Kiini cha matatizo ya Zanzibar, Mapinduzi ya mwaka yaliyomwondoa Sultani

Mkuu ukipenda kubebwabebwa hata iwe vipi, wewe ni masikini tu, na hilo ni mpaka uamue kuondokana na fikra ya kuishi kiutegemezi kwa watu masikini wa Bara.
Limeni, wekezeni, fanyeni kazi.
Mbaya zaidi hata viongozi wenu mambo yakiwaenda vizuri wanajenga DSM badala ya kwao, balaa tupu.
Hoja zimekuishia sasa unaanza viroja. Kaa kimya tu, ili ufiche niniii?
Ni ushauri tu.
 
Mkuu hadithi yako ingeekeweka kama ungeongekea vile vile , yaani wewe na mtu wako huyo aliyekuandikia barua jinsi watu wasio waafrika walivyoingia kisiwa cha waafrika.
Kusema kuwa waafrika walitoka huko bara na wakahamia Zanzibar, ni kujidanganya na kutoukubali ukweli wa waadrika waliokuwepo hapo kwa karne na karne.

Siyo siri, ni kasumba inayowamaliza waafrika wa huko unguja na Pemba , kupenda kuoa wale wasio asili yao.
Wengine hufanya hivyo ili kuonekana kuwa kastaarabika au amekuwa mwungwana.
Offspings za hao watu ndo wako mbele kuukana uafrika wao na kufanya allegience na asili za mama zao.

Hili nimeliona, its a weakness and strenrh at the same time!

Kwa mtu wa matamanio, angeweza kusema pengine baada ya karne Zanzibar itakuwa a mixed race country na hivyo kuondoa chokochoko zote za kisiasa, lakini hata leo si hivyo.
Kwa nini unataka watu waamini "hadithi" yako/zako lakini utake wengine watoe maelezo ya ziada ili uzikubali "hadithi" zao?

Mkuu unaleta longolongo ndefuuuu. Kitu ambacho unakikimbia ni kuusema ukweli. Na ukweli utakuweka huru. Huu ndio ukweli wenyewe.
CCM imeangukia pua kwa mara ingine huko Zanzibar.
CCM imeshindwa kwa mara ingine kupitia kisanduku cha kura.
CCM imekataliwa tarehe 25.10.2015 na wananchi wa Zanzibar kuongoza Serikali ya Zanzibar.

Huu ndio ukweli ambao unautafutia "hadithi" za kupotosha na kupindisha ukweli.

Mwaka 2010 Zanzibar/ wazanzibari walikubaliana kupitia miafaka/muafaka na kikatiba kuwa baada ya uchaguzi ni lazima iundwe serikali ya umoja wa kitaifa. Kwa hiyo, kushindwa kwa CCM haimaanishi kuwa hawatakuwemo ndani ya Serikali itakayoundwa. Kitakachofanyika mara hii ni kubadilishana "role". CUF itaongoza serikali na CCM itakamata "role" ya upinzani. CUF watakamata sukani na CCM itakuwa "conductor/utingo"

Kama tunaikubali demokrasia, basi ni lazima tulaani uhuni wanaoufanya CCM na CCM-Zanzibar. CCM wakabidhi madaraka kwa walioshinda uchaguzi.

Sitapenda urudi hapa na sababu za kizushi. Matokeo yote cha uchaguzi Zanzibar yalishatangazwa majimboni na washindi wa kura za uraisi Muungano ,wabunge wamejulikana pia kura za uraisi wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani zimejulikana.

CCM waache domokrasia, wakae pembeni maisha yaendelee.

Zanzibar hakuna mkwamo wala nini, ulioko ni ubakaji wa demokrasia unaofanywa na CCM.
 
Majibu ya mapinduzi sijui uwafrica, sijui uwarabu, upo humu 1448796430506.jpg
http://www.amazon.co.uk/Kwaheri-Ukoloni-Zanzibar-Mapinduzi-Afrabia/dp/0557384796
 
Masopyakindi,
Tufanye mjadala wa kistaarabu sote tufaidike mie na wewe na watazamaji.
Lugha za ''hadithi,'' mnakasha utaharibika kwani kejeli hazijengi.

