Kiingereza cha Rais Samia

Kiingereza cha Rais Samia

Akiwa anasoma, kuna afadhali kidogo.

Lakini akiwa anaongea kutoka kichwani ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa], anapata shida sana.

Yaani Magu na Hangaya walichaguana wote wakiwa weupe kwenye hiyo lugha pendwa.

Muangalie na msikilize kwenye video hapo chini. Yale ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa] kwenye karatasi, anapata shida kuyaongea.

Anajiuma uma tu. Hajiamini. Mpaka hata taarifa za ukweli [facts] anazikosea.

Uchaguzi mkuu wa Marekani wa 2020 haukuwa uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo kuwa na mwanamke kama mgombea umakamu wa Rais.

Wakati Geraldine Ferraro anagombea kwenye tiketi moja na Walter Mondale, Hangaya alikuwa wapi?

Wakati Sarah Palin anagombea na John McCain, Hangaya alikuwa wapi?

Au alitaka kusema kuwa 2020 ndo mara ya kwanza kwa mwanamke kuwa katika tiketi iliyoshinda uchaguzi lakini akajiuma uma na akakosea hizo basic facts?

Halafu, ni ‘the United States and Tanzania have enjoyed excellent relations [siyo relation], for the last [past sounds much better] 60 years’.

Halafu kuna watu wanadai eti Hangaya yuko vizuri kwenye Kiingereza [emoji1787]. Ama kweli hii lugha ni janga la kitaifa.

Maana mtu yeyote aijuaye vizuri hiyo lugha hawezi kusema eti Hangaya yuko vizuri.

Hangaya na Magu labda wanapishana kwenye lafudhi tu. Magu alikuwa na lafudhi nzito/ nene zaidi. Hangaya ya kwake si nzito kivile, hivyo kuonekana kama vile anaimudu, kumbe wapi!

Kwenye sintaksia, semantiki, sarufi, kunyambua vitenzi, n.k., hawapishani sana. Wote mulemule tu.

Hoja ya lugha ni ya kipumbavu sana kujadiliwa. Sijui nani kawaambia lugha (hasa kiingereza) ndio kila kitu? English sio lugha yake na hata hivyo huwezi tegemea perfection kutoka kwake kwa lugha isiyokuwa yake. Ni jambo la kawaida sana, na kama hujui ni kwamba Spain, Portugal, German, China Russia, Brazil na mataifa menine yenye lugha zao huwa wanajifunza kiingereza kama sisi tu! Usibabaike sana na lugha za watu wau kuwakosea wengine heshima kwa utamaduni usiokuwa wao!
 
Naomba nitoe ushauri na kuwatoa ushamba ndugu ZANGU kiingereza kwetu ni lugha ya kujifunza sio lugha MAMA na sio kwetu tu Hata KWA mataifa MENGINE makubwa kama china na urusi!!KWA huo hatuwezi kuiongea KWA lafudhi kamili ya wazungu au wamarekani!!kuongea kama wao sio kielelezo Cha u competence KWENYE lugha na utendaji tuachane na huo ushamba mbona hamuwakosoi wachina wanavoongea au warusi mmekomalia waswahili PEKEE!!?Mama ameeleweka na wamarekani wamemwelewa Sana!!! Ni nyie tu mmekosa mantiki!!
Huwezi linganisha China, Russia na hii nchi yetu ambayo ni ushuzi.

Hao ni wababe wa dunia, hao wanakoromeana na US uso kwa uso na kupigana vikumbo, sisi tunaweza? Hao ni wakubwa wa dunia usiwaige, sisi bado wanafunzi kidato cha kwanza wanabeba madawati, mifagio na ndoo kwenda shule.

Yaani wewe utapata faida zaidi ukijua Chinese kuliko Swahili.

Ukweli mchungu, lakini haina budi usemwe, hizi nchi zetu ni ushuzi tu..
 
