Kihesa Mgagao, Masege na Msalali Sasa Shida ya Maji Imeisha

Kihesa Mgagao, Masege na Msalali Sasa Shida ya Maji Imeisha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Kumtambulisha Mkandarasi Mradi wa Maji Kihesamgagao- Masege na Masalali

Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Mhe. Justin Nyamoga akiwa na uongozi wa RUWASA Wilaya ya Kilolo wamemtambulisha na kumkabidhi eneo la kutekeleza mradi wa ujenzi na usambazaji maji mkandarasi Mponela Construction JV Dimotoklasa wa Vijiji vya Kihesamgagao, Masege na Masalali ambao mkataba wake ulisainiwa tarehe 23/08/2023 na ujenzi wake unatarajiwa kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 18/09/2023.

Mradi huu unatarajiwa kugharimu jumla ya TZS Bilioni 1.6 bila VAT kwa muda wa miezi 6 ambapo utanufaisha jumla ya wakazi 5,561 (Masalali 1,653; Masege 1,460 na Kihesamgagao 2,448)

Idadi hii itaongeaza kusaidia kufikisha idadi ya watu 154,781 sawa na 77% ya wakazi wote wa vijijini wilayani Kilolo na kusogeza kufikia malengo ya dira ya Taifa ya 2025 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025

Kuchelewesha kwa utekelezaji wa mradi wa Maji wa Masege na Masalali ulisababishwa na Kijiji cha Kihesamgagao ambacho hakikuwepo kwenye mpango wa awali hivyo ililazimu kurudia upya kuandaa mradi ambao utajumuisha na Kijiji cha Kihesamgagao.

#MajiNiUhai
#MajiBombani
#KumtuaMamaNdooKichwani

WhatsApp Image 2023-09-15 at 01.57.35.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-15 at 01.57.37(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-15 at 01.57.36(1).jpeg
 
Back
Top Bottom