Kihongosi na Arusha nako utafanya kama ulivyofanya Simiyu?

Joined
Jan 30, 2023
Posts
74
Reaction score
80
RC Kihongosi akiwa RC Simiyu amelaumiwa sana na wananchi kwa kutumia muda mwingi kufanya siasa za sanaa za kurekodi clip na kumtumia Mh. Rais kwamba anafanya kazi nzuri ya kuwasaidia wananchi.

RC Kihongosi amelaumiwa sana kwa kuua zao la pamba kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo Bashe kwa kuwapa bei ndogo huku wanunuzi wakubwa wa zao la Pamba wakitajwa kuwa viongozi wakubwa wa kisiasa na kupanga bei wanayotaka.

Rc Kihongosi amelaumiwa kwa kufanya siasa za kusomba wananchi kwa malori na kuwalipa posho ili wafike kwenye mikutano yake na kupiga picha kutuma mitandaoni kuonyesha anakubalika kwa wananchi.

Mwisho wananchi wa Simiyu wamebaki na matatizo yao na hakuna alama hata moja ambayo ameiacha simiyu ya kuwasaidia kupiga hatua yoyote hadi leo wananmkumbuka RC Kafulila kama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu aliyepambana na Rushwa, Ufisadi na kupambana na walanguzi wa zao la Pamba.

Swali je watu wa Arusha watakubali kusafirishwa na Malori kwenda kwenye mikutano ya Kihongosi ili kupiga picha kuzituma mitandaoni?
 
Kihongosi amekunywa maji ya bendera ya CCM. Wapnzan wajiaandae kisaikolojia jamaa ni mhuni sana. Anajua kutesa wapinzani. Namuona kama Chalamila wa Iringa hivi ndo huyu sasa na wote ni wala mbwa. Kiufupi ni katili sana huyo jamaa
 
Kihongosi apewe maua yake anafanya kazi kweli hata kama kuna maigizo ni machache sana ambayo kila kiongozi anafanya.
Tangu kipindi cha JPM huyu kijana alikua anatoka ofisini kwenda kutatua kero zilizopo ndani ya uwezo wake
 
RC Kihongosi amelaumiwa sana kwa kuua zao la pamba kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo Bashe kwa kuwapa bei ndogo huku wanunuzi wakubwa wa zao la Pamba wakitajwa kuwa viongozi wakubwa wa kisiasa na kupanga bei wanayotaka.
Kwenye hili la ununuzi wa mazao ya biashara kufanya na wakubwa, Kihongosi mtamuonea tu.

Nenda tabora kwenye zao la tumbaaku utakutana na makampuni ya wanasiasa yakiwadhulmu wakulima.

Nenda kusini kwenye korosho, utakutana na wanasiasa ndiyo wanawaibia wakulima.

Tudai mabadiliko
 
RC Kihongosi akiwa RC Simiyu amelaumiwa sana na wananchi kwa kutumia muda mwingi kufanya siasa za sanaa za kurekodi clip na kumtumia Mh. Rais kwamba anafanya kazi nzuri ya kuwasaidia wananchi.

RC Kihongosi amelaumiwa sana kwa kuua zao la pamba kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo Bashe kwa kuwapa bei ndogo huku wanunuzi wakubwa wa zao la Pamba wakitajwa kuwa viongozi wakubwa wa kisiasa na kupanga bei wanayotaka.

Rc Kihongosi amelaumiwa kwa kufanya siasa za kusomba wananchi kwa malori na kuwalipa posho ili wafike kwenye mikutano yake na kupiga picha kutuma mitandaoni kuonyesha anakubalika kwa wananchi.

Mwisho wananchi wa Simiyu wamebaki na matatizo yao na hakuna alama hata moja ambayo ameiacha simiyu ya kuwasaidia kupiga hatua yoyote hadi leo wananmkumbuka RC Kafulila kama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu aliyepambana na Rushwa, Ufisadi na kupambana na walanguzi wa zao la Pamba.

Swali je watu wa Arusha watakubali kusafirishwa na Malori kwenda kwenye mikutano ya Kihongosi ili kupiga picha kuzituma mitandaoni?
Akija na siasa za aina hiyo arusha watamshangaza, arusha sio simiu
 
Ana roho ya kikatili.
Ameonekana ndie anafaa kupelekwa Arusha kwa sababu ni dhahiri Makonda alikuwa ameshindwa kazi Arusha.

Nidhamu pale nimeona wale wananchi walikuwa na nidhamu sana katika mkutano wa Rais,so disciplined,it was almost indecent.
 
Back
Top Bottom