Mimi si mpiga hadith.

Inawezekana kwa hakika kulikuwa na Waafrika katika visiwa hivyo wenyeji
na pia wakaja wahamiaji Waafrika na Waarabu kwa karne nyingi.

Historia hii kwa hivi sasa kwa kweli nionavyo mimi haina maana yoyote.
Zanzibar ya karne ya 18 si Zanzibar ya leo ya karne ya 21.

Mengi yamebadilika na ndiyo maana rafiki yangu akaniandikia barua hiyo
niliyoiweka hapo.

Ndiyo maana leo unaona mahasimu wakubwa wa miaka ya 1950 na kabla ya
mapinduzi leo wanaoleana bila kinyongo.

Wala wajukuu hawaelezwi uhasama uliopita kati ya babu zao hadi kufikia
kuuana.

Sitaki kutaja majina kwani kufukua makaburi hakujengi.

Tatizo kubwa linalowakuta watu wa Bara katika muungano ni kudhani kuwa
wenye haki Zanzibar ni hawa mahafidhina licha ya ukweli kuwa kila wakiingia
katika uchaguzi Wazanzibari wanawakataa sasa miaka 20.

Kitu cha kujiuliza hapa ni hii inasabishwa na nini?

Iweje hao wanaojigamba kuwa ni ''wanamapinduzi,'' leo wanakataliwa na
Wazanzibari?
Mkuu bado nasimamia pale pale wewe unspoweka hoja dhanifu.
Ukisema "inawezekana kwa uhakika kulikuwa na waafrika katika visiwa hivyo wenyeji" hapo tayari umejikita katika doubt ambayo watu wengi wapenda kuitumia.

Wengi wenu wanasema "Watu" walioanza kuingia visiwa hivyo ni wale waliotoka Uarabuni na baadaye waliingia watu toka bara.
Pitia mjadala mzima huu na utaona hilo.

Kiukweli ni kwamba visiwa hivi vimekuwa na muingiliano na watu wa bara kwa miaka nenda rudi
Hilo halina ubishi.

Kwamba waarabu waliingia na utamaduni wao na dini yao iliyopokelewa vema na wenyeji vile vile hslina ubishi.

Hapa mimi vile vile nimeweka dhana ya kuchambus ni kwa nini kuna makundi hasimu Zanzibar ya leo, ilihali mapinduzi ya kuondoa kile kilichoonekana kama utawala wa kikandamizaji ulioendelezwa na kundi moja vile vile la kuja , mwaka 1964.

Kuna ambao wamesema wazanzibari walikuwa wakiishi raha mustarehe kabla ya mapinduzi, kitu ambacho ni dhahiri ni uongo.

Sasa nakuuliza wewe Mohamed Said, kama kiini cha mgawanyiko si mapinduzi tu ya 1964, hebu na wewe changia.
Mi siamini kuwa ati kama wasemavyo wengine, watu wa Bara wanaitawal Zanzibar.
Pengine wangeenda mbali na kuwataja hao wabara wanaowatawala.
 
masopakyindi ni kilaza wa CCM na mbumbumbu wa historia ya Zanzibar

Bora kukaa kimya tu kuliko kutema pumba ulizokaririshwa na wahafidhina wa Lumumba...

Acha kuwa gozi...
 
Last edited by a moderator:

Asante , sasa ongea point yako juu ya mjadala maana sijaona kitu hapo.
 
Sasa wewe unaijua historia ya Zanzibar vizuri mbona hushiriki kutatua matatizo yake huko huko kwenu.
Siyo siri wazanzibari kwa midomo na kuongelea matatixo hamjambo, kimbembe ni akili ya kuyatatus hayo matatixo.

Kila anayeongekea utatuzi anaruka kama mmanga na kurushia Tanzania Bara utafikiri suala halimhusu!
Watu wanaendekea kuishi katika vibanda na hawafanyi kazi ya maana kutwa kunywa gahwa na kupiga stori.

