo. Kwanza: haki ya msingi ya kikatiba ya kila mtu kuchagua ama kuchaguliwa kuwa kiongozi. Hili halibishaniwi na wapenda haki wote. Pili, baada ya miaka mitano Ubunge wa Mbunge unakoma automatically, na hivyo anarudi kuwa sawa na wananchi wengine wanaotamani kuwa wabunge, wanagombea wote katika mazingira sawa. Ingekuwa kuna zuio la wengine kugombea ingekuwa udikteta. Wananchi kama hawamtaki Mbunge wana haki ya kumbadilisha, lakini kama wanampenda unaanzia wapi kuwanyima haki ya kumchagua tena. Msisahau kuwa Mbunge ni mali ya wananchi anaowawakilisha na wana uamuzi naye baada ya hiyo miaka mitano, sasa kwa nini tulazimishie awekewe ukomo? Nini hoja zenu kwenye hili? Ama ni wivu tu na chuki zilizojengeka bila sababu za msingi dhidi ya wabunge?

Tungekuwa makini kidogo tu zaidi ya hapa tulipo sasa hivi tungejifikiria kubadili mfumo wa watendaji wakuu wa serikali, maana hawa ndiyo wanaofanya kazi za kila siku zinazowagusa wananchi, ndiyo wenye mafungu na ndiyo wataalamu - tungeweka fursa ya ushindani kwa hawa kila baada ya miaka mitano ya mkataba ili kuruhusu ushindani na kuingiza mawazo mapya kwa njia ya usaili. Hawa wana dhamana kubwa sana lakini hakuna anayewatazama, mnahangaika na wabunge (wanaopiga kelele bure tu bila meno ya kuuma!)

Utofauti wa Urais na Ubunge kwenye hili uko wazi sana; tazama majukumu makubwa matatu ya Rais: mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu...haya ni madaraka na mamlaka makubwa sana kuwekwa kwa mtu mmoja, akiwa hatoshi ama mbaya na akaamua kung'ang'ania kwenye madaraka mtakoma naye! Na pia kwa madaraka aliyonayo...na kwa kuzingatia mfumo wa Presidential system ambao tunaufuata sisi, Rais wetu ni Rais Mtendaji (Executive President), hivyo kumuwekea ukomo ni jambo la msingi - japokuwa anaowateua na kupa madaraka makubwa sana hawana ukomo! Huyu Rais na Mbunge (asiye mtendaji) ni tofauti sana...Mbunge ni mpiga kelele tu na mpaka akasikilizwe basi kazi ipo! Watendaji wengine siku hizi hata wameishawadharau mawaziri na wabunge kwa kuwa hawana madaraka yoyote yale ya maana...wanamuogopa Rais tu!

Nadhani nimewajibu na wenzako wote wenye hoja kama zako. Ni kwa msingi huu mimi nitatetea tunapoifanyia kazi Rasimu ya Warioba, tubadilishe hiki kifungu haraka!

Wakatabahu,
HK.

NB: Mimi binafsi naweza kugombea Ubunge mara moja tu tena ama kutogombea kabisa...bado natafakari. Kwa hiyo ninachokisema hapa hakina uhusiano wowote ule na Ubunge wangu ama hali yangu ya kisiasa ya sasa.
 
Wabunge wa CCM ndiyo kina nani na Wabunge wa CHADEMA ndiyo wapi hao kwenye maswala yanayowagusa wananchi?.

Kwenye swala la posho za Wabunge wa JMT ambapo wanajikusanyia kama milioni 12 kwa kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano, wote wako pamoja ila kwenye swala hili la posho ya siku 90 ambayo kwa Wabunge wa JMT inakuwa ni kama mengineyo (top up) kwa vile bado wanaendelea kupokea mishahara yao ndiyo maana unawasikia wakitaka kujiosha kisiasa.

Wabunge wote ni wasanii ila usanii wao unazidiana kulingana na mazingira.

Hii hoja ya kusema kusiwepo ukomo wa wabunge ni muflisi hasa ikichukuliwa kuwa wanaweza kuwepo kwa vipindi 3 vya uhai wa bunge. Kuna wengine kwa sasa wanazeekea kwenye bunge na wakati waliingia wakiwa ni vijana. Ndiyo maana hata siasa zetu hazibadiliki kwa sababu kila mwaka mawazo ni yale yale na watoa mawazo ni wale wale.

