Kiingereza cha Rais Samia

Mimi tokea nimuone anaweka "he" sehemu ya "she" yani naogopa kuangalia interview zake za english..
Lakini kwa ujumla anajitahidi sana ukilinganisha na jiwe
Makosa yake ni madogo madogo ingawaje mi nashindwa kuyavumilia so nimeamua nisiangalie interview zake za english kwa heshima yake mama yetu huyu.
 
Wewe unakijua kingereza fasaha ukiwa umekaa Marekani miaka mingi nadhani miaka zaidi ya 25. Nyinyi ndio mliondoka TZ miaka ya 1990-95 wakati pakiwa na vuguvugu la kukimbia Tanzania ile ya Mwinyi akiwa anajiandaa kuondoka ikulu.

Tanzania hatuna utamaduni wa kuongea lugha moja tu asubuhi mpaka jioni januaty mpaka december, huwa tunazichanganya mara kwa mara.

Ni vigumu kuongea na muuza madafu au muuza maembe Muha wa Kigoma lugha ya malkia, utakuwa kama unamnyanyasa.

Lakini mataifa kama Ghana na Nigeria mchokoze yoyote unayemkuta njiani anatiririka na wewe kingereza bila ya kusoma au kugusa kitabu chochote, ni lugha waliyoizoea kuiongea muda wowote saa yoyote.

Hivyo usimshangae sana Hangaya wala hayati JPM, ni matunda ya msingi wetu wa kielimu jinsi ulivyo. Na hapo katika kingereza ndipo wanapotuacha mataifa kama Nigeria kwani wanajichanganya haraka sana na kuwa sehemu ya jamii ngeni za Ulaya na huko Marekani kirahisi tu.
 
Mama yupo vizuri sana. Wazungu wenyewe hata hawashangai mtu akibabaika kuongea kiingereza.
 
Ndiyo maana wanangu nimeamua kujikamua kuwapeka shule ambazo hii lugha pendwa wataongea kama vile kiswahili tu - najua itawaliapa tu mbeleni. Hii lugha ya kimataifa ni muhimu saana saana huwa kuna muda tunajidanganya kwamba eti kiswahili tuanze nacho Primary hadi Degree - maweeee !!

Maza afadhali lakini duh mzee wetu ilikuwa balaa "i dont have a word today like politicians, am here to act like catalyst of this reaction..... "

Mliosoma kemia mtaelewa zaidi hapo !!
 
Acha ushamba na Lugha wewe...Katafute hela, ukiwa na pesa Lugha ni mapambo tu...Wenzako wanakula mema ya nchi, weme umekazana na Lugha ya mkoloni. WATU WEUSI NA KUJIFANYA KUJUA SARUFI NA FASIHI YA KIINGEREZA.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Eti kuna kuna mtu humu anasema wageni kiswahili hakina msaada kwao haha
Wakati wawekezaji wakija wanajifunza mpk wanakielewa

Ova
 
S
i afadhali yeye angalau anangea hata hicho cha kubofoa...mbona husemi Kamala hata kiswahili hajui! angekuja Kamala Tanzania na kubofoa kiswahili wala msingemsema...ndio kwanza mngesifia kuwa angalau amejitahidi....! Nyani Ngabu..hii lugha ilikuja kwa Meli Mkuu....Hangaya ameanzia mbali sana kupata angalau hayo machache aliyomudu kwa Kiingereza, tumpe muda!
 
Muulize yule marehemu mungu wao wa Chato angeweza interview kwa kingereza?
 
Makosa wala sio madogo ni makubwa tu, yake maswali mawili aliyojibu jana nilishangaa kweli
 

Haya ni maono yako mimi naona anaongea vizuri. Kuwa na accent ni kawaida hawakuhitaji mtafsiri. Hata Kiswahili wengine hata wana accent ya kichaga, kihaya, kisambaa, kisukuma, kiarusha.......... English accent ni maono yako tu cha maana unaeleweka
 
Mkuu

Ni bora imejionea mwenyewe huko majuu kinachopambwa hakina sifa hiyo.

Marais walikokuwa wanajiamini katika uongeaji wa lugha ya king'eng'e ni Julius Nyerere na Benjamini Mkapa.

Wengine wote ni wachapiaji tu hawajui matumizi sahihi, fasaha ya grammar na structure zake zinazoendana na hadhira ni majanga ya karne
 
Hawa mabeberu ni watu hatari sana! Wakiona unajikombakomba sana!, watakutafutia kiki uli wakuingize mkenge!
 
"Discombobulation" 😁😁😁
 
Kila nikiuona huu uzi naishia kusema Mkuu Nyani Ngabu kumbe ni bure kabisa hamna kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…