Na ukimwuliza kwanini hafanyi kazi ati jibu yake hiyo ni kero ya muungano.
Kwa kupenda kubebwa kama mabebi hamjambo.

Sasa maalim tumia historia yako ili upande mikarafuu zaidi na uache kuagiza maboga, mchele , nyama na kuku toka Bara .
Hapo tutakuelewa kuwa kwa historia uliyo nayo, umeamua kujitegemea na kwuka utu wako mbele.
Ukiwa tegemezi kwa watu masikini vile vile wa Tanganyika, hueleweki ilhali una akili, siha njema na ardhi nzuri tu ya kuendeleza watu wenu.

Wewe kweli hamnazo!!! Sasa hayo maboga, Michele, nyama n.k yanaenda Zanzibar kama msaada au wazanzibar wananunua kwa hela zao!!?? Basi na nyinyi wadanganyika vaa makaniki na matenge maana ndio mnayozalisha!!! Pia hamtakiwi muagize magari, simu, matelevishen n.k na badala yake mtengeneze yenu.

Kuhusu wazanzibar kukakaa kwenye vibanda naona hujielewi unazungumza kitu gani!! Hebu tembelea Zanzibar nzima kama utakutana na uchafu mlionao Tanganyika wa nyumba za matembe!!

Nadhani pia hutambui ninani hasa wavivu kati ya wazanzibar na watanganyika!!! Fanya utafiti kidogo halafu uje tena hapa!!

Mwisho wazanzibar kwa kutumia hela zao wanauwezo wa kununua kitu popote pale duniani kitakapokuwa kinapatikana.
 
Mkuu bado nasimamia pale pale wewe unspoweka hoja dhanifu.
Ukisema "inawezekana kwa uhakika kulikuwa na waafrika katika visiwa hivyo wenyeji" hapo tayari umejikita katika doubt ambayo watu wengi wapenda kuitumia.

Wengi wenu wanasema "Watu" walioanza kuingia visiwa hivyo ni wale waliotoka Uarabuni na baadaye waliingia watu toka bara.
Pitia mjadala mzima huu na utaona hilo.

Kiukweli ni kwamba visiwa hivi vimekuwa na muingiliano na watu wa bara kwa miaka nenda rudi
Hilo halina ubishi.

Kwamba waarabu waliingia na utamaduni wao na dini yao iliyopokelewa vema na wenyeji vile vile hslina ubishi.

Hapa mimi vile vile nimeweka dhana ya kuchambus ni kwa nini kuna makundi hasimu Zanzibar ya leo, ilihali mapinduzi ya kuondoa kile kilichoonekana kama utawala wa kikandamizaji ulioendelezwa na kundi moja vile vile la kuja , mwaka 1964.

Kuna ambao wamesema wazanzibari walikuwa wakiishi raha mustarehe kabla ya mapinduzi, kitu ambacho ni dhahiri ni uongo.

Sasa nakuuliza wewe Mohamed Said, kama kiini cha mgawanyiko si mapinduzi tu ya 1964, hebu na wewe changia.
Mi siamini kuwa ati kama wasemavyo wengine, watu wa Bara wanaitawal Zanzibar.
Pengine wangeenda mbali na kuwataja hao wabara wanaowatawala.
Ndugu
Nchi zote za visiwa zina watu mchanganyiko. Au wewe unaelewa nchi za visiwa ambavyo ni nyeusi nyeusi, au nyeupe nyeupe tu?
Nipatie mifano kama unayo.
Zanzibar kama unaifahamu historia ilikuwa ni trade route kubwa na kituo kikuu cha biashara. Mchanganyiko huko usingeweza kuepukika.
Sasa kuleta ugozi ni kuikana historia hiyo. Unafanya hayo kwa maslahi ya nani?

