Kihongosi: Tunaona wenzetu wanapenda kuombaomba michango. Msiwachangie

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewakosoa vikali wanasiasa wanaotegemea michango ya wananchi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni “kuombaomba kisiasa,” kikiwataka Watanzania kuelekeza fedha zao kwenye shughuli za maendeleo badala ya kuchangia miradi isiyo na uwazi.

Akizungumza leo Aprili 17, 2026 wakati wa ziara yake mkoani Geita, Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi alisema chama hicho kinaamini katika kujenga uchumi imara kupitia uwekezaji, badala ya kutegemea michango ya wananchi.

“Tunafanya kazi na watu wote bila kujali vyama, lakini tunachotanguliza ni maslahi ya taifa. Sasa tunaona wenzetu wanapenda kuombaomba michango na wametangaza tone tone, wakati wenzao wengine wanaishi maisha mazuri nje ya nchi, bado wanataka fedha za Watanzania. Msiwachangie,” alisema.

Kihongosi alidai kuwa baadhi ya wanaoomba michango hiyo hawana uwazi wa matumizi ya fedha hizo, akiwaita “makanjanja wa kisiasa,” huku akihimiza wananchi kuwa makini na matumizi ya fedha zao
Your browser is not able to display this video.
 
Ili umuelewe huyu na mwenzie madelu inabidi kwanza uwe mlevi haswa wa konyagi
 
ccm karibia wote hawana akili timamu...
Walipora viwanja vya mpira na maeneo ya wazi kote nchini.
Sasa si bora aombaye kuliko mporaji!
 
CCM inachota kodi zetu bila huruma ndiyo sababu siku hizi hatusikii vilio vya wafanyakazi wake wakilalamika kukosa mishahara.
 
Pumbaavu.
 
Kuna namna ukisha kuwa veggie automatically una kuwa mjinga.Au ni wanao hutubiwa wanachukuliwa kuwa matutusa ndio maana viongozi wana ropokq namna hii?
 
Ili umuelewe huyu na mwenzie madelu inabidi kwanza uwe mlevi haswa wa konyagi
Mimi ni mnywaji na mlevi sana wa Konyagi lakini sijawahi muelewa Madelu wala mwana CCM yeyote wa zama hizi.
 
Acha roho mbaya, wivu na chuki watetezi wa kweli wataifa hili tutawachangia kwa wivu mkubwa na kwa upendo kutoka kwenye mioyo yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…