Sina Nia ya kubeza Imani ya mtu...zamani nikiwa mdogo nilikuwa na rafiki ambaye alikuwa anasoma kitabu flani cha dini yake kilichondikwa kwa lugha ya kigeni sasa siku moja nikaokota kipande cha gazeti ambalo limeandikwa kwa lugha hiyo nikamuomba aniambie gazeti Hilo limeandika kuhusu nini? Rafiki huyo akaniambia maandishi ya misahafu siyo sawa na maandishi ya gazeti japo ni lugha ile ile! Nilikuja kugundua kuwa huwa wanakaririshwa tu hata maana yake hawajuhi....kama mama alipitia masomo kama hayo hawezi kuhoji anachiandikiwa nini maana kukariri ndiyo asili yake!
Wameboresha siku hizi kukariri wanaita "KUHIFADHI"
 
tukubali tukatae,moja kati ya kosa kubwa ambalo nyerere na viongozi waliomfatia wamelikosea taifa hili, ni kutoruhusu lugha ya kingereza itumike kufundishia kuanzia shule ya msingi.

hili ni kosa kubwa sana, moja ya athari zake ndio kama hii ya watz wengi kuzungumza kingereza kibovu sambamba na kukosa confidence tunapokuwa kwenye international platform zinazokusanya watu wa mataifa mengine.
 
Watu wa kulaumiwa ni wasaidizi wake. Wao ndio wanaoandika hotuba. Vitu kama mgombea wa kwanza mwanamke wa umakamu wa urais havikutakiwa kuwepo, hasa enzi hizi za Google. Unless walikuwa wanamaanisha mgombea mwanamke mweusi. Kitu kingine ni party politics. Hapakuwa na haja ya kupongeza ushindi wa Tsunami wa Democrats wakati ukweli ni kuwa ushindi wao ulikuwa mwembamba sana na kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza House na Senate mwaka huu. Angeipongeza tiketi ya urais basi. Yote haya yanaonyesha kuwa wasaidizi wake hawako makini. Hilo anatakiwa alishughulikie mapema iwezekanavyo.

Amandla...
Huyu babu ni place holder tu.

Ona hapa…..sijui alikuwa anashikana na nani mkono. Imaginary friend wake? 🤣

Watu hawakumpigia kura yeye.

Walipiga kura dhidi ya Trump na yeye Biden kama place holder ndo akajikuta yupo kwenye hiyo nafasi.

Na kama ulivyosema, haukuwa ushindi wa kishindo.

Hangaya hazijui dynamics za US elections.

Ni kura takriban 40,000 na kitu tu ndizi zilizoamua mshindi.

Ku comment kuhusu party politics ni diplomatic faux pas.
 
Hapana.

Fluency haihusiani na kusoma vilivyoandikwa.

Ni kwamba hana lafudhi nzito/ nene. Hicho ndicho kinachomfanya aonekane ana afadhali.

Lakini maneno mengi sana yanampa shida kuyatamka.

Hata yale maneno ya kawaida ya hiyo lugha hawezi kuyatamka vizuri.

Ukimwandikia neno kama ‘xylophone’ au ‘discombobulation’, anaweza kupoteza fahamu akijaribu kuyatamka.
Ukimwandikia neno kama ‘xylophone’ au ‘discombobulation’, anaweza kupoteza fahamu akijaribu kuyatamka.😂😂😂😂😂😂😂
 
Yaani Tz ukiwa na stress umejitakia[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Unacheka Anna…??

Hebu jaribu kuyatamka wewe hayo maneno uone
Kuna waziri mmoja,mwanama na ana PhD ushawahi msikia akitema ngeli

Ova
 
Kipindi JPM anawasisitizia kujikubali,kujiaamini na kuthamini lugha yetu ya kiswahili,si mlimwita mshamba kutoka chato ?..sasa leo ndio mnaona umuhimu huo baada ya bibi yenu kupuyanga?
Sijawahi diss kiongozi yoyote kwenye upande wa lugha

Ova
 
Kiswahili kitamsaidia nini?
Kazi ipo kwetu tujue English ili tujikombe tukaombe misaada.

Kiswahili kitamsaidia nini mzungu?
Utumwa huo

Mbona wazungu wanakuja wanajifunza kiswahili

Unajua kwanini?

Ova
 
Akiwa anasoma, kuna afadhali kidogo.

Lakini akiwa anaongea kutoka kichwani ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa], anapata shida sana.

Yaani Magu na Hangaya walichaguana wote wakiwa weupe kwenye hiyo lugha pendwa.

Muangalie na msikilize kwenye video hapo chini. Yale ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa] kwenye karatasi, anapata shida kuyaongea.

Anajiuma uma tu. Hajiamini. Mpaka hata taarifa za ukweli [facts] anazikosea.

Uchaguzi mkuu wa Marekani wa 2020 haukuwa uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo kuwa na mwanamke kama mgombea umakamu wa Rais.

Wakati Geraldine Ferraro anagombea kwenye tiketi moja na Walter Mondale, Hangaya alikuwa wapi?