Huwezi kuzungumzia Dar es salaam na kuondoa mchanganyiko wa makabila na race tofauti unaoupata Dar au mwambao wa pwani ya Tanzania. Zamani dunia ilikuwa ni Pwani na mwambao. Biashara ilifanywa kutumia marikebu, meli na majahazi. Na makaazi ya watu na miji ilinawiri humo.

Longolongo hii ya mapinduzi, mapinduzi daima, nchi ya watu weusi ni siasa muflis.

Hivi maraisi wanaongoza Zanzibar wanachaguliwa wapi? Dodoma au Muscat?

CCM inawachagulia wazanzibari nani awe Raisi wao. Lakini pia polisi na JWTZ vyombo hivi vinatumika kuhakikisha CCM ndio inakuwa "mshindi" wa Urais huko Zanzibar.

Kama unataka kuona ukweli, ivue miwani nyeusi uliyoivaa.

Kama hujui Polisi na Jeshi ni la nani, msikilize MCCM hapa.

Last edited by a moderator:
Sasa wewe unaijua historia ya Zanzibar vizuri mbona hushiriki kutatua matatizo yake huko huko kwenu.
Siyo siri wazanzibari kwa midomo na kuongelea matatixo hamjambo, kimbembe ni akili ya kuyatatus hayo matatixo.

Kila anayeongekea utatuzi anaruka kama mmanga na kurushia Tanzania Bara utafikiri suala halimhusu!
Watu wanaendekea kuishi katika vibanda na hawafanyi kazi ya maana kutwa kunywa gahwa na kupiga stori.

Na ukimwuliza kwanini hafanyi kazi ati jibu yake hiyo ni kero ya muungano.
Kwa kupenda kubebwa kama mabebi hamjambo.

Sasa maalim tumia historia yako ili upande mikarafuu zaidi na uache kuagiza maboga, mchele , nyama na kuku toka Bara .
Hapo tutakuelewa kuwa kwa historia uliyo nayo, umeamua kujitegemea na kwuka utu wako mbele.
Ukiwa tegemezi kwa watu masikini vile vile wa Tanganyika, hueleweki ilhali una akili, siha njema na ardhi nzuri tu ya kuendeleza watu wenu.

Unadhani mtu akiongelea matatizo ya Zanzibar basi nae ni Mzanzibari sio??? Pole sana! Mi Mtanganyika halisi! Mfipa wa Lyamba lya Mfipa!!!
Jifunze ukweli uwe huru!
 
eti vita ya chini kwa chini,mara wanataka kuleta vita ,acha ulongo wa mchana
watu wengi hawajui historia hii ya Zanzibar.

kuna makundi matatu
1. waafrika weusi (waliofanya mapinduzi wengi walikuwa ni vijakazi, na waosha uchafu wa waarabu)
2. waarabu wa omani (hawa ndio waliopinduliwa na kufukuzwa visiwani (aliyekuwa sultani wa Zanzibar ni mu Omani)
3. Washirazi (hawa ni watu wa kati kipindi cha Sultani kabla ya mapinduzi, ni mixed wa arabu na watu weusi)

haya makundi matatu, mawili la kwanza na la tatu yanataka kuendelea kuwa kwenye muungano, wakati hilo la pili wanajaribu kuleta vita kutoka nje ili warudi tena kuendeleza utawala

vita hiyo ya chini chini iko tangu mapinduzi yatokee na Bara haitaruhusu tuwe na utumwa infront of our doors step.
 
Ndugu
Nchi zote za visiwa zina watu mchanganyiko. Au wewe unaelewa nchi za visiwa ambavyo ni nyeusi nyeusi, au nyeupe nyeupe tu?
Nipatie mifano kama unayo.
Zanzibar kama unaifahamu historia ilikuwa ni trade route kubwa na kituo kikuu cha biashara. Mchanganyiko huko usingeweza kuepukika.
Sasa kuleta ugozi ni kuikana historia hiyo. Unafanya hayo kwa maslahi ya nani?