Taasisi imara duniani hazijawahi kusifika kwa turn-over rate ya watu wake makini bali kwa institutional memory...naamini Bunge ni taasisi nyeti na inahitaji watu wazoefu ili kusaidia kutoa maamuzi, lakini pia kwa kuwa kuna wimbi kubwa la mabadiliko linalotokana na vijana wa kizazi chetu na wadogo zetu, haitotokea wazee tena wakajikuta wamebaki wengi bungeni kushinda vijana...kwa hiyo binafsi sioni haja ya kuweka ukomo.

Wakatabahu,
HK.
 
Sasa kama.mnapinga enyi Chadema si muitishe press tuwasikie sio kila mtu kutoa tamko alikojifichia!!!!!!!

Suala la bei ya umeme huyo Mnyika wako bado anakusanya signatures???!!!!!!

Kwa sasa wote kundi moja tu tofauti rangi!!!!!!!
Na watu kama wewe ndio maadaui wa ukombozi sababu kila wananchi wanapokaribia kuungana mnaleta utenganishi wa makundi ya kisiasa hii ni tabia ya kisyenzi kabisa na wewe ni mmoja kati ya wasaliti wa ndani!!!!!!!

Unafaa kabisa kuchinjwa wewe!!!!

jaribu kuwa na busara.
 
Mh.Hamisi Kigwangwala amesema si sahihi kuweko ukomo kwa mbunge kugombea jimbo fulani kwani wenye maamuzi ni wananchi.

Katika kutetea hoja yake hiyo,mh.Kigwangala amesema hata mataifa ambayo ni vinara wa demokrasia duniani kama Marekani na Uingereza,mbunge anaweza kudumu(kuchaguliwa) hata kwa muda wa miaka 30.

Wakati huo huo, mh.Mnyika ameunga mkono kuwepo kwa ukomo wa vipindi vitatu.

Kuhusu posho,Kigwangala amekataa kabisa kuzungumzia posho kwa maelezo sio hoja ya msingi.Kwa upande wa Mnyika,yeye amepinga posho hiyo ya 300,000 na kusema wasihukumiwe wabunge wote kwa hoja hiyo.

CHANZO:Star tv

MY TAKE:

kuna tofauti kubwa sana ya wabunge wa CCM na CHADEMA.

Tafakari na utajionea mwenyewe ni nani mbunge kimeo hapo.
Huu ni unafiki wa hali ya juu hivi Mnyika anaunga mkono ukomo wa vipindi vitatu vya ubunge vipi kuhusu ukomo wa mwenyekiti wa chama chake ambayo katiba yao imeruhusu kuzeekea madarakani.
dhana hiyo hiyo iliyotumika kuweka ukomo wa wabunge itumike kuweka ukomo wa mwenyekiti wa chama chao.
Kweli bora mchawi kuliko Mnafiki
 
Taasisi imara duniani hazijawahi kusifika kwa turn-over rate ya watu wake makini bali kwa institutional memory...naamini Bunge ni taasisi nyeti na inahitaji watu wazoefu ili kusaidia kutoa maamuzi, lakini pia kwa kuwa kuna wimbi kubwa la mabadiliko linalotokana na vijana wa kizazi chetu na wadogo zetu, haitotokea wazee tena wakajikuta wamebaki wengi bungeni kushinda vijana...kwa hiyo binafsi sioni haja ya kuweka ukomo.

Wakatabahu,
HK.

kwani wakiweka ukomo kuna tatizo gani?
 
Ndg. Alex,

Ninapotoa hoja nina misingi ifuatayo. Kwanza: haki ya msingi ya kikatiba ya kila mtu kuchagua ama kuchaguliwa kuwa kiongozi. Hili halibishaniwi na wapenda haki wote. Pili, baada ya miaka mitano Ubunge wa Mbunge unakoma automatically, na hivyo anarudi kuwa sawa na wananchi wengine wanaotamani kuwa wabunge, wanagombea wote katika mazingira sawa. Ingekuwa kuna zuio la wengine kugombea ingekuwa udikteta. Wananchi kama hawamtaki Mbunge wana haki ya kumbadilisha, lakini kama wanampenda unaanzia wapi kuwanyima haki ya kumchagua tena. Msisahau kuwa Mbunge ni mali ya wananchi anaowawakilisha na wana uamuzi naye baada ya hiyo miaka mitano, sasa kwa nini tulazimishie awekewe ukomo? Nini hoja zenu kwenye hili? Ama ni wivu tu na chuki zilizojengeka bila sababu za msingi dhidi ya wabunge?