Wakati Sarah Palin anagombea na John McCain, Hangaya alikuwa wapi?

Au alitaka kusema kuwa 2020 ndo mara ya kwanza kwa mwanamke kuwa katika tiketi iliyoshinda uchaguzi lakini akajiuma uma na akakosea hizo basic facts?

Halafu, ni ‘the United States and Tanzania have enjoyed excellent relations [siyo relation], for the last [past sounds much better] 60 years’.

Halafu kuna watu wanadai eti Hangaya yuko vizuri kwenye Kiingereza [emoji1787]. Ama kweli hii lugha ni janga la kitaifa.

Maana mtu yeyote aijuaye vizuri hiyo lugha hawezi kusema eti Hangaya yuko vizuri.

Hangaya na Magu labda wanapishana kwenye lafudhi tu. Magu alikuwa na lafudhi nzito/ nene zaidi. Hangaya ya kwake si nzito kivile, hivyo kuonekana kama vile anaimudu, kumbe wapi!

Kwenye sintaksia, semantiki, sarufi, kunyambua vitenzi, n.k., hawapishani sana. Wote mulemule tu.

Errors of facts kwenye prepared speech ni kielelezo cha uvivu. Mtu ambaye anajishughulisha hawezi kushindwa kugundua makosa ya wazi kama hili kwenye hotuba aliyotayarishiwa na wasaidizi wake!
 
Akiwa anasoma, kuna afadhali kidogo.

Lakini akiwa anaongea kutoka kichwani ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa], anapata shida sana.

Yaani Magu na Hangaya walichaguana wote wakiwa weupe kwenye hiyo lugha pendwa.

Muangalie na msikilize kwenye video hapo chini. Yale ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa] kwenye karatasi, anapata shida kuyaongea.

Anajiuma uma tu. Hajiamini. Mpaka hata taarifa za ukweli [facts] anazikosea.

Uchaguzi mkuu wa Marekani wa 2020 haukuwa uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo kuwa na mwanamke kama mgombea umakamu wa Rais.

Wakati Geraldine Ferraro anagombea kwenye tiketi moja na Walter Mondale, Hangaya alikuwa wapi?

Wakati Sarah Palin anagombea na John McCain, Hangaya alikuwa wapi?

Au alitaka kusema kuwa 2020 ndo mara ya kwanza kwa mwanamke kuwa katika tiketi iliyoshinda uchaguzi lakini akajiuma uma na akakosea hizo basic facts?

Halafu, ni ‘the United States and Tanzania have enjoyed excellent relations [siyo relation], for the last [past sounds much better] 60 years’.

Halafu kuna watu wanadai eti Hangaya yuko vizuri kwenye Kiingereza [emoji1787]. Ama kweli hii lugha ni janga la kitaifa.

Maana mtu yeyote aijuaye vizuri hiyo lugha hawezi kusema eti Hangaya yuko vizuri.

Hangaya na Magu labda wanapishana kwenye lafudhi tu. Magu alikuwa na lafudhi nzito/ nene zaidi. Hangaya ya kwake si nzito kivile, hivyo kuonekana kama vile anaimudu, kumbe wapi!

Kwenye sintaksia, semantiki, sarufi, kunyambua vitenzi, n.k., hawapishani sana. Wote mulemule tu.

Nimemsikiliza Hangaya, ana uwafadhali sana tena sana ukimlinga na Dr Jiwe, Dr Jiwe anaachwa mbali sana na Hangaya kwenye hii lugha.

Kama kuna mtu yeyote anabisha haya nisemayo aje kuthibitisha kwa ushaidi wa klip yake yoyote akiongea kiingereza Dr Jiwe.

Kuhusu kukosea juu ya kusema kuwa Kamala ndio mwanamke wa kwanza kugombea nafasi ya umakamu urahisi Marekani, kama mnakunbuka jiwe alisema kuwa Saddam Hussein Kuwait kipindi cha kampeni za 2015. mbele ya watanzania wenzake akiwa anaongea kiswahili kabisa.

Dr. Jiwe hakika aliufahamu udhaifu wake ndio maana hakutaka kutoka nje ya nchi hasa nchi za Ulaya na America, alifahamu atashikwa kigugumizi tu, badala yake akawa anawapekeka mama Samia na Majaliwa.

Nb. Anaepinga kuwa Dr. Jiwe hakujua kuongea lugha ya kiingereza aweke klip yake hapa.
 
Back
Top Bottom