Huwezi kuzungumzia Dar es salaam na kuondoa mchanganyiko wa makabila na race tofauti unaoupata Dar au mwambao wa pwani ya Tanzania. Zamani dunia ilikuwa ni Pwani na mwambao. Biashara ilifanywa kutumia marikebu, meli na majahazi. Na makaazi ya watu na miji ilinawiri humo.

Longolongo hii ya mapinduzi, mapinduzi daima, nchi ya watu weusi ni siasa muflis.

Hivi maraisi wanaongoza Zanzibar wanachaguliwa wapi? Dodoma au Muscat?

CCM inawachagulia wazanzibari nani awe Raisi wao. Lakini pia polisi na JWTZ vyombo hivi vinatumika kuhakikisha CCM ndio inakuwa "mshindi" wa Urais huko Zanzibar.

Kama unataka kuona ukweli, ivue miwani nyeusi uliyoivaa.

Kama hujui Polisi na Jeshi ni la nani, msikilize MCCM hapa.

Masuala ya muungano hayo, semeni tu bila kumung'unya kuwa hamuutaki muungano.
Hapo hapo mnajenga Mbgala na Tandika!
Halafu muwe wa kwanza kukataa viti huko Dodoma maana kwa msimamo wako mtakuwa mnajaza nafasi za posho tu.
 
Last edited by a moderator:
Ubaguzi ndo unawamaliza.
Sasa kama walipindua waafrika toka bara, na nyie wa Omani mlitoka wapi?
Maana huku si kwenu!

Masopakyindi,
Prof. Ibrahim Noor Shariff ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu
"Udini na Ugozi," Tanzania.

Mwandishi kakusudia kuandika kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie
wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.

Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali,
wanasiasa, mapadri na mashekhe.

Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini
zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.

Inatakiwa kila wenye uwezo wafanye juhudi kuondoa propaganda shuleni mwetu
na washikilie kusomeshwa historia ya ukweli.

Kitabu hiki ?Tanzania na Propaganda za Udini? kina milango mitatu na sahifa
152.

  1. Mlango wa Kwanza unahusu ''Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki.'' Hapa anaeleza kwa ushahidi wa taarikh usiokatalika kwamba Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita na Wabantu wamefika pwani hiyo katika karne ya 16 B.K. Makusudio ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa na wenyeji wengineo.
  2. Mlango wa Pili unazungumzia ''Propaganda za Siasa za Chuki na Athari Zake.''Humo tunaona uovu wa propaganda za udini zilizowatuhumu Waarabu na Waswahili Waislamu peke yao kukamata, kuuza na kumiliki watumwa. Propaganda hizo zimepelekea kuuliwa maelfu ya Waislamu bure bila ya sababu ilipovamiwa Zanzibar, nchi yenye Waislamu wengi, na kumezwa na Tanganyika 1964.
  3. Katika Mlango wa Tatu ''Tanzania na Propaganda za Udini Shuleni'' mwandishi, ambae ni Profesa wa Sanaa, anaonesha ubingwa wake wa kuchambua picha. Anatunakilia picha za kuchorwa kutokana na vitabu vya shule za Tanzania zinazoonesha Waarabu na Waswahili Waislamu wanawakamata, kuwapiga na kuwauwa wanyonge wa Kiafrika ili kuwafanya watumwa. Hapohapo Profesa Ibrahim anaonyesha uzushi wa picha hizo zilizokopiwa na kubadilishwa kutoka picha za wauzaji watumwa wa Kizungu huko Amerika. Pia ameonesha kwamba bila ya shaka picha nyingine zimebuniwa na wachoraji na hazina ukweli. Prof. Ibrahim Noor anakazia katika kitabu chake hiki kuyapitia na kuyatengeneza masomo ya taarikh (historia) katika shule za Tanzania. Anataka masomo haya yajengwe kwenye misingi ya taarikh ya kweli, sio misingi ya uongo wa siasa za udini unaotokana na ukoloni.