Tungekuwa makini kidogo tu zaidi ya hapa tulipo sasa hivi tungejifikiria kubadili mfumo wa watendaji wakuu wa serikali, maana hawa ndiyo wanaofanya kazi za kila siku zinazowagusa wananchi, ndiyo wenye mafungu na ndiyo wataalamu - tungeweka fursa ya ushindani kwa hawa kila baada ya miaka mitano ya mkataba ili kuruhusu ushindani na kuingiza mawazo mapya kwa njia ya usaili. Hawa wana dhamana kubwa sana lakini hakuna anayewatazama, mnahangaika na wabunge (wanaopiga kelele bure tu bila meno ya kuuma!)

Utofauti wa Urais na Ubunge kwenye hili uko wazi sana; tazama majukumu makubwa matatu ya Rais: mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu...haya ni madaraka na mamlaka makubwa sana kuwekwa kwa mtu mmoja, akiwa hatoshi ama mbaya na akaamua kung'ang'ania kwenye madaraka mtakoma naye! Na pia kwa madaraka aliyonayo...na kwa kuzingatia mfumo wa Presidential system ambao tunaufuata sisi, Rais wetu ni Rais Mtendaji (Executive President), hivyo kumuwekea ukomo ni jambo la msingi - japokuwa anaowateua na kupa madaraka makubwa sana hawana ukomo! Huyu Rais na Mbunge (asiye mtendaji) ni tofauti sana...Mbunge ni mpiga kelele tu na mpaka akasikilizwe basi kazi ipo! Watendaji wengine siku hizi hata wameishawadharau mawaziri na wabunge kwa kuwa hawana madaraka yoyote yale ya maana...wanamuogopa Rais tu!

Nadhani nimewajibu na wenzako wote wenye hoja kama zako. Ni kwa msingi huu mimi nitatetea tunapoifanyia kazi Rasimu ya Warioba, tubadilishe hiki kifungu haraka!

Wakatabahu,
HK.

NB: Mimi binafsi naweza kugombea Ubunge mara moja tu tena ama kutogombea kabisa...bado natafakari. Kwa hiyo ninachokisema hapa hakina uhusiano wowote ule na Ubunge wangu ama hali yangu ya kisiasa ya sasa.

Hebu subiri kwanza bwana mkubwa!!!!!!
1. Kwamba ukimaliza miaka mitano ya ubunge unakuwa sawa na mwananchi wa kawaida??!!!Mnagombea katika mazingira sawa yepi???!!! Wewe na huyo hasimu wako hapo muwekwe sawa na mwalimu mkuu anayetaka kugombea eti unaita mazingira sawa haya ya bastola mkononi au yapi???!!!! Hivi wewe si ndio unasemaga mimi na wananchi/wapiga kura wangu so and so then unaweka hoja leo wewe ndio umekuwa mali ya wananchi????!!!!! Kwamba wao ndio walipitisha mikopo yenu wapi wananchi wanasign kama wadhamini???!!!Please hebu usimshike
kipofu mkono!!!! Miaka kumi tu inatosha kama kweli unalengo kutumikia wananchi kwa miaka kumi inakutosha kuanzisha tool ya kutumikia wananchi,just register an organization tuunge nguvu tutetee afya za wanyonge kwa ku improve community based initiatives huko si ndio ulikobobea twende field mkuu!!!!!!

2. Hao unaowaita watendaji wa maisha ya kila siku tunawaachia nyie muhangaike nao sasa kama mnaona wana shida nyie si ndio wawakilishi sasa nawe unalalamika???! Crying father???? Hela zetu za majimbo si mnapewa nyie sasa unataka tukawakalie kooni kina nani??!!!! Hao nyie hangaikeni nao na mkishindwana si mmepewa nguvu ya kuvurumusha cabinet itumieni. Sisi tunawabana nyie mkisikia a pinch mtawasukuma wahusika. Unasema hamna meno na ni wapiga kelele tu sasa muda mrefu wa kupiga kelele wa nini kwa mtu mmoja?????!!!! Eti wao ndio wataalamu si ndio hii hoja inahitaji wabunge muwe na degree japo moja ili msisumbuliwe na.hao unaowaita wataalamu, sasa na hili chonde chonde uliongeze kule kwenye uzi wa maoni kuwa hapo waingie graduates ili mijadala iwe ya level hiyo unayoita ya kisomi!!!!

Thanx kwa uwepo wako tuitie na wengine huko wenye IDs huku labda nao wana yao!!!!
 
