Kiingereza cha kuongea

Kiingereza cha kuongea

Mr pesa

Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
79
Reaction score
7
Nimehitimu kidato cha nne mwaka juzi lakini sijui kingereza cha kuongea wala kuandika ujumbe. Wana Jf nifanyeje ili niwe mkali katika lugha hii
 
Tafuta mtu au watu utakaoweza kufanya nao mazoezi. Mazoezi ya kuongea na hata kuandika. Pia, jenga utamaduni wa kusoma kamusi - iwe ya Kiingereza pekee au hata ya Kiingereza-Kiswahili au Kiswahili-Kiingereza. Soma magazeti ya Kiingereza, angalia runinga hasa vipindi vilivyo katika lugha hiyo. Nunua flash cards ambazo utazitumia kuandika misamiati mipya na uwe unazibeba kila uendapo - kiasi tu lakini.
 
Kuongezea yaliyoandikwa hapo juu jitahidi kuangalia sana TV hususani stesheni kama BBC, CNN, Al jazeera zitasaidia kwa kiasi fulani. Pia cha muhimu jijengee utaratibu wa kusoma na kutafuta watu ambao utaweza kuwa unawasiliana nao kwa lugha hiyo.
 
Tafuta mtu au watu utakaoweza kufanya nao mazoezi. Mazoezi ya kuongea na hata kuandika. Pia, jenga utamaduni wa kusoma kamusi -
Asanteni sana Nyani na LUSAJO Kwa ushaur wenu mzuri ntatekeleza kama mlivyo nielekeza naamini ntaweza
 
Eti wanaJF vipi kuhusu sehemu wanazotoa English course kwa miezi michache nikienda kusoma siitanisaidia au wazinguaji tu.
 
Nenda british council kasome pale wakujenge kwanza. Pale watakupa mtihan kupima levo yako. Amini usiamin pale ni mahali sahihi kama unataka kufaham kwa ufasaha lugha.
 
Ungekuwa na uwezo ungeenda Zambia au Malawi Au Zimbabwe huko Kiingereza ndio kiswahili chao na kwa kuwa itakubidi kuongea itakusaidia kukujengea uwezo wa kuongea,siri ya kujua lugha ni kuongea na wenye lugha ni sawa na kama unataka kujua Kinyakyusa we shuka tu Makandana ,kaa hapo mwezi huku ukijichanganya na wenyeji hata kwa kuongea kinyakyusa mbofumbofu baada ya muda utakuwa unatema ugonile kama wewe ndio ugonile orijino
 
Anza kunywa pombe utajikuta unaongea 2 kidhungu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nenda british council kasome pale wakujenge kwanza. Pale watakupa mtihan kupima levo yako. Amini usiamin pale ni mahali sahihi kama unataka kufaham kwa ufasaha lugha.
British council? iko maeneo gan
 
Anza kunywa pombe utajikuta unaongea 2 kidhungu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

mjomba acha utani kwa hili.ulishawahi kunywa hiyo pombe ukaanza kuongea kiingereza? Ndgu unayehitaji kuongea na kuandika kizungu nikuulize unajua vema kiswahili au lufha yako ya mama?
 
Nenda british council kasome pale wakujenge kwanza. Pale watakupa mtihan kupima levo yako. Amini usiamin pale ni mahali sahihi kama unataka kufaham kwa ufasaha lugha.

Mkuu shafinho hivi pale British Council huwa wanalipa kiasi gani? kwa kozi, maana kuongea lugha sanifu ni tatizo la wengi hivyo sio mbaya tukipata msasa.
 
Last edited by a moderator:
British council, is a UK cultural centre,like many other countries cultural centres found in tz,one of their duty is to promote british culture which incl their language. They found at samora aven,they are conducting two modules of learning engl language, first is engl practice (which incl engl for beginner,interm level and adv level),when you go there you they arrange an appointment with you in which you will meet an english lady for speaking session (in which you will be asked different unplanned engl qstns abt hobbies and life in general) from this discusn is where they may group you in suitable level as beginner,interm or advanced. Other module is TOEFL (test of engl as foreign lang), this is specifically for those who are preparing to join in university in countries which are using engl as teaching lang,they must be tested either physically or online and their scores must be shown at their cert. (below certain scores,you cant be enrolled).
 
Back
Top Bottom