Kihongosi: Tunaona wenzetu wanapenda kuombaomba michango. Msiwachangie

Kihongosi: Tunaona wenzetu wanapenda kuombaomba michango. Msiwachangie

Hakuna anayetaka kuichangia cdm ataacha kwa kuambiwa na Kihongosi. Ccm wakubali tu kuishi kwa shida hivyo hivyo na cdm, kwani uwezo wa kuwashinda tena kiushawishi wa kisiasa ni kama haiwezekani.
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewakosoa vikali wanasiasa wanaotegemea michango ya wananchi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni “kuombaomba kisiasa,” kikiwataka Watanzania kuelekeza fedha zao kwenye shughuli za maendeleo badala ya kuchangia miradi isiyo na uwazi.

Akizungumza leo Aprili 17, 2026 wakati wa ziara yake mkoani Geita, Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi alisema chama hicho kinaamini katika kujenga uchumi imara kupitia uwekezaji, badala ya kutegemea michango ya wananchi.

“Tunafanya kazi na watu wote bila kujali vyama, lakini tunachotanguliza ni maslahi ya taifa. Sasa tunaona wenzetu wanapenda kuombaomba michango na wametangaza tone tone, wakati wenzao wengine wanaishi maisha mazuri nje ya nchi, bado wanataka fedha za Watanzania. Msiwachangie,” alisema.

Kihongosi alidai kuwa baadhi ya wanaoomba michango hiyo hawana uwazi wa matumizi ya fedha hizo, akiwaita “makanjanja wa kisiasa,” huku akihimiza wananchi kuwa makini na matumizi ya fedha zao
View attachment 3575058
Hiki chama hususani kwenye hiyo post ya Ukatibu mwenezi sijui kwanini tangu atoke Nape waliofuata wote wana tabia za kitoto na kijinga.
 
Back
Top Bottom