PostGE2025 Kihongosi: Wanasiasa acheni kutumia Majeraha ya Oktoba 29 kujinufaisha Kisiasa

PostGE2025 Kihongosi: Wanasiasa acheni kutumia Majeraha ya Oktoba 29 kujinufaisha Kisiasa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hiki kinyang'au kinataka tusahau kirahisi ndugu zetu?

Wameua watu na kufukia kama mizoga halafu wakasema nguvu iliyotumika ilikua sawa.
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (Itikadi, Uenezi na Mafunzo), Kenani Kihongosi, amewataka wanasiasa na vyama vya siasa nchini kuacha kutumia matukio ya Oktoba 29 kama ajenda ya kujijenga kisiasa, badala yake wawe wavumilivu na kusubiri matokeo ya Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na Rais.

Akizungumza na Clouds Digital 19/08/2026 kwenye mahojiano ya moja kwa moja Kihongosi ameeleza kuwa Serikali imechukua hatua za makusudi kwa kuunda tume hiyo ili kubaini chanzo, waliohusika na hatua za kisheria zitakazochukuliwa, hivyo hakuna haja ya kuendelea kulizungumza jambo hilo majukwaani kwa nia ya kutafuta maslahi binafsi. Amesisitiza kuwa kuendelea kulihubiri tukio hilo ni kuongeza majeraha kwa wananchi waliopoteza ndugu zao, badala ya kuonyesha huruma kwa maisha ya Watanzania na taifa kwa jumla.

Soma pia: Kihongosi: Kuna watu wanatumia video za matukio ya Oktoba 29 kama mtaji wa kisiasa

Kihongosi ametoa rai kwamba matukio hayo yanapaswa kutumika kama funzo la kulinda amani na umoja, huku akisisitiza haja ya wanasiasa kushirikiana katika kurudisha maridhiano na mshikamano ili kujenga taifa moja na kusukuma mbele maendeleo ya wananchi.

Natamani angemtaja na aliyesababisha majeraha hayo.
 
Back
Top Bottom