Ndg. Alex,

Ninapotoa hoja nina misingi ifuatayo. Kwanza: haki ya msingi ya kikatiba ya kila mtu kuchagua ama kuchaguliwa kuwa kiongozi. Hili halibishaniwi na wapenda haki wote. Pili, baada ya miaka mitano Ubunge wa Mbunge unakoma automatically, na hivyo anarudi kuwa sawa na wananchi wengine wanaotamani kuwa wabunge, wanagombea wote katika mazingira sawa. Ingekuwa kuna zuio la wengine kugombea ingekuwa udikteta. Wananchi kama hawamtaki Mbunge wana haki ya kumbadilisha, lakini kama wanampenda unaanzia wapi kuwanyima haki ya kumchagua tena. Msisahau kuwa Mbunge ni mali ya wananchi anaowawakilisha na wana uamuzi naye baada ya hiyo miaka mitano, sasa kwa nini tulazimishie awekewe ukomo? Nini hoja zenu kwenye hili? Ama ni wivu tu na chuki zilizojengeka bila sababu za msingi dhidi ya wabunge?

Tungekuwa makini kidogo tu zaidi ya hapa tulipo sasa hivi tungejifikiria kubadili mfumo wa watendaji wakuu wa serikali, maana hawa ndiyo wanaofanya kazi za kila siku zinazowagusa wananchi, ndiyo wenye mafungu na ndiyo wataalamu - tungeweka fursa ya ushindani kwa hawa kila baada ya miaka mitano ya mkataba ili kuruhusu ushindani na kuingiza mawazo mapya kwa njia ya usaili. Hawa wana dhamana kubwa sana lakini hakuna anayewatazama, mnahangaika na wabunge (wanaopiga kelele bure tu bila meno ya kuuma!)

Utofauti wa Urais na Ubunge kwenye hili uko wazi sana; tazama majukumu makubwa matatu ya Rais: mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu...haya ni madaraka na mamlaka makubwa sana kuwekwa kwa mtu mmoja, akiwa hatoshi ama mbaya na akaamua kung'ang'ania kwenye madaraka mtakoma naye! Na pia kwa madaraka aliyonayo...na kwa kuzingatia mfumo wa Presidential system ambao tunaufuata sisi, Rais wetu ni Rais Mtendaji (Executive President), hivyo kumuwekea ukomo ni jambo la msingi - japokuwa anaowateua na kupa madaraka makubwa sana hawana ukomo! Huyu Rais na Mbunge (asiye mtendaji) ni tofauti sana...Mbunge ni mpiga kelele tu na mpaka akasikilizwe basi kazi ipo! Watendaji wengine siku hizi hata wameishawadharau mawaziri na wabunge kwa kuwa hawana madaraka yoyote yale ya maana...wanamuogopa Rais tu!

Nadhani nimewajibu na wenzako wote wenye hoja kama zako. Ni kwa msingi huu mimi nitatetea tunapoifanyia kazi Rasimu ya Warioba, tubadilishe hiki kifungu haraka!

Wakatabahu,
HK.

NB: Mimi binafsi naweza kugombea Ubunge mara moja tu tena ama kutogombea kabisa...bado natafakari. Kwa hiyo ninachokisema hapa hakina uhusiano wowote ule na Ubunge wangu ama hali yangu ya kisiasa ya sasa.

Mh Kigwangalla,

Kwanza; ninaheshimu maoni yako. Lakini tunawaonee wabunge wivu kwa nini? Ina maana hata wale wanaopinga ubunge wa maisha wakiwa tayari ni wabunge nao wanaona wivu? Pili, usawa gani unauzungumzia kati ya mtu ambaye amekuwa mbunge au kwenye serikali tangu uhuru, mwenye rasilimali za kutosha, mtandao mkubwa nje na ndani ya serikali na kijana aliyemaliza St. Augustine, mwenye deni la Bodi ya Mikopo, hana kazi inayoeleweka lakini pia mwenye haki za kisiasa pia ya kupiga au kupigiwa kura? Is this what you call equality?

Tatu, kama kazi ya mbunge ni kupiga kelele, amepewa vipindi viwili, vitatu na kelele zake hazijaweza kusikika na kuleta mabadiliko kwa wananchi, unategemea miujiza gani akipewa kipindi cha nne? Au yeye pekee ndiye mwenye sauti katika eneo hilo?

Nne, ingawa sina nia lakini kama mtanzania hata mimi ninaweza kuwa mbunge Mungu akipenda siku moja na hivyo hicho ninachokiunga mkono kikanihusu pia, so nothing personal in my supporting term limit. Tujenge mentality ya ukomo hata kwenye vyeo vya kawaida la sivyo tunaweza kushtukia tunapata viongozi wa kudumu katika uongozi wa juu wa nchi. Kama mtu hana utashi wa ukomo katika ngazi za chini haitakuwa ajabu akipata uongozi wa juu asione umuhimu wa ukomo pia.
 
Back
Top Bottom