Prof. Ibrahim Noor ana hadharisha Watanzania wote na hatari ya kuendelea kupanda mbegu za chuki dhidi ya Waarabu, Wahindi na Waswahili na khasa Waislamu katika mipango ya masomo Tanzania. Hizi chuki za udini zitaleta balaa kubwa kuliko mauwaji ya Zanzibar ya 1964. Watakaoumia na chuki hizi ni wafuasi wa kila dini na kila kabila nchini Tanzania. Kitabu hiki kinahitajia kimfikie kila mwenye uwezo wa kubadilisha mambo Tanzania, kwa mfano:

a) Wahishimiwa Memba /Wabunge Tanzania

b) Memba wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

c) Mawaziri wa Serikali ya Muungano wa Zanzibar

d) Wakubwa wa Makanisa na Wakubwa wa Vyama vya Kiislamu

e) Wakubwa wa Vyama vya Siasa

f) Wakubwa wa Magazeti

g) Wakubwa wa TV na Radio

h) Na kabla ya wote hao waliotangulia ni mimi na wewe wananchi ambao tunapiga kura kuwachagua viongozi wema
 
Mkuu bado nasimamia pale pale wewe unspoweka hoja dhanifu.
Ukisema "inawezekana kwa uhakika kulikuwa na waafrika katika visiwa hivyo wenyeji" hapo tayari umejikita katika doubt ambayo watu wengi wapenda kuitumia.

Wengi wenu wanasema "Watu" walioanza kuingia visiwa hivyo ni wale waliotoka Uarabuni na baadaye waliingia watu toka bara.
Pitia mjadala mzima huu na utaona hilo.

Kiukweli ni kwamba visiwa hivi vimekuwa na muingiliano na watu wa bara kwa miaka nenda rudi
Hilo halina ubishi.

Kwamba waarabu waliingia na utamaduni wao na dini yao iliyopokelewa vema na wenyeji vile vile hslina ubishi.

Hapa mimi vile vile nimeweka dhana ya kuchambus ni kwa nini kuna makundi hasimu Zanzibar ya leo, ilihali mapinduzi ya kuondoa kile kilichoonekana kama utawala wa kikandamizaji ulioendelezwa na kundi moja vile vile la kuja , mwaka 1964.

Kuna ambao wamesema wazanzibari walikuwa wakiishi raha mustarehe kabla ya mapinduzi, kitu ambacho ni dhahiri ni uongo.

Sasa nakuuliza wewe Mohamed Said, kama kiini cha mgawanyiko si mapinduzi tu ya 1964, hebu na wewe changia.
Mi siamini kuwa ati kama wasemavyo wengine, watu wa Bara wanaitawal Zanzibar.
Pengine wangeenda mbali na kuwataja hao wabara wanaowatawala.

Masopakyindi,
Kama nilivyokutahadharisha mwanzo kuwa historia ya Zanzibar ya karne ya 18
haiwezi kuwa na maana sana hivi sasa.

Kwa ajili hii basi naona hakuna haja ya mie na wewe tukavutana katika hilo.
Unataka kweli mimi nichangie kuhusu historia ya Zanzibar?

Tuanze na haya machache na ikiwa hujatosheka tutaendelea In Sha Allah
hadi utakaponiambia,''Inatosha.''

Ingia hapa:

  1. Mohamed Said: MAISHA YA SIASA YA SHEIKH ALI MUHSIN BARWANI (1919 - 2006) - KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
  2. Mohamed Said: KUTOKA JAMIIFORUMS: MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA MAMLUKI KUTOKA SAKURA NA KIPUMBWI
  3. Mohamed Said: KITABU MAARUFU ''KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU'' KINACHOELEZA HISTORIA YA KWELI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KIMEWASILI NCHINI
 
Masopakyindi,
Prof. Ibrahim Noor Shariff ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu
"Udini na Ugozi," Tanzania.

Mwandishi kakusudia kuandika kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie
wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.

Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali,
wanasiasa, mapadri na mashekhe.

Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini
zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.

Inatakiwa kila wenye uwezo wafanye juhudi kuondoa propaganda shuleni mwetu
na washikilie kusomeshwa historia ya ukweli.

