Amani ni muhimu kwa usitawi wa jamii yetu, hawa vijana wanaojiingiza katika masuala ya kupoteza amani mashuleni wadhibitiwe mapema ili kuepusha usumbufu kwa wapenda amani na usitawi wa elimu kwa ujumla. Kibiti secondary ni miaka michache iliyopita matukio kama haya yaliwahi kutokea wenzao wakahamishwa shule ,leo yanaanza kutokea tena. Kumbuka serikali haina dini hivyo angalia madai yenu yanaendana na mahali mlipo? mfano madai ya nyumba za kuabudia, kujitenga mahali pa kulala, kula, kuoga, mwisho mtadai na madarasa ya kwenu wakati mnajua wote mlikutana bila kujuana imani yenu hapo kabla walahamkuletwa hapo kwa sababu ya imani yenu. soma kwa bidii ili ujikomboe namana ya kufikiri ewe kijana. Kwa upande wa Walimu acheni kuwapotezea wanafunzi kwa kuwadanganya kudai vitu ambavyo wewe hukudai wakati unasoma maana huo ni uvivu wa kufanya yale yaliyopo katika malengo yako wewe na wengine hapo shuleni. CHONDE CHONDE EPUKENI HAYA.