Kitabu hiki ?Tanzania na Propaganda za Udini? kina milango mitatu na sahifa
152.

  1. Mlango wa Kwanza unahusu ''Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki.'' Hapa anaeleza kwa ushahidi wa taarikh usiokatalika kwamba Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita na Wabantu wamefika pwani hiyo katika karne ya 16 B.K. Makusudio ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa na wenyeji wengineo.
  2. Mlango wa Pili unazungumzia ''Propaganda za Siasa za Chuki na Athari Zake.''Humo tunaona uovu wa propaganda za udini zilizowatuhumu Waarabu na Waswahili Waislamu peke yao kukamata, kuuza na kumiliki watumwa. Propaganda hizo zimepelekea kuuliwa maelfu ya Waislamu bure bila ya sababu ilipovamiwa Zanzibar, nchi yenye Waislamu wengi, na kumezwa na Tanganyika 1964.
  3. Katika Mlango wa Tatu ''Tanzania na Propaganda za Udini Shuleni'' mwandishi, ambae ni Profesa wa Sanaa, anaonesha ubingwa wake wa kuchambua picha. Anatunakilia picha za kuchorwa kutokana na vitabu vya shule za Tanzania zinazoonesha Waarabu na Waswahili Waislamu wanawakamata, kuwapiga na kuwauwa wanyonge wa Kiafrika ili kuwafanya watumwa. Hapohapo Profesa Ibrahim anaonyesha uzushi wa picha hizo zilizokopiwa na kubadilishwa kutoka picha za wauzaji watumwa wa Kizungu huko Amerika. Pia ameonesha kwamba bila ya shaka picha nyingine zimebuniwa na wachoraji na hazina ukweli. Prof. Ibrahim Noor anakazia katika kitabu chake hiki kuyapitia na kuyatengeneza masomo ya taarikh (historia) katika shule za Tanzania. Anataka masomo haya yajengwe kwenye misingi ya taarikh ya kweli, sio misingi ya uongo wa siasa za udini unaotokana na ukoloni.

Prof. Ibrahim Noor ana hadharisha Watanzania wote na hatari ya kuendelea kupanda mbegu za chuki dhidi ya Waarabu, Wahindi na Waswahili na khasa Waislamu katika mipango ya masomo Tanzania. Hizi chuki za udini zitaleta balaa kubwa kuliko mauwaji ya Zanzibar ya 1964. Watakaoumia na chuki hizi ni wafuasi wa kila dini na kila kabila nchini Tanzania. Kitabu hiki kinahitajia kimfikie kila mwenye uwezo wa kubadilisha mambo Tanzania, kwa mfano:

a) Wahishimiwa Memba /Wabunge Tanzania

b) Memba wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

c) Mawaziri wa Serikali ya Muungano wa Zanzibar

d) Wakubwa wa Makanisa na Wakubwa wa Vyama vya Kiislamu

e) Wakubwa wa Vyama vya Siasa

f) Wakubwa wa Magazeti

g) Wakubwa wa TV na Radio

h) Na kabla ya wote hao waliotangulia ni mimi na wewe wananchi ambao tunapiga kura kuwachagua viongozi wema
Mkuu you are seriously drifting away from the subject matter of discussion.
Hapa sijagusia udini, nikijua kuwa Zanzibar over 99% ya wananchi wa Zanzibar ni waislamu.
Na hali hiyo haikuwa issue wakati wa mapinduzi ya 1964 na si issue baada ya hapo.
Hii angle ya kuingiza udini ni la kwako na si vinginevyo.
 
Tatizo lako wewe nikujifanya unajua sana kumbe haujui chochote kinachoihusu Zanzibar na watu wake na badala yake unatuletea stori za waarabu kuwatesa watu weusi.

Story hizi unazikuta kanisani peke yake tena kwa lengo lao maalum ambalo wanalijuwa wao!!

Ukienda kanisa la mkunazini Zanzibar la Anglicans utakuta vinyago vya miti na historian utakayopewa hapo na kanisa nilazima utajenga chuki na waarabu na waislamu kwa ujumla!! Lakini tujiulize kwanini hizo history zimekuja baada ya mauaji ya 1964 (mapinduzi)!!!?? Hawa wachungaji wanasahau kuwa ni mfalme wa kiarabu aliekuwa akiongoza Zanzibar kwa wakati huo ndio aliewapa kiwanja cha kujenga kanisa ambalo linaweza likawa la kwanza au la pili kwa uzee Tanzania.

Sasa hilo soko la watumwa lilikuwa SAA ngapi na ibada SAA ngapi.

Nikweli 99% ya wazanzibar ni waislamu na ndio maana mkoloni mweusi anatumia kila analoliweza ili awadhibiti hawa 99%, tumemsikia lukuvi kanisani akiyasema haya.

Hata hiyo serikali ya umoja wa kitaifa iliyopo sasa katu haimfurahishi mkoloni mweusi na ndio maana katika hotuba nzima ya mh. Magufuli bungeni hakutambua uwepo wa raisi mstaafu wa Zanzibar mh. Karume kwa kuwa kitendo chake cha kukaa na wazanzibar wenzake na kujaribu kutatua matatizo yao kiliwauzi mkoloni mweusi! Huu muafaka wa maalim na kurume katu usingefikiwa kama mkoloni mweusi angalifahamu kabla maana Sera za mkoloni mweusi ni wagawe uwatawale
 
Sorry mkuu, you dont have an issue here, zaidi ya maji moto.
Na pengine ndio kielelezo cha msimamo wa wazanzibari wengi- they actually do not know what their problem is.
 
Ni zanzibar tu mwenyekiti kufanyamaamuzi ya mamlaka asokuwa nayo kisheria.
Ni zanzibar tu walioshinda hawatangazwi.
Ni zanzibar tu koloni la tanganyika
 
Masuala ya muungano hayo, semeni tu bila kumung'unya kuwa hamuutaki muungano.
Hapo hapo mnajenga Mbgala na Tandika!
Halafu muwe wa kwanza kukataa viti huko Dodoma maana kwa msimamo wako mtakuwa mnajaza nafasi za posho tu.
Mkuu
Nakushauri tena unapoishiwa na hoja , usifanye viroja. Angalia uliyaandika kwenye mchango wako. You are going nut, man.
Nani kazungumzia kuvunja Muungano au kujenga na kutokujenga nyumba?
Tume ya Warioba ilikusanya maoni ya wazanzibari kuhusu Muungano. Kwa sababu hoja zimekuishia unajifanya huyajui maoni hayo. Je kuna aliyesema muungano uvunjwe?

Pia Tume ilipendekeza nini kama Muundo mpya wa Muungano?

Kwa muktadha wa hoja yako, eleza wewe unautaka Muungano? Kwa nini unataka Muungano?
Unataka serikali moja? Mbili? Au Tatu?
Je atakaetofautiana na wewe juu ya maoni utakayotoa atakuwa anataka Muungano uvunjwe?

Unajitahidi kuukimbia ukweli lakini wacha nikukumbushe. CCM imeshindwa kupitia kisanduku cha kura huko Zanzibar, badala ya kuleta longolongo, CCM iache demokrasia ichukue mkondo wake.

Nimeona kwenye mchango wako mmoja hapo juu unatahadharisha watu wasitoke kwenye mada lakini angalizo hilo inaonekana halikuhusu wewe. Wewe unajaribu kupindisha maneno na hoja kama umemwagiwa maji washawasha.

Kujengewa Tandika na Mbagala ni faida kwako na CCM wenzako. Mchina atajenga bandari ya Bagamoyo je ni jambo linalokuudhi pia? Unaelewa thamani ya ujenzi huo?

Ukipata nafasi, waulize CCM- Zanzibar je wanataka Muungano wa serikali moja?
Ukipata majibu linganisha na maoni yako kuhusu Muundo wa Muungano unaoutaka wewe.

CCM iache kubaka demokrasia.
 
Back
Top Bottom